Friday, 15 May 2009

UMASIKINI WA WATANZANIA (KAMA UNAVYOONYESHWA KATIKA PICHA YA JUU kwa hisani ya Dr Faustine) UNACHANGIWA ZAIDI NA MAFISADI WACHACHE WASIONYIMWA USINGIZI NA MISHANGAO KAMA HIYO YA BALOZI WA SAUZI.HAWANA MUDA WA KUJALI NANI ANASEMA NINI,ALIMRADI VOGUE ZAO (kama katika picha ya mfano hapo chini) ZINAENDELEA KUWAPA UJIKO MTAANI!YALEYALE YA MTU ANAKUPORA MKEO KISHA ANAMPTISHA MBELE YAKO MAKUSUDI KUKURUSHA ROHO!
Na Claud Mshana

BALOZI wa Afrika Kusini nchini amesema anashangazwa kuona nchi iliyojaliwa rasilimali nyingi kama Tanzania kujiendesha kwa kutegemea misaada kutoka nchi wahisani na marafiki.

Balozi huyo, Sindiso Mfenyana alisema rasilimali zilizo nchini zinaweza kugeuzwa na kuwa tegemeo la misaada kwa nchi nyingine.

Mfenyana alisema hayo wakati akizungumza na wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari jijini Dar es salaam. Mfenyana alisema inashangaza kuona Tanzania ambayo imebarikiwa kuwa na rasilimali za kila aina ikiendelea kutegemea misaada katika uchumi wake.

"Kama rasilimali zilizopo zitatumiwa vizuri kwa maendeleo ya nchi hii na pia kukawa na usawa katika matumizi ya rasilimali hizo, nchi hii ingekimbiliwa na watu wengine kwa misaada," alisema balozi huyo.

Mfenyana alisisitiza kuwa Tanzania haina haja kuhofia wawekezaji kutoka Afrika Kusini, hasa wazungu kwa sababu zama za ubaguzi wa rangi zimeshapita na kwamba kilichopo sasa ni kuona nchi inakuwa na ushirikiano wenye manufaa bila kujali rangi wala historia baina ya nchi za Afrika.

"Ni ajabu kuona mtu anakuwa na wasiwasi kuingia ubia wa kiuchumi na 'Mzungu', pengine ni kutokana na historia iliyokuwepo kabla… inawezekana kuwa vyombo vya habari havikutangaza vya kutosha kuwa vita vya ubaguzi wa rangi vimekwisha," alisema.

"Leo hii mtu mweusi wa Afrika Kusini anakuwa na chuki na mtu mweusi mwenzake kuliko hata Mzungu, jambo hili linaonyesha kuwa enzi za kuchukiana kwa misingi ya rangi imeshapita.

Ni lazima tuendeleze uhusiano wetu kwa manufaa ya nchi zetu." Kwa upande wake, Meneja wa Jukwaa la Wafanyabishara wa Tanzania na Afrika Kusini, ambaye pia ni meneja wa hoteli ya Southern Sun, Adam Fuller alisema kumekuwa na maendeleo chanya ya ushirikiano wa kibiashara kwa nchi hizi mbili.

Alifafanua kuwa tofauti na zamani, Tanzania ilikuwa ikijitenga kiushirikiano na nchi nyingine labda kwa kuhofia ushindani, hivi sasa kuna tofauti kubwa na kuongeza kuwa wataendelea kushirikiana zaidi kwa kutumia fursa zilizopo kibiashara.

Kuhusu tatizo la umasikini nchini humo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo na wimbi la uhalifu, Mfenyana alisema serikali ya nchi yake imejipanga kukabiliana na hali hiyo na tayari hatua madhubuti zimeshachukuliwa kukabiliana na
tatizo hilo.

CHANZO: Mwananchi

INA MAANA BALOZI HUYU HAJUI KUWA RASILIMALI ZETU TAYARI NI MSAADA KWA MAFISADI?NCHI YETU IMEGEUZWA SHAMBA LISILO NA MWENYEWE,WATU WANAJICHUMIA WEE MPAKA WANAKINAI NA KULETA NYODO!INATIA UCHUNGU LAKINI NDIO HIVYO TENA.


0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget