PICHANI,NI MBUNGE WA IGUNGA,ROSTAM AZIZ,AKIKABIDHI KINACHODAIWA KUWA DOSSIER LENYE TUHUMA DHIDI YA MFANYABIASHARA RAGINALDMENGI.ANAYEKABIDHIWA NI AFISA UCHUNGUZI WA TAKUKURU GWAKISA.Picha hii ni kwa mujibu wa gazeti la The African.
HUU NI NI UPUUZI.YAANI HAINGII AKILINI HATA KIDOGO.JAMANI,HIVI LINI MMEWAHI KUONA TAKUKURU WAKIKABIDHIWA USHAHIDI/TUHUMA MBELE YA VYOMBO VYA HABARI AS SEEN IN THE PICTURE ABOVE?
HUU NI NI UPUUZI.YAANI HAINGII AKILINI HATA KIDOGO.JAMANI,HIVI LINI MMEWAHI KUONA TAKUKURU WAKIKABIDHIWA USHAHIDI/TUHUMA MBELE YA VYOMBO VYA HABARI AS SEEN IN THE PICTURE ABOVE?
HUYU ROSTAM AMEKUWA MITHILI YA MUNGU MTU: ALIPOTAJWA TU NA MENGI,MAWAZIRI WAZIMA NA BUSARA ZAO (SOPHIA SIMBA NA KAPTENI MKUCHIKA) WAKALIPUKA KUMTETEA (JAPO SASA WAMEKAA KIMYA ROSTAM ALIPORUDIA KILEKILE ALICHOFANYA MENGI).KISHA TAKUKURU NAO KATIKA HALI INAYOONYESHA NAMNA GANI TAASISI HIYO NI WABABAISHAJI WA DARAJA LA JUU WAKAANDAA MITHILI YA PRESS CONFERENCE YA KUMPOKEA ROSTAM NA KINACHODAIWA KUWA NI USHAHIDI WAKE DHIDI YA MENGI (JAPO KUNA MADAI KUWA WAJANJA WAMEMWINGIZA MJINI KWA KUMUUZIA "CHENI BANDIA"-ISOMEKE DATA FEKI).
HAWA TAKUKURU NI WAZEMBE ZAIDI YA WAZEMBE.HIVI UBABAIKAJI KAMA HUO WALIOFANYA KWA ROSTAM WANGEUELEKEZA KWA KAGODA SI TUNGEPIGA HATUA FLANI?AU WANGEKUWA "FASTA" NAMNA HIYO KATIKA,SIO KUITETEA BALI KUICHUNGUZA IPASAVYO KAMPUNI YA RICHMOND,KWA HAKIKA TUSINGEKUWA HAPA TULIPO SASA.
MBONA WENZETU MNAJIDHALILISHA KIASI HICHO?NI HIZO FEDHA ZA ROSTAM AU NJAA ZENU?THIS IS MORE THAN TOO MUCH.IT'S ABSURD,CRAZY AND UTTERLY NONSENSE.
Kaka. Pole saana kwa haya ukabilianayo nayo. Niliwahi kuuliza tangu mwanzo kuwa kama kuna wenye dhamana ya kutambua na kuwakamata hawa mafisadi, iweje leo hii waje watajwe na Mengi kabla yake? Yaani kama Mengi anafikia hatua ya kuwataja, basi ana (japo) ushahidi (anaoamini) wa kutosha kuwahusisha hawa watu na ufisadi huu. Lakini kama anaweza kuwa nao na wahusika TAKUKURU NA SERIKALI KWA UJUMLA hawana, basi ni afadhali tukabinafsisha hiyo taasisi kwa Mengi. Na swali lisiloulizwa ni kuwa huyo Mengi amepataje taarifa ambazo wengine hawana? Ana mtandao wake wa kusaka habari ana anatumia njia za kifisadi kuzipata taarifa hizo?
ReplyDeleteSasa ona haya yanayotia aibu kwa Takukuru kukabidhiwa ushahidi hadharani. Aibu kuliko maelezo.
Ni upumbavu uliozidi upumbavu wenyewe
Mzee wa Changamoto,yaani changamoto zinazolikabili taifa letu zinaongezeka kila kukicha na sijui hatma yetu ikoje!
ReplyDeleteHATIMA NI VITA, HAKUNA KINGINE, BILA KUTOANA ROHO ZA KIFISADI HAPO HATUENDI POPOTE.
ReplyDelete