Wednesday, 6 May 2009


NADHANI TAFSIRI SAHIHI YA "WORLD'S MOST INFLUENTIAL PEOPLE" INAWEZA KUWA NGUMU KWA LUGHA YETU YA TAIFA.SIJUI TUITE "WATU MAARUFU ZAIDI DUNIANI" AU "WENYE MVUTO ZAIDI" AU...?SINA HAKIKA KAMA INFLUENCE NI UMAARUFU AU MVUTO.ANYWAY,KWA MUJIBU WA ORODHA YA WATU 100 INFLUENTIAL KABISA DUNIANI KWA MWAKA 2009 INAYOANDALIWA KILA MWAKA NA JARIDA LA TIME LA MAREKANI,RAIS PAUL KAGAME AMESHIKA NAFASI YA 13.MARA NYINGI ORODHA HIYO HUPATA PIA UPINZANI NA KEJELI HUSUSAN KUTOKA KWA WAHAFIDHINA WANAOTAFSIRI JARIDA LA TIME NA ORODHA HIYO KUWA NA MRENGO WA KUSHOTO AU KILIBERALI ZAIDI.

"NDANI YA NYUMBA" PAMOJA NA KAGAME,NI MCHANYATO WA WANASIASA KAMA SENETA TED KENNEDY NA WAZIRI MKUU WA UINGEREZA GORDON BROWN,KIONGOZI WA KIYAHUDI MWENYE MSIMAMO MKALI KABISA AVIGDOR LIEBERMAN (Pichani Chini)
NA "MFALME WA UNGA" (COCAINE), JOAQUIN GUZMAN,"PABLO ESCOBAR MPYA" AMBAYE PIA NI MIONGONI MWA WATU MATAJIRI KABISA DUNIANI NA AMBAYE KICHWA CHAKE KIMEWEKWA REHANI YA US$ 5MILLION NA VYOMBO VYA DOLA VYA MAREKANI (Pichani Chini),MCHEZA SINEMA MWENYE MVUTO BRAD PITT,TAPELI LA PONZI BERNIE MADOFF,GWIJI LA "KUSEMA OVYO" RUSH LIMBAUGH,MWANAMUZIKI JOHN LEGEND(Pichani Chini),MWANADADA WA KIZAMBIA DAMISA MOYO (Pichani Chini)
BILA KUMSAHAU RAIS OBAMA NA MKEWE MICHELLE (Pichani chini na Oprah)
NA USUAL SUSPECTS KAMA TOM HANKS,GEORGE CLOONEY,TIGER WOODS NA WENGINEO.

BONYEZA HAPA KUANGALIA ORODHA KAMILI.HONGERA RAIS KAGAME.WANYARWANDA WANA KILA SABABU YA KUJIVUNIA UONGOZI WAKO HASA KWA TAIFA LILILOWEZA KUSIMAMA KIDETE KUTOKA KWENYE MAUAJI YA KIMBARI HADI KUWA HADITHI YA KUPIGIWA MFANO BARANI AFRIKA.ANYWAY,SIE TWAENDELEA KUJIVUNIA AMANI NA UTULIVU WETU UFISADI STYLE!!!

2 comments:

  1. Kagame anastahili kutokana na na rekodi nzuri ya maendeleo kwa nchi yake hasa ukilinganisha na nchi iliyokuwa na matatizo kama yake (jirani yao) na nchi zinazozidi kuisumbua (jirani zake wa kaskazini na magharibi).
    Huyu dada Moyo nimemsoma mawazo yake kuhusu uchumi na kama si matatizo ya uchumi ya kidunia, fikra zake zingefanyiwa kazi zingesaidia sana kuiondoa Afrika katika utegemezi wa misaada ya nje.
    Asante kwa listi.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli uliyosema Da Subi.Thanks for the compliments.

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget