Thursday, 14 May 2009


SOMA HABARI HII KISHA UNGANA NAMI MWISHONI KATIKA KUHOJI LOGIC YA TCRA.


Kusajili simu lazima
:: Ambazo hazitasajiliwa hadi kufikia Desemba kufungwa
:: Serikali, kampuni zote za simu kushirikiana pamoja
:: Usajili kuanza rasmi Julai mosi, lengo kuthibiti uhalifu

Na Debora Sanja

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewataka watumiaji wa simu za mikononi kusajili simu zao kabla ya Desemba, mwaka huu.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Connie Shirima kwa niaba ya Mhandisi wa mamlaka hayo James Kilaba, wakati akiwasilisha mada ya usajili wa kadi za simu kwa wahariri wa vyombo vya habari.

Shirima alisema, kwa wale wote ambao hawatasajili kadi zao za simu, ifikapo Desemba zitafungwa na hawatakuwa na uwezo wa kuzitumia
tena.

“Kazi ya kusajili kadi za simu za mikononi itaanza rasmi Julai mosi, mwaka huu, kwa kuwa wajumbe wote wa mamlaka husika wameshakaa na kujadili ni jinsi gani kadi hizo zitasajiliwa,” alisema Shirima.

Alisema wajumbe wa kamati hiyo ya usajili ni kampuni zote za simu nchini, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka, Idara ya Uhamiaji na TCRA
wenyewe.

Shirima alisema wameamua kushirikisha idara hizo zote, ili kuhakikisha zoezi hilo halikwami kutokana na kuacha kushirikisha idara ambayo ni
muhimu katika usajili huo.

Alisema Tanzania bado haijawa na vitambulisho vya uraia kwa watu wake, lakini vitambulisho mbalimbali vitatumika wakati wa kusajili simu hizo.

“Vitambulisho ambavyo vitatumika katika usajili huo ni kitambulisho cha kazi, leseni ya gari, kitambulisho cha benki, kitambulisho cha kupiga kura, kitambulisho cha bima ya afya, hati ya kusafiria, vitambulisho vya vyuo, vitambulisha vya umoja wa kikundi, na kadi za magari,” alisema Shirima.

Alisema vitambulisho ambavyo vitakuwa havina picha, mteja atatakiwa kupiga picha na kuipeleka kwa ajili ya usajili. Shirima alisema zoezi hilo linawezekana, kwa kuwa kuna nchi nyingi kama vile Afrika ya Kusini na Ufilipino ambako Serikali zimeweza kusajili simu zao za mikononi, japokuwa hawana vitambulisho vya uraia.

Alisema vitendo vya uhalifu wa kutumia simu za mkononi havitakuwapo tena kwa kuwa kila mwenye kadi ya simu atajulikana kutokana na taarifa zake ambazo atakuwa amejaza kabla ya kusajiliwa.

Akizungumzia tatizo la uuzaji wa kadi za simu kiholela, alisema wamiliki wote wa mitandao ya simu watatakiwa kuwasajili wachuuzi wanaouza kadi za simu kwa kuwapa namba maalumu, ambazo zitawezesha kujua mteja amenunua wapi kadi hiyo.

Wale wote watakaokuwa wanauza line za simu barabarani watapewa namba maalumu na fomu ambazo zitamuwezesha mteja kujaza taarifa zake muhimu kabla ya kununua kadi ya simu,” alisema.

Alisema kamati ya usajili imeamua fomu zote atakazojaza mteja kabla ya kununua kadi ya simu zitakuwa zinafanana, ili kuondoa utata ambao unaweza kujitokeza.

Katika fomu hizo, mteja atatakiwa kujaza jina lake kamili, namba yake ya simu, mkoa na wilaya anayotoka, kabila, namba ya kadi ya simu yake na namba ya sehemu ambapo amenunua kadi hiyo.

Vile vile alisema kuna sheria ambayo inaandaliwa kwa ajili ya kuboresha usajili wa simu za mikononi.

Akizungumzia suala la utumiaji wa namba za siri katika kupiga simu, amesema TCRA walishapiga marufuku tangu Machi mosi, mwaka huu.

TCRA imeanza jana kuadhimisha wiki ya Mawasiliano na Habari Jamii Tanzania (WTSD), ambapo jana imeanza na semina kwa wahariri wa vyombo vya habari nchini.

Miongoni mwa mada zilizojadiliwa, ni ujumbe wa mwaka huu wa kuwalinda watoto na utumiaji wa mtandao, shughuli za TCRA na nafasi iliyonayo ya udhibiti, jinsi ya kutumia teknolojia ya kisasa(digital) na usajili wa simu na kadi za simu.

Uzinduzi rasmi wa siku hiyo unafanyika leo katika hoteli ya Ubungo Plaza, ambako mada mbalimbali zitatolewa kujadili jinsi gani ya kumlinda mtoto na matumizi ya mtandao, na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na Teknolojia, Profesa Peter Msolla.

CHANZO:
Mtanzania


HII IMEKAA MKAO WA KURA ZA MAONI YA WAUAJI WA ALBINO.KAMA HUJANIELEWA,NAMAANISHA UTARATIBU ULIOZOELEKA WA KUJA NA MAAGIZO YASIYO PRACTICAL.MAMLAKA YA MAWASILIANO (TCRA) INALETA HADITHI ZA KULAZIMISHA KUSAJILI SIMU ZA MIKONONI.SABABU WANAYOONA YA MSINGI KUTOA AMRI HIYO NI KUPUNGUZA UHALIFU.HII NI SABABU DHAIFU KWA VILE KWANZA,UHALIFU ULIKUWAPO HATA KABLA YA UJIO WA MOBILE PHONES MWISHONI MWA MIAKA YA 90,NA TCRA HAWAJAELEZA LINI WALIFANYA UTAFITI ULIOONYESHA KUWA USAJILI WA SIMU ZA MIKONONI UTASAIDIA KUPUNGUZA UHALIFU. WANASEMA ZOEZI KAMA HILO LIMEWEZEKANA AFRIKA KUSINI NA UFILIPINO (SIO KWAMBA LIMEKOMESHA UHALIFU BALI LIMEWEZEKANA PASIPO VITAMBULISHO VYA URAIA)

ETI WANASEMA BAADA YA USAJILI HUO UHALIFU WA KUTUMIA SIMU UTAKOMA?KWA MIFANO IPI HAI?WHAT IF MTU ATANIOMBA SIMU YANGU,KISHA AKAITUMIA KWA SHUGHULI YA UHALIFU PASIPO RIDHAA YANGU?SI YANAKUJA YALEYALE YA KURA ZA MAONI KUHUSU MAUAJI YA ALBINO AMBAPO BAADHI YETU TULIONYA HATARI YA KURA ZA CHUKI?

LAKINI KUNA SUALA LA MUHIMU ZAIDI YA WHETHER MPANGO HUO UTAFANIKIA AU LA,NALO NI RIGHT TO PRIVACY.NASHANGAA MAKUNDI YA HAKI ZA BINADAMU YAMEKUWA KIMYA KUHUSU SUALA HILI.KAMA SUALA NI KUPUNGUZA ( AU KUTOKOMEZA UHALIFU) TAYARI TUNA MAMLAKA KAMA POLISI LENYE JUKUMU HILO NA SIJAWAHI KUSIKIA LIKIDAI KUWA UHALIFU UNAONGEZEKA KWA VILE SIMU HAZIJASAJILIWA.VILEVILE,JESHI HILO LINAPASWA KUWA NA TEKNOLOJIA YA KU-TRACE SIMU SIMU ZINAZOSHUKIWA KUHUSIKA NA UHALIFU.

HII NI VICTIMIZATION OF WATUMIAJI WOTE WA SIMU IN THE SENSE KUWA KILA MTUMIAJI SIMU NI POTENTIAL CRIMINAL.TUKIRUHUSU SUCH ABUSE OF OUR HUMAN RIGHTS INAWEZA KUPELEKEA FURTHER ABUSES KWENYE MAENEO MENGINE KAMA VILE INTERNET.KWA VILE KUNA TOVUTI ZINATUMIA TEKNOHAMA KUFANYA MAMBO YASIYOSTAHILI SIO EXCUSE KWA MAMLAKA HUSIKA KUZI-CRIMINALIZE TOVUTI ZOTE.IN THE SAME LINE OF THINKING,KWA VILE BAADHI YA WAHALIFU HUTUMIA SIMU KATIKA KUTENDA UHALIFU SIO SABABU YA KU-CRIMINALIZE KILA MTUMIAJI WA SIMU.

NA PENGINE CHA MUHIMU ZAIDI NI USALAMA WA HIZO PERSONAL DETAILS ZITAKAZOHITAJIKA WAKATI WA KUKAMILISHA USAJILI WA SIMU.KAMA MITIHANI INAVUJA HUKO NECTA,FEDHA ZINAIBIWA BENKI KUU (NOT MENTIONING KUIBIWA KWA LAPTOP YA IGP OFISINI KWAKE),KWANINI TUSIHOFU KUWA SIKU YA SIKU PERSONAL DETAILS HIZO ZINAWEZA AIDHA KUIBIWA AU KUUZWA? HIVI KWANINI TCRA HAIZUNGUMZII USALAMA WA DATA HIZO,ITAZIHIFADHI KWA MUDA GANI,NA HATUA ZIPI ZITACHUKULIWA PINDI DATA HIZO ZITAKAPOTUMIKA NDIVYO SIVYO?

HIVI TAASISI ZA HAKI ZA BINADAMU HUKO NYUMBANI ZIKO WAPI?AU ZIKO BUSY NA KUOMBA POSHO KWA WAFADHILI FOR PERSONAL PURPOSES?

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget