Saturday, 9 May 2009


Kibaka aduwaza walinzi Ikulu

2009-05-08 13:51:35
Na Jacqueline Mosha

Mfanyabiashara wa Kariakoo jijini Dar es Salaam, Ally Nasoro (41) amefikishwa mahakamani kujibu shitaka la kuingia Ikulu ya Rais Jakaya Kikwete na kuiba ua moja lenye thamani ya Sh. 5,000, mali ya Ikulu hiyo.

Mshitakiwa huyo alifikishwa mbele ya Hakimu Mwajuma Diwani wa Mahakama ya Mwanzo Kariakoo jijini Dar es Salaam jana, na kusomewa shitaka hilo.

Akisoma hati ya mashitaka, karani wa mahakama hiyo, Caphren Maduhu, alidai mbele ya hakimu Diwani kuwa mshtakiwa alifanya kitendo hicho Mei 2 mwaka huu.

Mahojiano mahakamani hapo yalikuwa kama ifuatavyo:

Karani: Kesi hii ni ya wizi na imefunguliwa na mlalamikaji ambaye ni askari mwenye namba E 4716 Koplo Mnyaga.

Mshitakiwa katika shitaka hili ni Ally Nasoro, anaishi eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam na anakabiliwa na kosa wizi alilofanya Mei 2, mwaka huu, saa 4:24 usiku huko Ikulu ya Rais.

Hakimu: Mshitakiwa umesikia mashitaka ya kosa lako, unajibu nini?

Mshitakiwa: Mimi nilikuwa napima uwezo wa akili wa walinzi waliowekwa Ikulu ili kumlinda Rais wa nchi, maana isije ikawa wako wako tu kumbe hawana hata uwezo wa kumlinda.

Hakimu: Ile ni sehemu ya heshima na inalindwa iweje wewe upate wazo la kutaka kuingia ndani, ulikuwa na nia gani?

Mshitakiwa: Nilichokigundua siku hiyo ni kwamba kumbe naweza kuingia Ikulu kiulaini bila hata ya kuguswa na mtu. Kwanza nilipofika pale getini nilitaka kufahamu kama naweza kufanikiwa kuingia, hivyo, nilisimama kwa saa nne nje ya geti bila hata kuulizwa chochote na walinzi. Baadaye nilifanikiwa kupata mwanya wa kuingia ndani na kweli niliingia kiulaini bila hata 'shobo'.

Hakimu: Ilikuwaje mpaka ukaiba hilo ua?

Mshitakiwa: Nilipolichukua lile ua na kulibeba ndipo walinzi waliniona na baada ya kuniona walinzi hao walibaki wakitetemeka huku mimi nikiwa nimeshikilia ua na ndipo waliponikamata na kunichukulia hatua. Kama naweza kuchukua ua si ningeweza hata kuingia ndani kwa Rais kiulaini? Yaani walinzi wamelala pale. Hawako makini kama nilivyodhani.

Hakimu: Unajibu nini kuhusu shitaka la wizi huo?

Mshitakiwa: Si kweli, sijaiba ua.

Hakimu Diwani aliahirisha kesi hiyo mpaka itakapotajwa tena mahakamani hapo Mei 11 mwaka huu. Mshitakiwa alipelekwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ambayo ni kuwa na wadhamini wawili.

CHANZO: Nipashe

SOMEONE SOMEWHERE IS NOT UP TO THE TASK.AWALI,RAIS MSTAAFU MWINYI ALIZABWA KIBAO HADHARANI,A COUPLE OF WEEKS AFTER MSAFARA WA JK KURUSHIWA MAWE HUKO MBEYA.SUPPOSE HUYU KIBAKA HAD INTENDED TO,NOT TEASE THE GUARDS WITH A STOLEN FLOWER BUT, CAUSE HARM TO THE PRESIDENT.....

SECURITY SLACKNESS

2 comments:

  1. I'M SICK AND TIRED OF BEING SICK AND TIRED.
    Viongozi wa polisi wanaibiwa kompyuta zao, na sasa walio chini yao wanashindwa kumlinda Rais.
    tHAT'S TOO MUCH

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli ni jambo la kusikitisha sana. Na inakatisha tamaa kama siku moja tutakuwa na maendeleo Tanzania yetu

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget