Saturday, 15 May 2010

Kwa hakika baadhi ya kauli za Rais wetu Jakaya Kikwete zinachanganya kupita kiasi.Juzijuzi tu alisaini kwa mbwembwe sheria tuliyoambiwa imelenga kudhibiti rushwa katika chaguzi.Tukiweka kando suala la wasaidizi wake kumwingiza mkenge kwa kuchomekea vipengele kinyemela,sambamba na mapungufu lukuki katika utekelezaji wa sheria hiyo (kubwa likiwa uswahiba kati ya CCM ya Kikwete huyohuyo na mafisadi),uamuzi wa kuwa na sheria hiyo ulileta faraja kidogo kwamba angalau mkuu wa nchi sasa anaanza kuikabili rushwa kwa vitendo badala ya maneno na ahadi tupu.

Sasa kabla hata sheria hiyo haijapata nafasi ya kutumika ipasavyo,JK kaja na hadithi mpya.Kwa mujibu wa vyombo vya habari,Rais amewaeleza viongozi wa dini kuwa suala la takrima kwenye chaguzi ni gumu kulidhibiti.Kama huelewi vizuri maana ya takrima basi naomba nikugamishe kuwa hiyo ni jina la kistaarabu (polite name) la rushwa au hongo wanayotoa wagombea kwa kisingizio cha 'ukarimu'.
Kinachonifanya nishindwe kumuelewa JK ni hiki: ina maana wakati anaipigia chapio sheria anayoamini itadhibiti rushwa kwenye chaguzi alikuwa hafahamu kuwa takrima (ambayo ni rushwa) ni ngumu kudhibitiwa? Au tuseme JK haamini kuwa takrima ni rushwa na ndio maana iliharamishwa?Na je kama takrima ni ngumu kudhibitiwa kwahiyo inakuwa halali?Je kiongozi wetu huyu haoni kuwa mkanganyiko anaozua unaweza kupelekea mvurugano baada ya uchaguzi ambapo wagombea watakaoshindwa kutokana na uwezo wao duni kumudu kutoa takrima wakikimbilia mahakamani,watoa rushwa (takrima) watatumia kauli ya JK kuhalalisha kuwa walichofanya ni sehemu ya utamaduni wetu wa ukarimu ("kama alivyobainisha Rais tarehe 14/05/2010)?

Habari kamili kuhusu kauli hiyo ya JK soma HAPA na HAPA.

Related Posts:

  • Ah,JK Vipi Mbona Haeleweki?Kwa hakika baadhi ya kauli za Rais wetu Jakaya Kikwete zinachanganya kupita kiasi.Juzijuzi tu alisaini kwa mbwembwe sheria tuliyoambiwa imelenga kudhibiti rushwa katika chaguzi.Tukiweka kando suala la wasaidizi wake kumwingiz… Read More
  • Kauli Hizi za JK ni HatariKatika siku za hivi karibuni,Rais Jakaya Kikwete amekuwa akitoa kauli ambazo kwa namna flani zinaweza kupelekea uvunjifu wa amani.Sote tunakumbuka hotuba yake kali aliyotoa mbele ya walioitwa 'wazee wa jiji la Dar es Salaam' … Read More
  • Jini Ndani ya Chupa...Likitoka LimetokaNadhani unamfahamu Christina Aguillera,na kama unamfahamu basi ni dhahiri utakuwa unakumbuka 'singo' yake ya kwanza kabisa Genie in a Bottle (Kama huukumbuki basi cheki video hii hapa).Ushaikumbuka?Well,lengo la makala hii si… Read More
  • JK Anatania,Tendwa Anatania,Na Siasa Zetu ni Utani MtupuOfkoz,Mtukufu Rais Jakaya Kikwete alikuwa anatania alipotetea rushwa hadharani kwa kudai takrima haikwepeki.Ndio,Rais alikuwa anatania,na ndo maana,Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa amekaririwa na magazeti kadhaa akimtet… Read More
  • REDET: Pinda Mchapakazi Zaidi Ya Kikwete na SheinMatokeo ya utafiti uliofanywa na Mradi wa Utafiti na Elimu na Demokrasia Tanzania (REDET) yanaonyesha kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ni mchapakazi zaidi ya 'bosi' zake,Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Ali Mohammed Sh… Read More

1 comment:

  1. Huyo ndiyo rais mwenye "personality mbili za uongozi...Kwanza ndiyo mtu wa mwisho kupitisha sheria za nchi na pia ndiye anyeshabikia kuzivunja kwa sababu yeye ndiyo mtu mwenye wazifa wa juu kabisa ktk mahamuzi ya serikali ya Jamhuri ya Tanzania....Angalia Chenge, Mkapa wote wanafurahia taratibu hizo zake kwa sababu ndizo zinawafanya kuwa huru mtaani kufurahia maisha ya uvunjaji sheria bila kuadhibiwa na sheria zilizopo..

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget