Tuesday, 27 July 2010


Mtunzi wa kitabu hiki maridhawa si mwingine bali ni mchambuzi na mwandishi mahiri wa makala,Mwalimu Nkwazi Nkuzi Mhango,Mtanzania mwenye makazi yake nchini Kanada.Licha ya ualimu na uandishi wa habari,Mhango pia ni mwanaharakati wa haki za binadamu.Miongoni mwa safu maarufu za Mwalimu Nkwazi (pichani chini) ni zile zinazopatikana katika gazeti la Tanzania Daima,ambapo hutumia jina la MPAYUKAJI MSEMAOVYO.Kadhalika,mwandishi huyu ni hodari katika fani ya kublogu,na "uwanja wake" unafahamika kama Free Thinking Unabii .Vilevile,unaweza kusoma makala za Mwalimu Nkwazi katika jarida la The African Executive
Usikose nakala ya kitabu hiki ambacho kinakuja wakati mwafaka kabisa kwa Watanzania waliochoshwa kuona nchi yao ikigeuzwa "shamba la bibi" na mafisadi wanaopita huku na huko "kuomba ridhaa yetu" warejee madarakani kutufisadi zaidi.

9 comments:

  1. Umenifumbua macho. Sikuwa nimewahi kumsoma huyu jamaa. Baada ya kusoma blogu yake nimemkubali mia kwa mia. Naweza kupata jinsi ya kuagiza book hili hasa kwa mtu kama mimi aishiye ughaibuni. Chahali fanya hima nipate copy please

    ReplyDelete
  2. Big up mzee kwa kutuhabarisha. Hiki kitabu nilipewa nyuzi yake na jamaa yangu mmoja aishie Arusha. Anasema ni funika sana na hatari kama kitafanyiwa kazi. Kudos Chahali.

    ReplyDelete
  3. Nondo hii usiambiwe. Nimeipata pale Samora. Ingekuwa wakati wa mchonga kisingetoka na jamaa angeishia lupango bila shaka. Kazi pevu ile mbaya. Nilipata habari zake kupitia rafiki yangu padri Karugendo. Usiambiwe jamaa ni hatari.Natamani mtalii wetu Jakaya Kikwete apate na asome ajione alivyovuliwa mavazi.

    ReplyDelete
  4. Mimi naishi Sichuan hapa China nimeishapata kopi yangu. Kazi hii ni pevu.Nilipata habari zake kupitia blogu ya profesa Matondo Nzulilima wa Marekani. Hakina matusi wala kuzungusha bali kutoa dozi baada ya dozi. Mbwa kweli kala mbwa. Good job.

    ReplyDelete
  5. bila shaka wanene hawatakizuia kifike kwenye mikono ya wadau wanaohitaji kukisoma.

    Safi sana!

    ReplyDelete
  6. Wanene wetu wa sasa ni weupe. Hawasomi zaidi ya kujikita kwenye ujasiriamali. Hivyo hii nondo inaweza kupeta na kupetuka bila wasi wasi.

    ReplyDelete
  7. Mimi ni mwanasheria. Nimepata kopi ya kitabu hiki. Ni kizuri na mapinduzi makubwa katika uandishi nchini hasa staili iliyotumika kufikisha ujumbe. Kazi safi sana ukiachia makosa madogo madogo ya kisarufi na lugha.

    ReplyDelete
  8. Wow! Baada ya kukusoma hapa kwenye ulingo nimeingia nyikani na kupata kitu hiki usiambiwe!

    ReplyDelete
  9. Nami baada ya kukitafuta nimebahatika kupata nakala yake ya hichi kitabu.

    Wowowo!!!!!!!!!Bila shaka huyu mpiganaji mwenzetu amesema kweli tupu na ndiyo tunachohitaji kwa sasa, nategemea waandishi wengine watawakilisha mawazo yao kwenye maandishi pia ili tuendelee kujitambua wapi tulipo, wapi tulipotoka, na wapi tunakwenda na njia zipi na mbinu sahihi za kutufikisha huko tunakotaka tufike kihalali.

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget