Monday, 1 April 2013
Well, unless wewe msomaji ni mgeni wa Tanzania yetu, na unless hufahamu kuwa April Mosi ni siku geni, tunaweza tu kutamani kusikia Rais wetu akichukua hatua kali dhidi ya wazembe waliopelekea vifo kadhaa vya Watanzania wenzetu.
Ni hivi, kama ilivyokuwa kwa milipuko ya mabomu Mbagala naGongo la Mboto, na kama ilivyokuwa kwa mtukio ya kusikitisha ya kutekwa na mateso kwa Dkt Ulimboka na Kibanda, na mauaji ya mwandishi Mwangosi, zitaundwa tume, wajumbe wa tume watatafuna fedha za bure, na hatimaye karatasi zitakazotumika kuchapisha ripoti za tume itakayoundwa kufuatia ajali hiyo mbaya kabisa ya kuporomoka jengo zitaishia kufungiwa maandazi kama si chapati au vitumbua.
Hii ndio Tanzania yetu, na leo ni April Fool's Day
Samahani kama kichwa cha habari hii kimekupa matumaini hewa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment