Wednesday, 17 April 2013




 Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Frans Timmermans akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika makazi rasmi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo jijijini The Hague na kufanya naye mazungumzo rasmi.

Ina maana Waziri Mkuu wa Uholanzi hakuona umuhimu wa kumkaribisha Rais Kikwete yeye mwenyewe hadi akamtuma Waziri huyo wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo? Zingatia maneno yenye herufi nyekundu: tukio hilo limetokea kwenye makazi ya Waziri Mkuu huyo.Hii ni fedheha!

Ikumbukwe hali kama hiyo ilijitokeza katika ziara ya Rais Kikwete nchini Ufaransa ambapo badala ya kupokewa na Rais Hollande, alipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Maendeleo wa nchi hiyo Pascal Canfin.

Bottom line is, hata kama angepokelewa na viongozi wakuu wa nchi hizo, bado ukweli unabaki kuwa Kikwete atabaki kwenye kumbukumbu za Tanzania (na pengine duniani kwa ujumla) kama Rais anayependa mno safari za nje licha ya safari hizo kuwa mzigo mkubwa kwa walalahoi wa Tanzania.

Kwa mujibu wa takwimu za mtandao wa Jamii Forums, hadi kufikia mwezi huu wa April 2013, Kikwete amesafiri mara 365 (sawa na idadi ya siku katika mwaka mmoja) tangu aingie madarakani mwaka 2005. 

Mwaka juzi, gazeti lililokuwa mwiba kwa serikali ya Kikwete hadi likafungiwa la Mwanahalisi liliripoti kuwa safari hizo za Kikwete zinachangia mno kukausha fedha huko Hazina

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget