Wednesday, 17 April 2013



Kwanini ninasema Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi a.k.a Mzee Ruksa AMELIKOROGA? Hebu soma msimamo wake wa awali kuhusu suala la kuchinja

Mwinyi: Kila mtu ruksa kuchinja • ASEMA IMANI NI NAFSI, HATA KULA CHURA SAWA
 na Asha Bani
RAIS mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amerejea kauli yake kuhusu mgogoro wa udini akisema kila mtu ana haki ya kuchinja kutokana na imani yake ilimradi tu asivunje sheria za nchi. 
Mwinyi alisema anashangaa kuona watu wakigombania kitu kidogo kama kuchinja ilihali Tanzania ina utamaduni wa amani siku zote na kwamba kila mtu ana imani yake ya dini anayoiamini. 
Kiongozi huyo mstaafu alitoa msimamo huo jana jijini Dar es Salaam katika kongamano juu ya utamaduni wa Kiislamu Afrika Mashariki ambapo Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji.
“Imani ni nafsi ya mtu na haitakiwi kumlazimisha kula nyama iliyochinjwa na mwenzie. Na kama unaona aliyochinja mwenzio ni kibudu basi usile chinja yako, kula hata ukitaka kula chura, mjusi, konokono, kula utakacho ruksa ilimradi tu usiingie katika jinai,” alisema. 
Mwinyi alikumbusha kuwa hata wakati wa utawala wake majaribu kama hayo yaliwahi kumtokea, lakini alijitahidi kuweka sawa kwa kumwambia kila mtu ale kile anachofikiri ni chakula bila kumlazimisha mwenzake. 
Alisema Watanzania wamezaliwa ardhi moja na kwamba kinachotakiwa ni kuwa na misingi ya kuvumiliana, na kwamba sifa ya Uislamu ni pamoja na kuwa na uvumilivu.
Aliongeza kuwa Uislamu si kufanya vurugu kama inayotafsiriwa na makundi ya wanaotaka kuvunja amani ya nchi kwa kutumia jina la dini ya Kiislamu.

Sasa linganisha msimamo huo wa awali na hicho alichoongea Mzee Ruksa kwenye video hapo juu.

Yawezekana Rais huyo mstaafu ameamua 'kulamba matapishi yake' (kusema 'amefafanua' ni kupotosha ukweli kwani alichoongea kwenye video ni tofauti kabisa na alichoongea awali) baada ya kupata shinikizo kutoka kwa Waislam wenzie. Au albda nafsi tu imemsuta.

Nitajadili kwa kifupi suala hili kama Mtanzania na pia kama Mkristo. Kama tunakubaliana kuwa Tanzania haina dini, lakini Watanzania wana dini,basi kila dini inapaswa kuheshimu uhuru na haki za wenzao. Kama sheria za kidini zinawataka Waislam kuchinja, na zile za Wakristo haziwalazimishi kuchinja, basi kila mmoja afuate kile kinachoelekezwa na dini yake.

Mzee Ruksa anaposema Biblia ipo kimya kuhusu suala la kuchinja haimaanishi kuwa ukimya huo unatoa ruhusa kwa Wakristo kulazimishwa kufuata matakwa ya Waislam au wapagani.Msimamo wake wa awali ulikuwa sahihi kabisa: kila mtu afuate imani yake, na hata mtu akitaka kula chura aachiwe uhuru wa kufanya hivyo.

Kimsingi, Mwinyi amechochea moto kwenye mjadala huo japo katika video hiyo anaonekana kama angependa Watanzania waishi kwa amani na umoja. Lakini haiwezekani kuishi kwa amani na umoja iwapo dini moja inafanywa kuwa yenye haki zaidi ya dini nyingine. Haki ya Waislam kuchinja shurti iendane na utambuzi wa haki ya Wakristo kutolazimika kuchinja. Hatuwezi kuzungumzia haki za Waislam lakini wakati huohuo tukapuuza haki za Wakristo.

Hivi ikitokea Wakristo wanataka kuchinja nguruwe itabidi watafute Musilam wa kuwacvhinia ilhali nguruwe ni haramu kwa Waislamu?

Sorry Mzee Ruksa, hii flip-flop imeturejesha kwenye tatizo lile lile la udini: kuangalia upande mmoja wa imani na kupuuza upande mwingine. 



 

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget