Thursday, 13 January 2011


Katika moja ya maeneo machache ambayo Watanzania tumepiga hatua ya kuridhisha ni fani ya kublogu.Ni vigumu kufahamu idadi kamili ya mabloga wa-na blogu za- Kitanzania (ndani na nje ya nchi) lakini haihitaji sensa kutambua kuwa idadi ni ya kuridhisha.Iwapo idadi hiyo inaendana na matarajio ya wasomaji,hilo ni suala jingine.

Kwa haraka haraka,ni rahisi pia kutambua blogu za picha (zinazoambatana na habari) ndizo zinazotamba zaidi.Pengine ni kwa vile,kama wasemavyo, "PICHA MOJA INAWEZA KUWAKILISHA MANENO ELFU MOJA".Lakini inawezekana pia kuwa wasomaji wetu wengi wako bize,na hawana muda wa kusoma makala ndefu kwenye blogu kama hii.Kadhalika,na hili nalitamka kwa uangalifu mkubwa,huenda kuna kundi dogo la wenzetu ambao kwa mtizamo wao,kusoma ni mithili ya self-inflicted third degree torture.

Blogu hii ina umri wa miaka mitano kasoro miezi mitatu (ilizaliwa mwezi April 2006).Ukiangalia idadi ya wasomaji wanaoitembelea (visitors),unaweza kudhani imeanzishwa miezi michache tu iliyopita.Kuna blogu kadhaa zenye visitors milioni kadhaa,na baadhi yao zina umri haba kulinganisha na wa blogu hii.

Unaweza kudhani inakatisha tamaa.Hapana.Binafsi,naamini nina kundi dogo la wasomaji "tunaoelewana".Yaani namaanisha wasomaji ambao kwa kiasi kikubwa wanaafikiana na dhima kuu ya blogu hii: harakati za haki kwa jamii na mapambano dhidi ya uhujumu uchumi,ukiukwaji haki za binadamu na utawala bora.Haimaanishi kuwa wasomaji hao wanaoiamini blogu hii wanaafikiana na kila nachoandika.Hapana.Kuna nyakati tunatofautiana kimtazamo,na wengi wao huwa huru kunikosoa au kutoa mawazo tofauti na yangu.Of course,kuna nyakati,baadhi ya wasomaji huamua kutumia lugha isiyofaa kuwasilisha ujumbe/mtizamo wao.Hizo ni changamoto katika maisha kwani ukiona kila kitu kinakwenda sawia basi huenda kuna walakini mahala flani.

Of course,ingependeza kuona blogu hii nayo ina visitors milioni 5 au zaidi.Lakini what if kati ya hao,ni asilimia ndogo tu wanaochukulia kwa makini ujumbe uliomo bloguni hapa?Kwangu,idadi ya visitors hainusumbui kwa vile naamini nina kundi dogo la wasomaji makini ambao wanaichukulia blogu hii kama kiwanja chao cha mazoezi kwa ajili ya mapambano ya kusaka uhuru wa pili wa Tanzania,sambamba na kuhabarishana kinachojiri kwenye korido za watawala wetu.

Enewei,kisa cha kuandika post hii ni mfadhaiko nilioupata siku chache zilizopita pale nilipotuma post (niliyoichapisha hapa) kwa bloga mwenzangu wa picha-habari.Kuna nyakati huwa naona umuhimu wa kufikisha ujumbe wangu kwa wasomaji wengi zaidi,hususan wale wapenda picha lakini sio habari.Na kwa kutambua kuwa blogu ya rafiki yangu huyo inatembelewa na wasomaji wengi kuliko hii,na pia kwa vile alishatoa wazo la kumtumia angalau makala moja kwa wiki,nikaona hakuna ubaya wa kumtumia post hiyo.

Cha kusikitisha,sio tu hakuichapisha bali amekuwa akikwepa hata meseji nazomtumia (sio kumkumbushia kuhusu post husika bali mawasiliano yetu ya kawaida tu).Nafahamu kuwa baadhi ya "waswahili" wanapata wakati mgumu sana kuwa wawazi na wakweli kusema "samahani,hii haiendani na hadhi ya blogu yangu".Mhusika anadhani kukaa kimya kutapelekea mie kusahau ombi langu kwake,na ishu itamalizika kienyeji.

Najua kwanini bloga huyo aliogopa kuchapisha post niliyomtumia.Anaogopa mamlaka.Lakini uoga wa nini wakati kilichoandikwa si mawazo yake?Binafsi,kuna nyakati huwa natumiwa habari au matangazo mbalimbali,na ninachofanya ni kuyatundika sambamba na kubainisha chanzo au mtumaji.

Ushirikiano ni muhimu kwa mabloga hasa kwa vile yawezekana mwenzangu hana nilichonacho,nae anacho kile ambacho mie sina.Wingi wa idadi ya visitors isiwafanye  baadhi ya "mabloga wenye majina makubwa" (kama huyu rafiki yangu nayemzungumzia hapa) wajisahau kuwa sisi kama wanadamu ni wanyama tunaohitaji sana ushirikiano (social animals).Na sio lazima ushirikiano huo uwe kwenye kublogu pekee bali mambo mbalimbali yanayotugusa binafsi au jamii kwa ujumla.

Enewei,simlaumu ndugu yangu huyo kwa vile kama ilivyo katika blogu hii,yeye pia ana haki yake ya kikatiba kutochapisha kitu anachoona hakiendani na maudhui ya blogu yake.Lakini,japo pia ni haki yake ya kikatiba,kufanya dharau si jambo la kiungwana.Kunifahamisha kuwa "aah ndugu yangu ile kitu naona inaweza kuniletea matatizo..." sio kauli ngumu,hasa ikitolewa kwa njia ya meseji.

Well,wakati tunaanza mwaka mpya ni vema kufanya inventory ya kuangalia watu walio na umuhimu kwako na wale ambao wanaongeza tu idadi.Namshukuru ndugu yangu huyu kwa kunirahisishia zoezi hilo.



5 comments:

  1. Evarist,
    Well said.Kama kuna ambayo nimeyapata katika hili ni kwamba bloggers wa kitanzania bado hatuthamini vya kutosha suala la ushirikiano.Suala la kusaidiana kusambaza habari.Pili kuna uoga.Kuna kulinda maslahi binafsi kuliko kuweka mbele maslahi ya umma ambayo bila shaka yanaweza kupatikana kwa kuanzia kwenye habari na hivyo "knowledge".

    Bado kazi ya kuelimishana sisi wenyewe kama bloggers ni muhimu.Nafurahi kwamba umeliweka hili wazi.Ni changamoto kwetu sote.Blogging for social change.Naipenda mada hiyo

    ReplyDelete
  2. Shukrani Jeff.Siku zote nimekuwa naiangalia Bongo Celebrity (BC) kama mfano wa kuigwa na bloga wengine hasa kutokana na unavyohamasisha na kudumisha ushirikiano kati yako,sie bloga wenzio na wasomaji.I wish kila bloga mwenye jina angejifunza kutoka kwako.Tuna safari ndefu,lakini natumaini tutafika.Asante sana.

    ReplyDelete
  3. Jeff hupaswi kuandika haya unayoandika kwani nawe ni mmojawapo wa woga na watu wasiopenda ushirikiano. Sitataja jina langu. Lakini ukisoma ukisoma ujumbe huu utajua ni lini uliwahi kushindwa kutoa ushirikiano na ukandengua kana kwamba uliotufanyia vile hatukuwa na kitu. Ulipokuja kugundua kuwa kumbe uliita almas jiwe it was indeed too late. Anyway na wanafiki ni watu na huwezi kuwajua kwa sura zao.Nawe ni mmojawapo. Kama umetubia okay. Kama bado una kazi.

    ReplyDelete
  4. Chahali now you are boring. I sent a comment regarding Msangi's double standard. To my surprise, you have decided to slaughter that comment.I did not write the same to attack your friend but to remind him to be fairly even to others.
    Thanks and you can even kill this one shall you deem it fit.

    ReplyDelete
  5. Evarist,
    Asante kwa mchango wako.Bila shaka wewe umeangalia mifano halisi na ndio maana ukaandika ulichoandika.

    Ningefurahi sana kuingia kwenye "mdahalo" na Anonymous kuhusu anachokizungumzia hususani kwenye "uoga".Lakini kwa sababu Anonymous huenda sambamba na "uoga",basi naomba nihifadhi maoni yangu kwa leo.Ila kama kuna dukuduku la msingi,tafadhali Anonymous usisite kuniandikia...e-mail yangu ni bongocelebrity at gmail dot com.Pamoja.

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget