Mkutano mwingine wa wawekezaji umeanza leo jijini Dar es Salaam.Mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano mingine inayopigiwa debe kwa nguvu kuhusiana na umuhimu wa wawekezaji kwa uchumi wetu.
Naamini wengi wet bado tunakumbuka vuguvugu la Mkutano wa Sullivan.Baadaye ukafuatiwa na mkutano mkubwa wa mambo ya uchumi (economic forum).So far,hayo yamebaki kuwa matukio tu ambayo kwa upande mmoja yamewaachia baadhi ya wajanja utajiri wa kutosha baada ya kupewa tenda za chakula,malazi,vifaa,nk huku Watanzania wakiendelea kubaki masikini (na hapo tukiweka kando adha ya usafiri kutokana na barabara kufungwa kwa ajili ya misafara ya waheshimiwa).
Wakati viongozi wetu wakituhadaa na mikutano ya kila mwaka ya wawekezaji,kuna umuhimu wa kufanya uchambuzi wa kina kuhusu suala zima la uwekezaji.Kama uwekezaji mkubwa uliopo hadi sasa hauna manufaa kwa Mtanzania wa kawaida,ni miujiza gani itapelekea wawekezaji wapya walete mabadiliko?
Suala moja la msingi linalopuuzwa na watawala wetu ni ukweli kwamba wawekezaji sio taasisi za hiari za kutuletea maendeleo yetu.Hawa ni wafanyabiashara ambao miaka michache tu iliyopita tuliwaita kila aina ya majina-from watangulizi wa ukoloni to mabeberu.Of course dunian imebadilika,lakini mabadiliko hayo sio yawe at expense of wazawa au wenye nchi.
Tunaingia gharama kubwa kuvutia watu wa aina ya Richmond,Dowans,wezi wa madini huko migodini,na wababaishaji wengine.Wengi wa wanaoitwa wawekezaji wanakuja na briefcase tupu zikiwa na mikataba tupu lakini ikishasainiwa,na baada ya miaka michache wanaondoka wakiwa na mamilioni kwenye akaunti zao-huku wakiacha,kwa upande mmoja, mafisadi wameongeza idadi ya nyumba ndogo zao,mahekalu yao na magari yao ya kifisadi,na upande mwingine walalahoi wakikodolea ardhi yao iliyoachwa mashimo matupu baada ya raslimali yote kuibiwa.
Tunakaribishaje wawekzaji kabla ya kutengeneza sera na sheria mwafaka za kutuwezesha kunufaika na ujio wa wawekezaji hao?Na uwekezaji wa aina ya "kupangisha nyumba kisha mwenye nyumba kulala mtaani" ni uhayawani usiopaswa kuendelea.
Tunafahamishwa wizi unaofanywa na baadhi ya makampuni ya simu ambayo kila baada ya muda flani yanabadili majina ilhali huduma zao mbovu zikiendelea kuwa zile zile za kuchefua.
Tunakaribisha wawekezaji wakati baadhi ya hao waliopo wanapata hadi jeuri ya kuchoma moto wazawa (rejea tukio la Kigamboni)lakini vyombo vya dola vinachelea kuchukua hatua zinazostahili.
Viongozi wetu wanapaswa kuwa makini na kurejea yaliyotokea nchini Afrika Kusini hivi karibuni ambapo wazawa waliamua kuelekeza hasira zao kwa wageni wakiamini kuwa ndio chanzo cha matatizo yao ya kila siku japo ukweli ni kwamba chanzo cha tatizo ni uongozi mbovu wa watawala wa nchi hiyo.
Tumeshuhudia jana baadhi ya wakazi wa Kigamboni wakiamua kupambana na wawekezaji japo kama ilivyo kawaida waliishia kudhibitiwa na polis,na huenda wakafunguliwa mashtaka huku mwekezaji aliyeua akiachwa "anakula kuku kwa mrija".
Nikirejea tukio hilo la Kigamboni,nilifadhaika kusoma tweet ya Mbunge wa jimbo hilo akieleza bila aibu kuwa "maandamano yamekuwa SUPPRESSED na CULPRITS watachukuliwa hatua za kisheria".Huyu ni mwakilishi wa watu haohao waliompoteza mwenzao kwa kuchomwa moto na mwekezaji!
Anyway,ujio wa wawekezaji ni habari njema kwa mafisadi kwani unapanua fursa za kupata teni pasenti na vijizawadi vya likizo huko ughaibuni,huku the so called wawekezaji wakigeuza nchi yetu kuwa shamba la bibi.
0 comments:
Post a Comment