Wednesday, 27 April 2011


Niliposoma stori hii almanusura abiria wenzangu kwenye basi wadhani nimepandwa na uchizi kwa kicheko.Yaani mgodi kugundulika shuleni,kisha walimu na wanafunzi kuachana na elimu na kuchangamkia kusaka utajiri kwa kuchimba madini...hahahaha,Lol! (Picha ya juu haihusiani na habari hii bali taswira tu ya wanafunzi wa shule ya msingi).



CHANZO: Tanzania Daima.

What about kujiburudisha na video hii ya Kanye West "Diamond Are Forever"?

Mgodi wa dhahabu waibuka shuleni
• Walimu, wanafunzi waacha masomo, wachimba madini

na Makunga Peter, Bukombe

MGODI mpya wa machimbo madogomadogo ya dhahabu umeibuka katika Shule ya Msingi Nganzo, wilayani Bukombe, mkoani Shinyanga na kufanya viongozi wa wilaya kwa kushirikiana na mwalimu mkuu wa shule hiyo kuufanya kuwa mradi wao wa kujiingizia fedha.

Machimbo hayo yaliyoibuka takriban miezi miwili iliyopita yamesababisha shughuli na masomo katika shule hiyo kusuasua kutokana na walimu na wanafunzi kujiingiza katika shughuli za uchimbaji huku wakisahau kuzingatia masomo hali ambayo imesababisha utoro mkubwa wa wanafunzi.

Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho yalipo machimbo hayo, Boniphace Mashebela, alisema kuwa machimbo hayo madogo kwa sasa yanamilikiwa na kamati ya shule na kijiji lakini yanaendeshwa kwa ridhaa ya Ofisa Elimu wa Shule za Msingi, Fides Munyogwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Kuruletera Majige, kwa kigezo kuwa machimbo hayo yapo katika eneo la shule.

Mmoja wa wachimbaji wadogo wanaoendesha shughuli za uchimbaji katika eneo hilo, Masamaki Kambale, alisema wao wapo hapo kisheria na si wavamizi kwani wao hufika na kuripoti ofisini kwa mwalimu mkuu pamoja na mtendaji wa kijiji na wao hugawiwa viwanja kabla ya kuzamisha maduwara yao.

Masamaki alisema kuwa kila duara linasajiliwa kwa sh 40,000, ambapo fedha hizo hupewa mwalimu mkuu na mtendaji wa kijiji na pindi duara linapofikia kuanza uzalishaji kila utoapo mifuko 10 ya mawe kati ya hiyo miwili ni mali ya viongozi hao wa wilaya hiyo.

Alisema kuwa kwa upande wa kamati ya shule na mtendaiji wao hutoza ushuru wa sh 1,000.

Kwa upande wake Ofisa Madini wa Wilaya ya Kahama na Bukombe, Medard Msengi, alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya shutuma hizo alisema mgodi huo mpaka sasa ofisi yake haiutambui na kuomba kuongozana na waandishi wa habari hadi katika eneo hilo kujionea.

Ofisa huyo alipofika alijionea kuwa machimbo hayo yanaendeshwa kinyume cha sheria, kwani kipimo kutoka shimo hadi shimo kinatakiwa kiwe futi 10 kwa 10 lakini hayo yapo futi mbili hadi tatu, hali ambayo inaweza kusababisha maafa ya watu kufunikwa na kifusi wakati wowote wa uchimbaji.

Aidha, alitoa ushauri kuwa ni bora machimbo hayo yakafungwa kwa kuwa yapo katika eneo la shule, hali ambayo inachangia wanafunzi kutosoma vizuri na walimu kukimbilia kufanya biashara hiyo ya uchimbaji, hali ambayo itadhoofisha maendeleo ya elimu katika shule hiyo kwani hayana uataratibu wowote.

Alisema katika eneo hilo hakuna vyoo, hakuna mtaalamu anayetambulika katika ofisi yake ambaye anashughulikia madini katika eneo hilo maarufu kama waangalizi wa madini ili kufanya hali ya usimamizi katika eneo hilo kuwa rahisi na kudhibiti wanafunzi na walimu kufanya kazi hiyo.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe alipoulizwa kwa njia ya simu, alisema kuwa kweli machimbo hayo yapo katika eneo la shule na kuongeza kuwa tayari ameshatoa taarifa kwa mkuu wa wilaya ya maandishi, ila alikanusha kuwa yeye hahusiki katika kuchukua mifuko katika eneo hilo na kuiuza kama inavyosadikiwa

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget