MBUNGE KALALA FOFOFO: Hawa ndio wa kulipwa posho nono za mamilioni? |
Pengine umeshasahau neno UNYONYAJI.Neno hilo lilikuwa maarufu sana nyakati za Ujamaa na Kujitegemea.Katika kipindi hicho tulikuwa tukihamasishwa sana kupamana na unyonyaji na wanyonyaji.Kimsingi,unyonyaji ni sawa na wizi au ujambazi.Kuvuna usichopanda,au kuvuna zaidi ya ulichopanda,tena kwa njia zisizo stahili.
Baada ya kifo cha Ujamaa,unyonyaji ukahalalishwa,si kwa Watanzania wote bali kwa wateule wachache.Hivi ukiangalia nukuu hiyo hapo chini kutoka gazeti la Mwananchi,kuna justification gani kwa mbunge kulipwa fedha zote hizo ilhali kuna mamilioni ya Watanzania wanaolipa kodi na hawana uhakika wa mlo wao wa kila siku?
Hivi Mtoto wa Mkulima Mizengo Pinda anaweza kweli kusimama mbele ya Watanzania akawaambia mamilioni haya wanayolipwa wabunge ni jambo lisiloepukika?Kwanini serikali yetu inaruhusu wizi huu wa mchana kweupe?
Na kwanini wafadhili wetu wanaendelea na usingizi wao wa pono kuachia huku fedha wanazotusaidia kwa maendeleo yetu zikiishia kuendeleza vitambi na nyumba ndogo za waheshimiwa?
Enewei,soma nukuu ifuatayo,na nina hakika utaafikiana nami kuwa kuna haja ya kukomesha ujambazi huu uliohalalishwa na serikali
Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili umebaini kuwa malipo ya wabunge yamegawanyika katika sehemu nne; mshahara ambao ni Sh2,300,000 kwa mwezi, posho ya Ubunge kila mwezi ambayo ni Sh5 milioni, posho ya kujikimu (Per-Diem) kwa Sh80,000 wawapo nje ya majimbo yao kikazi na posho ya vikao (sitting allowance) kwa siku Sh70,000 kwa kila mbunge.Posho ya Ubunge ya kila mwezi ambayo ni Sh5 milioni ni kwa ajili ya mafuta, matengenezo ya gari, malipo ya dereva na wasaidizi wa mbunge.Kwa maana hiyo, kwa kawaida mbunge hulipwa Sh7.3 milioni kila mwezi kabla ya kukatwa kodi na wawapo Dodoma na Dar es Salaam kwa ajili ya vikao vya kamati na Bunge au mikoani kwa ajili ya kukagua shughuli zilizopo chini ya kamati zao, hulipwa kiasi cha Sh150,000 kila siku; Sh70,000 kwa ajili ya vikao na Sh80,000, kwa ajili ya kujikimu.Kwa maana hiyo Bunge linatarajiwa kutumia kiasi cha Sh1.788 bilioni kwa ajili ya kugharimia vikao 73 vya Bunge la bajeti iwapo wabunge wote 350 waliopo watahudhuria vikao hivyo.Kwa hesabu hizo kila mbunge katika mkutano wa Bunge la bajeti anatarajiwa kuondoka na kikita cha Sh5.1 milioni mbali na Sh5.58 milioni ambazo ni malipo kwa ajili ya kujikimu (Per diem), fedha ambazo ni mbali na mshahara wake kwa mwezi na posho ya ubunge.
CHANZO: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment