Sio siri kwamba upole wa Watanzania ni miongoni mwa sababu kuu za mabaya mengi yanayotokea huko nyumbani.Na kama kuna suala linalosikitisha kuhusu mwamko wa Watanzania kudai haki zao ni tatizo la mgao wa umeme sambamba na ubabaishaji wa hali ya juu wa serikali na Tanesco katika kushughulikia tatizo hilo.
Sasa hivi,mitandao ya jamii ya Twitter na Facebook imetawaliwa na malalamiko ya Watanzania wengi kuhusu mgao.Wengine wanaishiwa na uvumilivu na kuishia kuitukana Tanesco,kana kwamba matusi hayo yatarejesha umeme.Wengine wamekuwa wakipeana taarifa kuhusu maeneo ambayo "Tanesco wameshachukua umeme wao".Kwa kifupi,kinachosikika zaidi ni manung'uniko,lawama,vilio na hata matusi.Cha kusikitisha ni kwamba hakuna dalili yoyote kutafsiri malalamiko hayo into vitendo.
Sio kama nawasimanga ndugu zangu.I really feel you lakini ukweli mchungu ni kwamba kelele zenu haziwezi kumaliza tatizo hilo.Kinachohitajika ni kudai haki kwa nguvu.By "nguvu" simaanishi vurugu bali kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha serikali na Tanesco wanawajibika.Mgao utaendelea milele iwapo Watanzania wataishia kulalamika tu.Hakuna miujiza katika kuleta mabadiliko.Either watu wajitoe muhanga kudai haki yao kama walipakodi au waendelee kuteswa na mgao.
Bahati nzuri,wenzetu nchini Senegal wanatuonyesha namna gani matatizo yanayoathiri nchi yanavyoshughulikiwa na umma.Nisieleze kwa maneno yangu bali naomba usome habari ifuatayo:
Associated PressDAKAR,Senegal: Maelfu ya waandamanaji wameingia mitaani katika mji mkuu wa Senegal kupinga kukatika umeme mara kwa mara.Maandamano hayo ni tukio la tatu la vurugu nchini humo ndani ya wiki.Wananchi wenye hasira walivamia ofisi za shirika la umeme la Senelec,jijini Dakar baada ya maandamano ya kupinga kukatika kwa umeme kwa muda mrefu.Watu kadhaa walishambulia majengo ya serikali hapo jana.Wanadaia kuwa baadhi ya maeneo yamekuwa yakikosa umeme kwa masaa 24 au zaidi.Kama ilivyo kawaida kwa vyombo vya dola barani Afrika,askari wa kikosi cha kutuliza ghasia walipambana na waandamanaji kwa kutumia maji na mabomu ya machozi.Msemaji wa polisi hakuweza kuthibitisha idadi ya waliojeruhiwa katika ghasia hizo.Alhamisi iliyopita,vurugu kubwa ziliibuka kupinga mpango wa mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo
Uchaguzi ni wenu Watanzania wenzangu.Mwendelee kulalama huku Serikali na Tanesco wakiendelea kuwasanifu (mgao wa umeme hauwagusi kwa vile aidha wana jenereta zinazojazwa mafuta na hela yako mlipakodi au maeneo wanayoishi hayakatwi umeme kutokana na unyeti wake) AU muige mfano wa wenzetu wa Senegal.Hakuna njia ya mkato katika kutatua matatizo sugu yanayosababishwa na watendaji wasiotimiza wajibu wao.It's now or never!
0 comments:
Post a Comment