Wakazi wa Uingereza leo Jumatano watapata fursa ya kuona kupatwa kwa mwezi ambapo mwezi unatarajiwa kugeuka "mwekundu kama damu" kwa takriban dakika 100.Hata hivyo,wanasayansi wa taasisi ya mambo ya anga ya Marekani (NASA) wanaeleza kuwa wakazi wa Ulaya hawatofaidi vizuri tukio hilo kwani linatarajiwa kutokea kabla ya mwezi kuchomoza (kwa majira ya Ulaya)
Tukio hilo linatarajiwa kuanza saa 12 na dakika 24 jioni kwa muda wa majira ya joto hapa Uingereza (1824 British Summer Time) na kuendelea hadi saa 6 usiku (0000 BST) lakini kwa Uingereza litaanza kuonekana saa 3 na dakika 19 usiku (2119 BST).
Wakazi wa maeneo ya nusu ya mashariki ya bara la Afrika,eneo la Mashariki ya Kati,Asia ya Kati na magharibi mwa Australia wataweza kuliona tukio zima (yaani dakika hizo takriban 100 za kupatwa kwa mwezi).Hata hivyo,wakazi wa Marekani hawatoliona tukio hilo kwa vile litatokea majira ya mchana kwa mida ya huko.
Kijiografia,asili ya mwanga wa mwezi ni mionzi ya jua.Tukio la kupatwa kwa mwezi ni pale Dunia,Jua na Mwezi zinapokuwa mstari mmoja,na kivuli cha Dunia kinaangukia kwenye Mwezi kamili.Uwekundu kama damu katika tukio hili la leo ni matokeo ya miale ya jua kupita Duniani kisha kuangukia kwenye uso wa mwezi.
0 comments:
Post a Comment