Tuesday, 19 July 2011


Rais Kikwete kutembelea Afrika Kusini 
Monday, 18 July 2011 21:28

Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete, jana alianza ziara ya kihistoria ya kidola nchini Afrika Kusini, ikiwa ni ziara ya kwanza ya aina yake, kufanywa na Rais wa Tanzania katika nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Rais Kikwete anafanya ziara hiyo kwa mwaliko wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ambaye utawala wake umekuwa uhusiano wa karibu na Tanzania, tangu aliposhika madaraka ya kuongoza taifa hilo kubwa kiuchumi kuliko mengine, katika Afrika.

Rais Kikwete na ujumbe wake unaojumshia pia mkewe, Mama Salma Kikwete, uliondoka nchini jana mchana kwenda Pretoria, kwa ziara hiyo ya siku nne.Pamoja na kwamba marais wa Tanzania waliomtangulia Rais Kikwete wametembelea Afrika Kusini mara nyingi kwa shughuli mbalimbali, lakini hakuna kiongozi aliyepata kualikwa kufanya ziara rasmi, ya kiserikali ama ya Kidola, tangu nchi hiyo ilipoingia katika mfumo wa demokrasia mwaka 1994.

Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, Rais Kikwete na ujumbe wake, watapokelewa rasmi leo asubuhi katika Jumba la Serikali, mjini Pretoria.Tayari Rais Zuma na mkewe walikwishajipanga kwa sherehe za makaribisho zitakazofuatiwa na mazungumzo rasmi ya Kiserikali kati ya Tanzania na Afrika Kusini.

Mazungumzo hayo, yatafuatiwa na utiaji saini wa mikataba na makubaliano katika nyanja mbalimbali kati ya nchi hizo mbili.Baadaye, viongozi hao wawili watahutubia mkutano wa waandishi wa habari na baada ya hapo, Rais Kikwete atatembelea Uwanja wa Uhuru akiandamana na Rais Zuma.

Mchana viongozi hao watahudhuria chakula cha mchana kikiwashirikisha pia wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika Kusini ambao watazungumza na kuelezea umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya nchi hizo mbili.Jioni, Rais Zuma ataandaa dhifa ya kitaifa kwa ajili ya Rais Kikwete na ujumbe wake .

Keshokutwa, Rais Kikwete na ujumbe wake watakwenda Cape Town, ambako miongoni mwa mambo mengine ujumbe huo utatembelea Kisiwa cha Robben ambako wapigania uhuru maarufu wa Afrika Kusini, akiwamo Rais Mstaafu Nelson Mandela, walifungwa kwa miaka mingi na makaburu. Rais Kikwete atarejea nyumbani keshokutwa asubuhi.

CHANZO: Mwananchi 

LABDA AKIREJEA KUZURURA TATIZO LA UMEME LITAKUWA LIMEPATA UFUMBUZI. 

1 comment:

  1. Hatuna rais hapa. Amekuja kufanya utalii ikulu, sijui anaraha gani kufanya sherehe za ndugu zake, huku taifa lipo kwenye msiba mkubwa wa giza.

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget