Saturday, 30 July 2011


Mitandao ya jamii ya Facebook na Twitter imetengeneza kizazi kinachoendekeza umimi kupita kiasi kiasi kwamba watu hawajali masuala mengine huku wakiwa na tamaa kama watoto wadogo kuona watu wanasema mazuri kuhusu wao,picha zao,wanayoandika kwenye mitandao hiyo,nk.

Kuendelea kuwepo kwenye mitandao hiyo kwa muda mrefu kunamwacha mtumiaji akiwa na mgogoro wa kujitambua (identity crisis),tamaa ya kutambulika katika namna ileile mtoto mdogo anamwambia mzazi wake, "Mama,nimefanya hivi."

Baroness Greenfield,profesa wa taaluma ya madawa (pharmacology) katika Chuo Kikuu cha Oxford,anaamini kuwa kukua kwa urafiki wa mtandaoni-sambamba na matumizi makubwa ya michezo ya kompyuta-vinaweza kupelekea kuuchanganya ubongo.

Hii inaweza kusababisha upungufu kwenye kukazani mambo ya muhimu,hitaji la kutamani kusifiwa na uwezo mdogo wa mawasiliano yasiyohitaji kutumia maneno (non-verbal communication) kwa mfano kumwangalia mtu usoni wakati wa maongezi.

Zaidi ya watu milini 750 duniani wanatumia mtandao wa Facebook kuonyeshana picha na video na mara kwa mara hubandika maelezo kuhusu mienendo na mawazo yao.

Mamilioni pia wamejiunga na mtandao wa Twitter ambao huwawezesha watumiaji kusambaza ujumbe mfupi na picha kuhusu wao wenyewe.

Baroness Greenfield,mkurugenzi wa zamani wa taasisi ya utafiti ya Royal Institution alisema, "kinachonipa wasiwasi ni ile hali ambapo unaweza kutarajia mtu atawaza au kusema nini ambayo ni hali ya kawaida huko Twitter."

"Kwanini mtu ahitaji kujua umekula nini wakati wa kifungua kinywa?Inanikumbusha jinsi mtoto mdogo anavyosema, 'mama angalia ninachofanya' "

"Ni kama mgogoro wa kujitambua.Kimsingi,hali hii inaufunga ubongo kwenye kuhusisha wakati/muda"

Mwanataaluma huyo alidai kuwa baadhi ya watumiaji wa Facebook wanajisikia wanapaswa kuwa "watu maarufu wadogo wadogo" (mini celebrities) ambao wanaangaliwa na kunyenyekewa na watu wengine kila siku.

"Wanafanya vitu vinavyoendana na Facebook kwani njia pekee wanayoweza kutumia kujitambulisha kwa umma ni kwa kuwafahamisha watu wengine kuhusu kinachoendelea kwenye maisha yao."

"Ni kana kwamba watu wanaishi katika dunia isiyo halisi bali dunia ambayo kinachomata ni nini watu wanafikiria kuhusu wewe au kama wanaweza kubonyeza kwenye picha au ulichoandika," alisema Profesa huyo.

"Fikiria kuhusu madhara kwa jamii ikiwa watu wanajali zaidi kuhusu nini watu wengine wanafikiria kuhusu wao kuliko nini wanachofokiria kuhusu wao wenyewe."

Mawazo ya mwanazuoni huyo yaliungwa mkono na Sue Palmer,mtaalam wa fasihi andishi na mtunzi wa vitabu,ambaye alisema kuwa wasichana hususan wanaamini wao ni bidhaa ambayo lazima iuzwe kwenye Facebook.

Alisema: 'Watu walizowea kuwa na picha ya kuchora (zinazowaonyesha wao) lakini sasa tunaweza kujichora wenyewe mtandaoni.Ni kama kuwa mshiriki kwenye shoo yako mwenyewe ya TV ambayo umeiunda na kuiweka hadharani kwa dunia kuiona.'

CHANZO: Habari hii imetafsiriwa kutoka gazeti la Daily Mail


0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget