Thursday, 7 July 2011


Nasikitika kuwafahamisha kuwa baba mzazi Mzee Philemon Chahali amepata ajali mbaya asubuhi hii huko Ifakara.Amegongwa na pikipiki ambazo ndio usafiri mkuu wa huko.Kwa mujibu wa habari nilizonazo hadi muda huu,hali yake ni mbaya,ambapo licha ya kuvnjika mguu pia ameumia kichwani.Kibaya zaidi ni kwamba umri wake ni kwenye miaka ya 80 kwa hiyo mshtuko tu wa ajli unaweza kumwathiri sana.

Basi naomba kutumia fursa hii kuomba sala zenu.Sie Wakristo tunaamini kuwa wanapojumuka wengi kufanya sala basi Mungu naye anakuwepo.Natumaini kwa sala zenu na za familia yetu Mungu atamjalia baba apone na kurejea katika hali yake ya kawaida.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.Asanteni 

8 comments:

  1. Pole MKUU!

    Na nakutakia upone haraka Mzee Philemon Chahali !

    ReplyDelete
  2. Pole sana kaka Chahali na familia yote,Mungu yu pamoja na tuko pamoja katika maombi.

    ReplyDelete
  3. Tuko pamoja kwenye maombezi ili baba yetu aweze kupona haraka.

    ReplyDelete
  4. Asanteni sana,Malkiory na La Princessa

    ReplyDelete
  5. tunamtakia kila la heri aweze kupona haraka

    ReplyDelete
  6. Rejea Maandiko matakatifu tunafundishwa kuwa hakuna linaloshindikana kwa Mungu hivyo wote kwa pamoja tunajongea mbele ya Mungu kwa unyenyekevu na kumwombea mzee wetu Philemon Chahali aweze kupona haraka na kuendelea na shughuli za maisha..AMEN!

    ReplyDelete
  7. Mungu mwenye nguvu, asiyeshindwa na lolote, kwa hakika atamponya mzee wetu Chahali na kumpa nguvu za kuendelea na majukumu yake. Tupo pamoja katika kumuombea mzee wetu

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget