Tuesday, 5 July 2011


Nimekutana nayo huko Jamii Forums.For the time being,taarifa hii inabaki kuwa tuhuma tu hadi hapo itakapothibitishwa.

Wana Jf Mm nimefikia hapa hoteli inayoitwa AFRICA TULIP hapa Arusha mbunge wa CCM Viti maalum kutoka mbeya,Mary Mwanjelwa amekamatwa akiwa ameiba Mataulo,Vikapu vidogo ambavyo huwekwa maua chooni wafanyakazi wa hapa wanadai tukio hili ni la pili baada ya mwezi uliopita kufanya tukio la aina hiyo aliondoka salama wafanyakazi wakakatwa mshahara leo wakati ana check out wafanyakazi waliamua kumsachi na kweli wakakuta ameiba.Hili ni tukio la aibu ameaibisha nchi, bunge na chama chake. Wafanyakazi wa hapa leo wanadai kwamba mabinti wawili mwezi Jana walikatwa kiasi cha shilingi laki 2 nilikua na wazungu wamesikitika sana baada ya kufahamu kuwa huyu ni mbunge.Wanajf nimesikitika nikasema nanyi muipate taarifa hii ni aibu kwa Taifa,Fatilieni ni tukiop la Leo hapa Hotelini ni AIBU NI AIBU NI AIBU DUH Wana Jf nimefatilia Mara ya kwanza alifikia chumba namba 14 akafanya wizi wa soup dish,wizi wa mara ya pili ni room namba 20 miongoni mwa vitu alivoiba ni Pambo la Kitanda,Marekebisho ni kwamba aliiba siku ya Jpili si leo.Naomba kuwasilisha.

3 comments:

  1. Mwehh kazi ipo mwizi ni mwizi tuu hata akija kuiba kwako akishindwa hata makaa ataiba tuu,loohhh Aibu kubwa!!!!!

    ReplyDelete
  2. Hii imenikumbusha kisanga kilichonipata kwenye mwaka 1994 katika mbuga ya Serengeti. Tuliondoka Mwanza, kwa safari ya Arusha, tukiwa wa-Swahili wawili watatu na wazungu hivyo hivyo, katika gari letu. Tulilala kwenye hoteli moja pembeni ya mbuga.

    Asubuhi sana, bado na kagiza, tukaingia zetu safarini. Kuja kwenye kituo ndani ya Serengeti, tukapigwa stopu na mgambo na kuambiwa ni lazima tusachiwe. Kisa? Hotelini tulikolala imeripotiwa kuwa taulo haionekani.

    Kwa hivyo, wote tulipigwa sachi ya nguvu kwenye mabegi yetu. Hamna cha m-Swahili wala mzungu, wala cha profesa gani sijui. Amri moja. Taulo haikuonena. Tukaruhusiwa kuendelea na safari.

    ReplyDelete
  3. Itabidi tuwasamehe wachukue tu sitting allowances bado haijaondolewa na mambo ni haya. Je ikiondolewa? Lakini mwizi ni mwizi tu nakumbuka kuna mtoto wa tajiri mmoja alikua anaiba nguo mall na dollar stores.

    Lakini anaweza akasema kuna mtu kamset up tena Arusha? CCM!!!!

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget