Wednesday, 31 August 2011


Natumai Muwazima wa Afya Njema na Happy Eid kwa Ndugu zetu waislam wote hapo kazini, Samahanini sana kwa usumbufu tunaomba Msaada wenu mtusaidie kutoa taarifa hiyo hapo chini ya juu ya mabadiriko ya jina la website yetu na pia jina la Radio. Natanguliza Shukkrani zangu. Kazi Njema.

TAARIFA YA MABADILIKO YA JINA NA LINK YA TONE INTERNET RADIO KWENDA TONE ONLINE RADIO
Tone Multimedia Company Limited inapenda kuwapa taarifa wananchi wote popote Duniani kuwa tumefanya mabadiliko ya jina la Radio pia jina la Tovuti ambapo mala ya kwanza ilikuwa inaitwa Tone Internet radio na Jina la Tovuti lilikuwa ni www.toneinternetradio. blogspot.com, Kutokana na Sababu za kimsingi za kuingiliana kwa mtandao na Radio moja iliyopo USA inakwenda kwa jina la Tune Internet Radio ndio sababu iliyo tupelekea kubadilisha  jina na kuzaliwa kwa jina jipya la Tone Online Radio ambapo tovuti yake sasa itakuwa ni www.toneonlineradio.blogspot. com na ikumbukwe pia Tone Online Radio ni Radio inayo tumia internet Pekee hatuna Frequency za aina yoyote. asanteni sana atakae pata link hii ampatie na mwenzake. Kwa pamoja tunaendelea kuleta maendeleo ya mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.
Natanguliza Shukrani kwa niaba ya Uongozi,
Imetolewa na,
Joseph Mwaisango
Mkurugenzi wa Mawasiliano
Tone Multimedia Company Limited.

KUSIKILIZA TONE ONLINE RADIO BOFYA HAPA:  www.toneonlineradio.blogspot. com

Monday, 29 August 2011



Raymond Kaminyoge
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imeshusha bei ya mafuta kuanzia leo.Kwa hatua hiyo, bei ya ukomo ya petroli kwa Mkoa wa Dar es Salaam sasa itakuwa Sh2,070, huku dizeli ikiwa Sh1,999 na mafuta ya taa Sh1,980. Bei ya ukomo wa bidhaa hiyo itatofautiana kulingana na umbali wa maeneo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu alisema hiyo ni kutokana na kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo katika soko la dunia.Alisema ikilinganishwa na bei ya zamani, petroli imeshuka kwa Sh44.55 sawa na asilimia 2.11 huku dizeli ikishuka kwa Sh31.99 sawa na asilimia 1.57 na mafuta ya taa yakishuka kwa Sh25.62 sawa na asilimia 1.28.Mnamo Agosti 2, Ewura, ilishusha bei ya mafuta.

ZAIDI SOMA HAPA
Petroli ilishuka kwa Sh202.37 kwa lita ambayo ilikuwa ni sawa na asimilia 9.17, dizeli kwa Sh173.49 sawa na asilimia 8.32 na mafuta ya taa kwa 181.37, sawa na asilimia 8.70 hali iliyosababisha vurugu na uhaba wa bidhaa hiyo.

Lakini, siku 11 baada ya kushusha bei hiyo, Ewura ilipandisha tena bei ya mafuta kutokana na kile ilichodai kuwa ni kupanda bei katika soko la dunia na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania na kusababisha Bodi ya mamlaka hiyo kubanwa na Baraza la Mawaziri.

Thursday, 25 August 2011






BY COSMAS MLEKANI

Chama cha Madaktari nchini (MAT) kimesema tiba inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapila, kwa njia ya kikombe kwa ajili ya kutibu magonjwa sugu, imeleta maafa makubwa kwa wagonjwa.

Makamu wa Rais wa MAT, Dk. Primus Saidia, alitoa tamko hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana suala zima la magonjwa yasiyoambukiza na tiba mbadala.

Alisema kuwa wagonjwa wengi baada ya kunywa kikombe cha Babu waliacha kunywa dawa za magonjwa yaliyokuwa yakiwasumbua na kusababisha wengi wao kupooza, kufa na wengine hali zao kuzidi kuwa mbaya.

“Ni vyema wananchi walio wagonjwa wa shinikizo la damu, kisukari, anemia na magonjwa mengine wakafuata ushauri wa madaktari badala ya kulaghaiwa na wachache,” alisema Dk. Saidia bila kufafanua zaidi.

Alisema umma wa Watanzania umekuwa ukilaghaiwa kwa tiba mbadala na kuacha kutumia dawa za hospitali hivyo kuongeza ukubwa wa tatizo na wanapokimbilia hospitali tayari hali zao zinakuwa mbaya.

Dk. Saidia alisema ili dawa iweze kutumika hufanyiwa utafiti kwa kati ya miaka 10 hadi 15.

Naye Katibu Mkuu wa MAT, Dk. Richard Kabangira, ambaye ni daktari bingwa ya tiba wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, alisema: “Serikali yetu haisikilizi wana taaluma, mfano Babu wa Loliondo utafiti uliofanyika pale ni wa dawa kutokuwa na madhara kwa binadamu na sio kutibu magonjwa.” alisema Dk. Kabangila na kuongeza:

“Hospitali ya Rufaa ya Bugando ilipokea wagonjwa wengi wa kisukari baada ya kutoka Loliondo kufuatia wagonjwa hao kuacha kunywa dawa walizopewa hospitalini.”

Alisema waliwasiliana na wanachama wao nchini kote kufuatilia hali za wagonjwa waliokuwa wamekwenda kwa Babu kupata kikombe na waligundua kwamba waliokuwa wanatumia dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi (ARV), shinikizo la damu, kisukari na hata saratani waliacha dawa baada ya kunywa kikombe cha Babu.

Alisema pamoja na watu kadhaa kutoa ushahidi kuwa wamepona kwa dawa hiyo, utafiti uliofanywa na MAT, umegundua kuwa hakuna hata mtu mmoja aliyepona baada ya kunywa dawa ya Babu.

Alisema watumiaji wa ARV walipungua kama ilivyo kwa hao wengine, lakini baada ya muda hali zao zilikuwa mbaya wengine walikimbilia hospitalini lakini kwa kuwa walikuwa wamevuruga mtiririko wa tiba, walipata madhara makubwa.

Dk. Kabangira alisema MAT ilimwandikia barua Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii juu ya hatari ya tiba ya Babu, na kutoa ushauri wao, lakini ulipuuzwa kwa sababu za kisiasa.

Kufuatia hali hiyo, MAT imetoa wito kwa Serikali na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuwaeleza wananchi ukweli ili wasiangamie huku wakieleza kusikitishwa kwao kutokana na tiba hiyo kutumika kisiasa.

Mchungaji Mwasapila alianza kutoa tiba hiyo mapema mwaka huu na kusababisha maelfu ya wananchi kutoka pembe zote za nchi na nje ya nchi kukimbilia nyumbani kwake katika kijiji cha Samunge, Loliondo katika Wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha kupata tiba hiyo dhidi ya magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kisukari, Ukimwi, saratani na shinikizo la damu.

Viongozi mbalimbali wa madheheu ya dini nao walikuwa miongoni mwa maelfu waliokwenda Samunge na kupata kikombe huku wakitoa ushuhuda kwamba wamepona kwa dawa ya Mchungaji Mwasapila maarufu kwa jina la Babu.

Safari ya kwenda Samunge ilikumbana na changamoto ya barabara mbovu zilizosababisha misongamano na kuilazimisha serikali kuingilia kati kupanga utaratibu pamoja na kusaidia kuboresha miundombinu.

Chama hicho leo kinafanya mkutano wao mjini Mwanza, suala la tiba ya Babu linatarajiwa kuibuka katika mkutano huo unaowakutanisha wanachama wake. SOURCE: NIPASHE




Sharing this story may save some life,may touch someone's life in a similar related problem,may bring hope to hopeless situation.Yawezakua si wewe na unaweza kuchukulia just simple.ila yaweza kumgusa mwenzio na kupelekea ku save maisha yake..
tumekua tukiamka kila leo na kutembea , unaweza kujiona una nguvu na afya tele bila ya kujijua kuwa kuna ugongwa unakula ndani kwa ndani,
au unaweza kutokewa na hali isiyoya kawaida ya hafla ila ukapuuzia na kuipa kisogo,waweza kugundua tatizo kwa mtoto wako ndugu yako,jirani yako au mtu yeyote 
yule wa karibu bali ukajenga woga au  ukazarau na kutokutilia manane hali yake,bila ya kujua kuwa ukimya wako unazidi kuhatarisha maisha ya mwenzako huyo.

Kila kiungo kina u.muhimu katika mwili wa binaadamu ila siku ya leo napenda kugusia zaidi kwenye  Macho.
CONE SHAPE YA CORNEA

KERATOSCONUS 
 Ni jina kutoka Greek na ni  miongoni mwa magojwa ya macho.na naweza kuitafsiri kama hali ya kuendelea ambayo inafanya muundo wa kawaida wa cornea ambao ni curve kwenda kwenye muundo wa cone.

 Ukijiuliza chanzo au sababu ya maradhi haya jibu ni kuwa hakijulikani ingawa wana sayansi wamejaribu kuleta vyanzo tofauti.
Wapo wanaosema ni urithi na mazingira yanachangia.Keratoconus huathiri mtu mmoja kwenye watu zaidi ya 2000.ingawa kwa hivi sasa maradhi haya yanakua zaidi.

Back to my story nilipokua na umri wa miaka 4 nilianza kupata tatizo la macho na baada ya kupelekwa hospital nilishauriwa kuanza kutumia miwani

Jambo hili halikuungwa mkono na mama angu na ikambidi ajaribu kutafuta njia na ushauri kutoka kwa madaktari mbalimbali..na ndipo aliposhauri badala ya kuvaa miwani nijaribu kutumia tiba mbalimbali na vyakula vitakavyonisaidi hadi umri wangu utakaposogea mbele
nilipofika std 5 hakukuwa na jinsi tena bali ni kurudi hospital na kuanza kuvaa miwani kwani tayari macho yangu yalishaanza kupoteza uwezo wa kuona bila ya masaada huo.

Sikuwa napenda kuvaa miwani kwani yalikua yakinikosesha raha na kunizuia kushiriki katika michezo mbalimbali shuleni na badala ya takecare of myself inanibidi ni takecare of my glasses,haikua rahisi.


ASANTE REA KWA MAKALA HII NZURI.KWA NIABA YA WASOMAJI WA KULIKONI UGAHIBUNI TUNAKUTAKIA HERI NYINGI KATIKA SIKU HII UNAYOSHEREHEKEA KUZALIWA KWAKO.MWENYEZI MUNGU AKUZIDISHIE KILA LILILO JEMA NA PIA TUNAKUTAKIA SWAUM NJEMA.

Tuesday, 23 August 2011



PICHA ZOTE HIZI ZIMEPIGWA KATIKA KIKAO CHA BUNGE KINACHOENDELEA HUKO DODOMA.HIVI WAZIRI MZEMBE KAMA HUYU ANAYEDIRIKI KULALA OVYO OVYO HADHARANI  (BUNGENI) AKIWA OFISINI KWAKE SI NDIO ANAJIFUNIKA NA SHUKA KABISA.JE CHANZO CHA KULALA LALA OVYO KAMA TEJA NI UCHOVU NYAKATI ZA USIKU (ATUELEZE ANAKESHA AKIFANYA NINI),MARADHI KAMA SLEEPING SICKNESS AU "TEJA"?

JE INAWEZEKANA WASSIRA ALIKWENDA KWA BABU WA LOLIONDO KUSAKA TIBA YA SLEEPING SICKNESS?


KIONGOZI MCHOVU KAMA HUYU ANAPASWA KUSTAAFISHWA KWA MANUFAA YA UMMA.LAKINI INAELEKE KULALA HADHARANI NI TATIZO LINALOANZIA NGAZI ZA JUU KABISA

 NA LIMESAMBAA MIONGONI MWA VIGOGO,KAMA PICHA ZIFUATAZO ZINAVYOONYESHA (MAJI HUFUATA MKONDO)








ENEWEI,HEBU PATA UHONDOMWINGINE WA WACHAPA USINGIZI HAWA.WANASEMA RAHA YA USINGIZI IPATE MLALAJI









Monday, 22 August 2011


Imetumwa na mdau Kato Lukaija

Wapo watu wanoamini kwamba pakipatikana suluhisho la matatizo ya biashara na uchumi kati ya bara na Zanzibar, basi kero za muungano zitakua zimekwisha. Hawa wanafanana na viongozi wetu wanaoamini kwamba muungano wa kiuchumi wa Afrika mashariki ni atua itakayotosheleza kuleta muungano wa kisiasa na kiutamaduni .Kwa mtazamo huu, uchumi ndio msingi wa kila jambo, liwe la kitamaduni,kisiasa au kitaifa. Na ndio maana nguvu zinaelekezwa zaidi kwenye diplomasia ya uchumi.

Lakini Muungano wetu,pamoja na kuunganisha uchumi wetu kwa matumizi ya sarafu moja,bado umegubikwa na hali ya kutosikilizana.Hali imekua hivyo kwa muda mrefu. Kwa hiyo kero zake,kama mijadala mingi inavyoonesha,haisababishwi na matatizo ya uchumi peke yake. Kuna tatizo la utata wa historia yenyewe ya muungano.

Kuna historia mbili za Muungano. Watu wa bara wanaona Muungano ni matokeo ya Mapinduzi ya Zanzibar yalioundoa utawala wa kitumwa wa Waarabu. Lakini nje ya madarasa rasmi ya historia hiyo,wapo vijana wanaharakati wa Zanzibar, kama Harith Ghasany,mwandishi wa KWAHERI UKOLONI,KWA HERI UHURU. Wanaharakati hawa wanadai kwamba Mapinduzi ya Zanzibar ni tunda la usuda ya Nyerere na kanisa dhidi ya waislamu na waarabu wa Zanzibar.Hivyo Muungano unaonekana kama ukoloni.

Hali hii inahitaji Wazee wakae na kukubaliana kuandika historia moja.  Wafanye kama Rais Kagame. Pamoja na kuangaikia uchumi,Kagame amehakikisha kwamba historia ya kweli ya mauaji ya 1994 ndio inayofundishwa na watu wote.Kagame anajua kwamba mtu haishi kwa mkate tu,ila kwa kila neno litokalo kwa bwana. Kwa hiyo vijana tunaomba wazee waandike historia moja tu. Wazee  wakisimamia historia moja tu, Muungano wetu utapona.

                             ------Kato Lukaija,  P.O.BOX 10351, DAR ES SALAAM.
                                         



Taarifa ifuatayo imetumwa na mwananchi aliyejitambulisha kama Msemakweli.Naiwasilisha kama ilivyo:
 Uvamizi wa wanajeshi dhidi ya wanakijiji Kimbiji ! Polisi kigamboni wamekua BUBU!hawajakubali kupokea malalamiko ya wanakijiji ! nani ? wa  kumfunga simba kengele? 
MALI NA MAKAZI YA WANAKIJIJI WAPATAO 200 Kimbiji zimeharibiwa.
 Uvamizi uliofanyika 16.08.2011 jumatano saa 4.00 hasubui wakazi kijiji cha Kimbiji,nje kidogo ya jiji la Dar,wamekuwa na mashaka ya maisha baada ya makazi na mazao yao kuharibiwavibaya na wanajeshi (JWTZ) ambao walivamia kijiji hiko na kuvunja vunja makazi ya raia..kinyume cha sheria. 
Hata hivyo baadhi ya wanakijiji walipereka taarifa katika vya  vituo vya polisi vya Kigamboni na mji mwema,havijakubali kupokea malalamiko ya wanachi walioharibiwa mali zao na kutishiwa usalama wao,hadi sasa inaonekana kuwa wanachi wa Kimbiji hawana wa kuwalinda wao na mali zao,kama inavyoeleza katiba ya nchi kuwa kila raia ana haki ya kupewa ulinzi wa maisha yake na mali zake! 
Katika Sakata hili la wanajeshi (JWTZ) kuvamia makazi ya raia na kuharibu mali za raiabado lina utata  wa nani ? kumfunga kengengele simba?

Sunday, 21 August 2011





AFISA UBALOZI "USTAADH" IDRISA ZAHARANI AKIKARIBISHA WAGENI





Add caption






Salam,

Ubalozi wa Tanzania Hapa London Leo uliwaalika watanzania wote kutoka madhehebu na dini mbalimbali kuja kupata futari ya pamoja walioandaa ikiwa ni ishara njema ya kuonyesha amani,upendo, ukarimu kwa watanzania wote. Vyakula vya aina mbalimbali viliandaliwa  na vilipikwa katika hadhi ya kitanzania. Naibu Balozi Mh Chabaka aliwashuru wadau wote ambao waliweza kuja na kujumuika na kufuturu kwa pamoja. Aidha Mh Balozi aliahidi kushirikiana na watanzania kwa ukaribu zaidi katika hali na mali pia kuwaomba kutoa ushirikiano wao na ubalozi katika kuboresha mawasiliano na utendaji wa kazi ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo. Aliendelea kwa kusema Ubalozi upo kwa ajili yetu hivyo tuutumie ipasavyo.

Kwa niaba ya URBAN PULSE CREATIVE Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ubalozi wetu kwa namna walivyojitolea kutengeneza futari na kuwakaribisha wadau kuja kufuturu.

Asanteni Sana,

MUNGU IBARIKI AFRICA, MUNGU IBARIKI TANZANIA

URBAN PULSE CREATIVE



BENDI ya mziki ya msondo ngoma imepata TUZO ya the Best Rhumba Group katika East Africa Music Awards mashindano yariyofanyika Nairobi Kenya na kukusanyika kwa bendi za Afrika Mashariki na bendi ya msondo kuibuka Kidedea katika mashindano hayo akisibitisha ushindi uho meneja wa bendi Saidi KIbiriti alipokuwa akiongea na Msemaji wa Bendi hiyo, Rajabu Mhamila , Super D (pichani)

Alisema wameshinda tuzo hiyo na watahakikisha wanaionesha kwa mashabiki wa bendi hiyo ili kudhirisha kuwa bendi ipo ng'ang'ari popote duniani mana bendi imekamilika kila idara alisema Super D
(pichani)

Bendi hiyo itanza mazoezi siku ya jumatatu kwa ajili ya kujiandaa na sikukuu ya Iddi inayotarajia kufanyika wiki ijayo ambapo wanaingia kambini kusuka vibao vipya ikiwemo na kuvifanyia kazi vile vya Zamani

Super D alisema bendi hiyo siku ya Iddi Mosi itapiga katika viwanja vya TTC Chang'ombe ambapo mashabiki watapata kuona tuzo hiyo ya Afrika Mashariki walioitwaa hivi karibuni na kupata fursa ya kupiga nayo picha katika viwanja hivyo

Bendi hiyo inayotamba na vibao vyake vipya vya Suluu uliotungwa na Shabani Dede na Nadhili ya Mapenzi uliotungwa na Juma Katundu

Rajabu Mhamila 'Super D'
Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com www.burudan.blogspot.com
 Mob;+255787 406930
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania




Bondia YOhana Robart wa kambi ya Ilala akioneshana ufundi wa kutupa masumbwi na mtoto, Zainabu MHamila 'IKOTA' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi hiyo juzi.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com )

kondo

Kocha wa mchezo wa ngumi kondo Nassoro (kulia) akimwelekeza mtoto Zainabu Mhamila 'IKOTA' jinsi ya kutupa masumbwi wakati wa mazoezi ya kambi ya Ilala yanayoendelea katika ukumbi wa Amana CCM Dar es salaam.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com )
--
Super D Boxing Coach
Photojournalist at Majira, Business Times Email.superdboxingcoach@gmail.com www.burudan.blogspot.com
 Mob;+255787 406930
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

Saturday, 20 August 2011







Thank you so much from the bottom of my heart to all my fans.

LAST NIGHT THE SPORAH SHOW WON AN AWARDS FOR THE FACE OF 2012  SPECIAL RECOGNITION AWARDS ON WORLD HUMANITARIAN DAY 19TH AUGUST 2011 AT  THE ROYAL BOROUGH OF KENSINGTON & CHELSEA.




Sporah Sporah in the building.


The World Humanitarian Day is a celebration of people helping people. Every day humanitarian aid workers help millions of people around the world no matter who they are or where they are. The day recognizes the sacrifices and contributions of those who risk their lives to give others help and hope.


 WALKING THE ROOM..!





YES! WE WON IT..!




Sporah Accepting The Award from Dorothy.!




 All thanks goes to our adoring fans who watch The Sporah Show on TV, follow us on Twitter, Facebook, Blog etc day in and day out.




Special thanks goes to all my entire team who work tirelessly on this production.


RECOGNITION IS GREAT WHEN IT COMES FROM ANYONE.!



 SPORAH ON INTERVIEW WITH OTHER PRESS AFTER RECEIVING THE AWARD.!

 The Sporah show would like to thank Dorothy and the Team for Organising the Awards, and of course to YOU, You Guys make The Sporah Show What It Is..! Thanks for your continuing support, we could't have done this without you..!  

I LOVE YOU, I LOVE YOU, I LOVE YOU ALL XOXO



Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget