Nadhani suaskia stori kadhaa kuhusu mama wakwe.Wajuzi wa ndoa wanadaia ukitaka ndoa ivunjike basi mruhusu mkeo amlete mama yake muishi pamoja.Sijui kwanini,lakini mama wakwe ni watu wanaotazamwa kama vyanzo vya matatizo kwenye ndoa.
Sasa leo katika pita pita zangu mtandaoni nimekutana na tangazo huko Gumtree ambapo kuna jamaa ameweka tangazo kuwa "anamtoa mama mkwe wake bure." Kwa Kiingereza chenye lahaja ya Kiskotishi tangazo husika linasomeka hivi:
Free Mother In Law
Glasgow
MOANY, GREETIN' FACED!!!!!! USES YOUR WASHING MACHINE ALL THE TIME FOR NOTHING....... DESPERATE TAE GET RID OF HER!!!!! APPLY A.S.A.P.
Sasa,kama yeye mwenye mkwe yamemshinda,anatarajia nani atakayekubali kupokea mtambo huo wa kuzalisha gubu?
0 comments:
Post a Comment