Saturday, 6 August 2011
Kwanza nitoe ufafanuzi wa neno "Dola ya Kiusalama", ambalo ni tafsiri yangu isiyo rasmi ya security state.Kwa kifupi,dola ya kiusalama inaruhusu bughudha na unyanyasaji kwa wananchi wasio na hatia kwa kisingizio cha maslahi ya usalama wa taifa.
Kwa makusudi,Tanzania yetu inaelekea kurejeshwa kwenye zama hizo za wanausalama kupewa ruhusa ya kumbughudhi mwananchi yoyote yule kwa kisingizio cha "kusaka taarifa za kiusalama." Of course,sheria za nchi zinavipatia mamlaka vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wao katika namna inavyoweza kutafsiriwa kama unyanyasaji wa wananchi,lakini hilo si tatizo kubwa iwapo uchunguzi huo unafanyika kwa maslahi ya umma.
Taarifa nilizonazo ni kwamba wanausalama wetu wameanza kuwasumbua baadhi ya wananchi wasio na hatia wakishinikiza kufahamu "chanzo cha tetesi za ufisadi mkubwa huko JWTZ".Usidhani kuwa wanasaka chanzo hicho kwa minajili ya kusaidiana nacho katika uchunguzi wa suala hilo (kama upo).Wanataka kumfunga mdogo.
Huu ni uhuni wa kitaaluma.Kama huyo anayetuhumiwa kukibwa fedha za umma anaona amekashifiwa,kwanini asiende mahakamani?Nini kinafichwa katika suala hili?Natambua kuna wanaodai kuwa suala hili ni nyeti sana na linaweza kupelekea uasi huko jeshini (ambapo asilimia kubwa ya askari wanaishi maisha magumu kulinganisha na makamanda wao).Lakini hoja hiyo haina uzito kushinda ukweli kwamba fisadi ni fisadi,awe raia au kamanda wa jeshi,na hatua za kisheria lazima zichukuliwe dhidi yake.
Watawala wanataka kulificha suala hili chini ya zulia.Lakini itambulikwe kuwa tunaishi zama tofauti na huko nyuma.Iwapo suala hili halitashughulikiwa kikamilifu na kiuadilifu,basi wahusika wakae wakijua kuwa kuna siku litalipuka upya.
Na nyie mnaojaribu kunyanyasa wananchi kuwashinikiza wawaambie vyanzo vya tetesi za ufisadi jeshini ACHENI MARA MOJA.Hatupendi kuharibu hadhi ya nchi yetu kwa nchi na taasisi wafadhili lakini mkiendeleza uhuni huu tutashawishika kuweka hadharani jinsi mnavyojaribu kufunika ufisadi kwa kuwanyanyasa wanaoibua taarifa hizo.
Nimechukua hatua zaidi kwa kum-tweet Rais Jakaya Kikwete (@jmkikwete) kama invyoonekana mwanzoni mwa makala hii.
Related Posts:
TAARIFA YA SIRI: Nimetumiwa Nami Naiwasilisha Kama IlivyoAwali nilitundika taarifa ifuatayo baada ya kuiona huko Jamii Forums kabla ya post husika kufutwa.Mzembe mmoja akanitumia email akidai mie ndio mtunzi wa taarifa hiyo.Mchumia tumbo huyo alikuwa na kila sababu ya kukasirika ju… Read More
Mashushushu Wanajiandaa Kuchakachua Matokeo ya Uchaguzi?Nimekumbana na post ifuatayo hapo Jamii Forums.Naiwasilisha kama ilivyo kisha tujiulize kwa pamoja (kama tuhuma hizo ni za kweli) wanafanya hivyo kwa faida ya nani?Taarifa ya Siri - Mikakati ya Kuiba Kura Inavyoendelea USALAM… Read More
Dkt Slaa: Serikali Imetuma Maofisa Usalama wa Taifa Mikoani Kuhakikisha Ushindi kwa KikweteCHADEMA: Synovate wahini mahakamani*Slaa asema wanazo nyaraka za utafiti wao.*Adai kuna mbinu za 'kuchakachua' matokeo.Na Tumaini Makene CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeivaa kampuni utafiti ya Synovate kikisis… Read More
Makala yangu ktk Raia Mwema Toleo la Mei 4: "Ya Obama,Kikwete na Usalama wa Taifa"Makala yangu katika toleo la wiki hii la jarida maridhawa la Raia Mwema inafanya uchambuzi linganifu kuhusu,kwa upande mmoja,tuhuma zilizomwandama Rais Obama kuwa sio raia wa Marekani,na hatimaye uamuzi wake kutoa cheti chake… Read More
Msikie Huyu NaeMakala yangu katika jarida la Raia Mwema toleo la wiki iliyopita ililenga kuchokoza mjadala kuhusu "mashushushu".Nilijaribu kutengeneza mazingira ya kumwezesha msomaji kuhitimisha iwapo madai ya mgombea urais kwa tiketi ya Ch… Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment