Thursday, 22 April 2010

Majuzi Rais Jakaya Kikwete alimteua Doug Pitt,mdogo wa staa wa filamu Brad Pitt,kuwa balozi wa heshima (goodwill ambassador) kusaidia kuitangaza Tanzania hususan kwenye sekta ya utalii.Kwa kuzingatia wasifu wa Doug,na umuhimu wa kuitangaza nchi yetu,uteuzi huo unastahili pongezi za kutosha.Hat hivyo,ili Doug awe na umuhimu kwa Tanzania,au uteuzi wake uzae matunda yanayotarajiwa,kuna mambo kadhaa tunayopaswa kuyaangalia kwa makini 
Kwa hakika hatuna kisingizio cha kwanini nchi yetu inahitaji nguvu za ziada (kama akina Doug) katika kujitangaza.Tuna kila aina ya utajiri na vivutio ambavyo laiti tungejibidiisha kuvitangaza kwa bidii basi huenda tungekuwa mbali sana kimaendeleo.Kwa mtizamo wangu,kikwazo kikubwa ni uhaba wa uzalendo.Baadhi ya wateule wanaopaswa kuwajibika ipasavyo kulitangaza taifa letu na raslimali zake wako bize zaidi kuangalia maslahi yao binafsi badala ya kufanya kile wanacholipwa mshahara kukifanya.

Lakini kama unadhani hilo ni tatizo dogo basi kuna suala la mazingira yanayopaswa kuboreshwa ili jitihada za Doug ziweze kuwa na maana au zilete ufanisi unaotarajiwa.Kwa mfano,Doug anaweza kuhamasisha watalii waje kwa wingi Tanzania,lakini kwa ufisadi unaoendelea kila kukicha katika sekta ya umeme,ni dhahiri kuwa watalii watakaoitikia wito wa Doug wanaweza kuhisi 'wameingizwa mkenge' baada ya kukutana na adha za mgao wa umeme ambao unazidi kuzoeleka kwa Watanzania wengi.Danadana zinaendelea kuhusu kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo sugu la umeme.Na kikwazo kikubwa katika kupatikana ufumbuzi huo ni wahusika kutanguliza maslahi yao binafsi badala ya yale ya taifa.Ni katika mazingira hayo ndipo matapeli wa Richmond na Dowans walifanikiwa kutufisadi.

Kwa Watanzania walio nje watakubaliana nami kwamba kwa hawa wenzetu,'holidays' ni suala lenye umuhimu wa kipekee katika kalenda na ratiba zao.Ni matarajio ya wengi kwamba holidays walizozihangaikia kwa muda mrefu zitaacha kumbukumbu nzuri maishani mwao,na sio kugeuka 'holidays from hell'.

Kuna tatizo jingine katika suala la udokozi.Pale Mwalimu Nyerere International Airport panahitaji tahadhari kubwa ili mizigo ya msafiri itoke eneo hilo salama.Sasa kama kweli tunataka jitihada za akina Doug ziwe na maana ni vema tukafahamu kuwa pasipo kudhibiti wahuni hawa wa airport ambao inaonekana dhamira yao kuu ni kutoa 'karibu Tanzania ya majonzi' tutaishia kukimbiza watalii badala ya kuwafanya wawashiwishi ndugu na jamaa zao nao waende Tanzania kutalii.Wadokozi wengine mahiri wako Posta.Kwa vile mawasiliano yetu bado si ya kisasa sana,umuhimu wa Posta unabaki kuwa mkubwa,na si ajabu kwa baadhi ya potential watalii kutumia huduma hiyo kabla ya kwenda Tanzania,au wakati wakiwa hapo.Sasa it seems as if baadhi (au pengine most) ya watumishi wa Posta wana 'allergy' na kitu chochote chenye address ya ng'ambo.Ni lazima wafungue na wakikuta chochote 'wanakitaifisha'.

Tuna matatizo ya miundombinu.Tumeruhusu wahuni wa TRL wafanye usanii wao pasipo kuleta mabadiliko yoyote ya muhimu zaidi ya kuandika historia ya kuwa wawekezaji wa kwanza kusaidiwa na serikali kulipa mishahara ya wafanyakazi wao.Ni dhahiri kuwa laiti waliosaini mkataba wa wababaishaji hao angekuwa mzalendo wa dhati angetambua kuwa wangekuja kuikongoroa zaidi Reli ya Kati kuliko walikvyoikuta.Je watalii wakitaka kutumia usafiri wa treni kutalii inakuwaje?Huko TAZARA nako hadithi ni ileile.Na hii ni njia muhimu kwa mtalii anayetaka 'kuifaidi' hifadhi ya Selous.

Kuna tatizo la barabara zetu.Na hapa kuna suala la barabara za msimu ambazo kupitika kwake kunatarajia msimu wa mwaka.Nyingi ya barabara hizi hufanyiwa ukarabari pale tu panapokuwa na ujio wa kiongozi.Uelekeo wa kule kwetu Ifakara tuna hifadhi ya msitu asilia,lakini kufikika kwake ni mbinde msimu wa masika.

Kwa kifupi,nachojaribu kupigia mstari hapa ni umuhimu wa kuboresha mazingira yatakayopelekea watalii kuhitimisha kuwa hawakufanya makosa kukubali ushauri wa Doug kuitembelea Tanzania.Pasipo mazingira bora basi tunaweza kuteua mabalozi Hollywood nzima lakini itakuwa kazi bure.

Na jingine la muhimu zaidi ni manufaa ya ujio wa watalii kwa Watanzania.Sote tunashuhudia jitihada za kuvutia wawekezaji na mwitikio wao lakini pia sote twafahamu namna uwekezaji ulivyoshindwa kuwa na manufaa kwa Watanzania walio wengi.Makampuni ya madini yanazidi kumaliza raslimali zetu huku sie wenye utajiri huo tukibaki na mashimo matupu.Sasa Doug anaweza kulivalia njuga suala la kuhamasisha watalii,nao wakaitikia wito lakini kitakachopatikana kikaishia kwenye ununuzi wa ma-vogue,ujenzi wa mahekalu au kuongeza idadi ya nyumba ndogo za mafisadi.

Ndio maana basi,pamoja na kupongeza uteuzi wa Doug Pitt kuwa balozi wa hisani wa Tanzania huko Marekani,ni muhimu kuwekeza zaidi katika uzalendo utakaopelekea kuzalisha akina Doug wa ndani (na hakutokuwa na gharama ya kuwafuata ng'ambo) na, cha muhimu zaidi,kuchangia maendeleo ya taifa letu 'changa'.

1 comment:

  1. Tanzania ina wawakilishi wa hadi ngazi ya kibalozi kamili tena ni wawili huko Marekani mmoja akiwakilisha serikali na ofisi yake hipo Washington DC na mwingine anawakilisha umoja wa mataifa kama balozi wa kudumu zaidi ya hiyo kuna wizara ya mambo ya nje na pia ya utalii. Sasa kumwomba bwana Doug ni kuthibitisha timu yake ya Uongozi Bwana Kikwete siyo kamilifu. Au ndiyo amekubali sasa kuwa Shirika la reli arudishiwe Mjerumani na serikali yake pia yote(kurudi kwa mkoloni). Maana sisi wenyewe tumeshindwa kuwa wabunifu na kujitawala

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget