Sunday, 4 April 2010

Ukifuatilia kwa karibu namna nchi yetu ilivyogeuzwa 'shamba la bibi' unaweza kupata shinikizo la damu siku si zako.However,shinikizo la damu or not,tutaendelea kufahamishana namna ufisadi unavyoiteketeza nchi kwa kasi,ari na nguvu kubwa.Na haya yanatokea wakati kuna watu wanalipwa mishahara kuhakikisha hayatokei. Nimekutana na habari moja kwenye gazeti la Mwananchi ikieleza kwamba Jeshi la Magereza limekumbwa na kashfa ya ufisadi wa shilingi milioni 300.Ufisadi huo umewekwa hadharani na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa Kamati Ya Bunge ya Hesabu za Serikali.Yaani taasisi iliyopewa jukumu la kuwahifadhi na kuwarekebisha tabia wafungwa nayo inafanya yaleyale yaliyopelekea wengi wa wafungwa kuwa jela in the first place.Well,namaanisha wale waliofanya uhalifu lakini hawakuwa na majina ya kuwalinda au hawakuwa na uwezo wa kuhonga ili kesi zao zife kienyeji.

Kichekesho ni kwamba wezi wa mamilioni hayo walifikishwa mahakamani (pengine katika kutuzuga kuwa sheria inachukua mkondo wake) lakini wakaachiwa huru katika kile kinachofahamika kisheria kama want of prosecution.Kichekesho kingine ni kwamba licha ufisadi huo,Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi imelipa jeshi la magareza 'hati safi'.Yani ni kama wanapongwezwa kwa kuiba mamilioni badala ya mabilioni kaka wenzao huko Benki Kuu,TRA,nk.Na kikubwa zaidi ya kichekesho ni kauli ya Mbunge Mudhihir Mudhihir,ambaye ni mjumbe wa Kamati hiyo ya Bunge,kwamba "Pamoja na kwamba mna hati safi, lakini upotevu huu wa fedha unasikitisha sana..."Hivi kusikitika sana kunasaidia nini?Kwanini badala ya kupoteza muda kusikitika,Mbunge huyo na Kamati yake wakaagiza hatua zaidi za kisheria?Rais anasikitika,mawaziri wanasikitika,wabunge wanasikitika!Yani utadhani kwa kusikitika kwao mafisadi watapatwa na huruma na kusitisha ujambazi wao.

Well,makala hii inauliza Mdhibiti na Mkaguzi wa nini nikimaanisha ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali inavyofanya kazi ya kujaza maji kwenye gunia.Ikumbukwe kuwa uandaaji wa ripoti za ofisi hiyo unahisisha matumizi ya fedha za walipakodi.Kinachokasirisha ni ukweli kwamba taarifa za ofisi hiyo zimeendelea kuwa kama utaratibu tu wa kusukuma siku kwani wenye mamlaka ya kuzifanyia kazi hawaonekani kuguswa kwa namna yoyote na wingi wa tarakimu katika fedha zilizofisadiwa.

Picha hapo juu inamwonyesha Rais Kikwete akipokea ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu,Ludovic Utouh.Unaweza kupata matumaini kuwa labda ripoti hiyoi inaweza kufanyiwa kazi mwaka huu kwa vile kuna uchaguzi,au kwa vile CCJ imezaliwa...kalagabaho,huo ni utaratibu tu.Utouh katimiza wajibu wake,na JK nae katimiza wajibu wake wa kupokea taarifa,na kupigwa picha inayoashiria kuwa tuna Tanzania ina uongozi unaoguswa sana na matumizi ya fedha za umma!

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget