Thursday, 5 August 2010

Natoa wito kwa wanachama walioomba nafasi lakini wakakosa, jamani msiwe chanzo cha mifarakano ndani ya chama, KAZI ZIPO NYINGI,TUNAWEZA KUTEUANA, fanyeni kazi ya ushindi kwa chama chetu,” .Hayo si maneno yangu bali ya Rais Jakaya Kikwete aliyoyatoa siku alipochukua fomu za kuogombea tena urais kwa tiketi ya CCM.Ni kweli kazi zipo nyingi ikiwa ni pamoja na kilimo au biashara lakini haiingii akilini kwa watu waliokataliwa na wananchi kupewa nafasi kwa mlango wa "kuteuana".

Hili ni tatizo sugu katika siasa za Tanzania.Utakuta mtu ameboronga sehemu moja kisha anahamishiwa sehemu nyingine.Yayumkinika kusema kuwa kuteua "rejects" hao sio tu matumizi mabaya ya ruhusu inayotolewa na katika kufanya teuzi mbalimbali bali pia ni dharau ya moja kwa moja kwa wananchi.

Haiwezekani kwamba nchi yenye watu zaidi ya milioni 40 iwe na kikundi kidogo tu cha watu wenye uwezo wa kuwa viongozi.Na kibaya zaidi kikundi hicho kikijumuisha watu waliokataliwa na wananchi katika chaguzi au maombi yao ya kutaka wachaguliwe kuongoza.

Na ukiingia kiundani zaidi kuangalia tabia hii isiyopendeza,unaweza kuyumkinisha kuwa hata uteuzi wa Dkt Gharib Bilal unaangukia kwenye eneo hilohilo.Bilal alitaka ridhaa ya vikao vya CCM kuwa mgombea wa Zanzibar lakini "kura hazikutosha".Hata hivyo,katika kile kinachoelezwa kama kujenga mshikamano miongoni mwa wana-CCM,Bilal aliteuliwa na JK kuwa mgombea mwenza wake.Kwa maana nyingine,mtu aliyekataliwa na kikundi kidogo (kikao cha CCM kilichpiga kura kumpata mgombea urais wa Zanzibar) anaweza kuwa Makamu wa Rais wa Watanzania milioni 40 na ushee pindi JK akishinda katika uchaguzi ujao.

Tumekuwa tukishuhudia teuzi za mabalozi wetu nje ya nchi,wenyeviti wa bodi za wakurugenzi wa taasisi mbalimbali,wakuu wa mikoa na wilaya na nafasi mbalimbali zinazojazwa kwa teuzi zinazofanywa na rais zikijazwa na "rejects"-watu walionyimwa ridhaa ya kuongoza na wananchi lakini wanaishia kuwa viongozi kwa mlango wa nyuma.Yaleyale ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa UWT,Hasna Mwilima.Kikundi kidogo katika jumuiya hiyo ya akinamama wa CCM kilimkataa,huku sababu kuu ikitajwa kuwa ni uongozi mbovu.Lakini siku chache baadaye,Rais akamteua mwanamama huyo kuwa Mkuu wa Wilaya.Busara kidogo tu zinaweza kubainisha kuwa kuwa mtu alokataliwa kuongoza UWT hawezi kuwa "rais wa wilaya" (DC) lakini kwa vile Katiba inamruhusu Rais kuteua yeyote amtakaye,analotaka liwe litakuwa.

Ni katika mazingira haya ndio maana tetesi kuwa Lowassa,Waziri Mkuu aliyelazimishwa kujiuzulu kutokana na ufisadi wa Richmond,atarejea madarakani pindi JK akishinda hapo Oktoba zinazidi kupata nguvu kwa vile Rais akiamua iwe na itakuwa.Na kwa vile Watanzania wanasifika kwa upole wao,hakutokuwa na "kelele" za kupinga uteuzi huo.

Nguvu anazopewa Rais kwenye Katiba hazimaanishi ajifanyie mambo anavyotaka bali ni kwa minajili ya kuwatumikia Watanzania kwa ufanisi.Lakini kwa upande mwingine,lawama zinaweza kuelekezwa kwa taasisi zinazomshauri Rais kuhusu teuzi mbalimbali (ikiwa ni pamoja na kuchunguza 'usafi' na uwezo wa wateuliwa watarajiwa) kwa sababu inaelekea kwa wao,kila jina linaloletwa na Rais ni 'safi'.Professionalism na ethics zinawekwa kando kwa minajili ya kumfurahisha mkuu wa nchi.

Related Posts:

  • Kama Hii Ni Kweli Basi TUMEKWISHAHapa chini kuna habari ambayo kama ni ya kweli basi hatma ya nchi yetu iko mashakani.Lakini kabla hujaisoma,angalia picha ifuatayo na inaweza kukusaidia kukupa uelewa wa namna tulivyofika tulipo.KUMBE Rais Jakaya Kikwete haku… Read More
  • JK NA MIPASHO KATI YA MWILIMA NA SOPHIA SIMBAKama Mtanzania mzalendo na mwenye kupenda nchi yangu nawajibika kuwa na heshima kubwa kwa Rais wangu Jakaya Kikwete.Hata hivyo,heshima inapaswa kuendana na matendo ya mheshimiwa.Kwa maana hiyo,naamini simkosei heshima Rais wa… Read More
  • REDET: Pinda Mchapakazi Zaidi Ya Kikwete na SheinMatokeo ya utafiti uliofanywa na Mradi wa Utafiti na Elimu na Demokrasia Tanzania (REDET) yanaonyesha kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ni mchapakazi zaidi ya 'bosi' zake,Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Ali Mohammed Sh… Read More
  • Ah,JK Vipi Mbona Haeleweki?Kwa hakika baadhi ya kauli za Rais wetu Jakaya Kikwete zinachanganya kupita kiasi.Juzijuzi tu alisaini kwa mbwembwe sheria tuliyoambiwa imelenga kudhibiti rushwa katika chaguzi.Tukiweka kando suala la wasaidizi wake kumwingiz… Read More
  • 'Ushindi' wa Obama na fundisho kwa JKKiongozi shurti awe na msimamo na kisha asimamie kile anachoamini.Kwa mara nyingine,Rais Barak Obama ameithibitishia dunia kuwa ni 'mwanaume wa shoka' linapokuja sula la kuamini anachosimamia.Hatimaye jana Obama alifanikiwa k… Read More

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget