Sijui ndio dalili kuwa mwenendo wa kampeni unakwenda ovyo au ni ubabaishaji tu,lakini "mkwara" uliochimbwa na mnajimu mahiri,Sheikh Yahya Hussein,kwamba anampatia Rais Jakaya Kikwete ulinzi wa majini ni suala linalopaswa kukemewa kwa nguvu zote.Na ukweli kwamba mtajwa-i.e. Kikwete- amekaa kimya ni ushahidi tosha kuwa ananufaishwa na majini hayo.
Kwa baadhi yetu tunaofahamu yanayofanyika "nyuma ya pazia" (behind the scene) hatushtushwi kihivyo na habari hizo kwa vile siasa za Tanzania na ushirikina ni kama samaki na maji.Hakuna msimu mzuri kwa waganga wa kienyeji kama huu wa uchaguzi ambapo wanasiasa wababaishaji wanajaribu kupata msaada wa nguvu za giza ili wapate ushindi.
Awali,Sheikh Yahya alitoa tishio kuwa atakayejitokeza kuwania nafasi ya urais na Kikwete atakutwa na mauti.Well,so far tukio pekee la kutishia uhai wa mwanasiasa katika harakati za uchaguzi wa mwaka huu ni kudondoka jukwaani kwa Kikwete wakati anazindua kampeni zake kwenye viwanja vya Jangwani.Whether majini yaligoma kutumikishwa au Kikwete alikiuka masharti ya mganga wake Sheikh Yahya leaves a lot to be desired.
Binafsi natafsiri tishio hili jipya la Sheikh Yahya kama mkakati mufilisi wa Kikwete na CCM yake kuwatisha wapiga kura.Yea,kwani kama si hivyo kwanini basi mhusika asikanushe hadharani na kusema "ulinzi pekee nilionao ni huu unaotolewa na Idara ya Usalama wa Taifa".Hawa ni wataalam wa ulinzi wa viongozi na wanalipwa kwa ajili ya kazi hiyo.Sasa kama kuna ulinzi mwingine wa nguvu za giza,na ambao Kikwete anauamini,basi pengine ni muhimu kuokoa fedha za walipa kodi kwa kusitisha ulinzi anapotatiwa na "walinzi binadamu" na abaki na hayo majini ya Sheikh Yahya.
Samahani kama nitakuudhi lakini nashawishika kueleza kuwa napatab tabu sana kuelewa kwani pamoja na madudu yote haya-from sera to ushirikina,from afya mgogoro to kurudia ahadi za 2005 as if hii ndio mara ya kwanza kwa JK kuwania urais-bado kuna Watanzania wenzetu wanatamani mwanasiasa huyu na chama chake warejee madarakani.Jamani,hivi Kikwete na CCM wafanye nini zaidi ili mfikie hatua ya kusema "aah sasa basi,just go away!"?
Hivi mkiweka kando ushabiki,hizi "ahadi za fotokopi" anazotoa Kikwete zilishindikana vipi kutekelezwa katika miaka yake mitano aliyokuwa madarakani?Hata kama angejitetea kuwa muda mwingi alikuwa nje ya nchi kutalii bado alikuwa na baraza kubwa la mawaziri ambalo lingeweza kabisa kutekeleza maagizo yake.
Kama mnampenda kwa dhati basi bora msimpe kura ili aweze kupumzika kwa amani kwani kumrejesha tena Ikulu hapo Oktoba ni kumbebesha mzigo ule ule uliomshinda katika miaka mitano tunayomaliza.Hii ni kwa faida yake na yenu.Na anazidi kuwaonyesha kuwa badala ya kutegemea mambo halisi kufikia malengo yaliyokusudiwa,sasa kageukia majini.Nchi haiwezi kuongozwa kwa msaada wa majini.Na kamwe Tanzania haiwezi kupiga hatua kama miongoni mwa wasaidizi wa Rais ni majini.
MPIGA KURA,SHEIKH YAHYA AMEKUPA SABABU NYINGINE KATI YA NYINGI ZILIZOPO ZA KUMNYIMA KURA YAKO KIKWETE.KURA KWA KIKWETE ITAKUGHARIMU MIAKA MITANO IJAYO AMBAPO LICHA YA UFISADI,FEDHA ZA WALIPAKODI ZITATUMIKA KULIPA FADHILA KWA MAJINI WANAOMPATIA ULINZI WAKATI HUU WA KAMPENI.
KUMBUKA JINI LIKITOKA KWENYE CHUPA HALIRUDI.IN CASE YOU FORGET,VIDEO IFUATAYO ITAKUKUMBUSHA(GENIE IN A BOTTLE)
Hapo umenena kweli tupu Kaka....
ReplyDeleteUislamu unakataza mambo hayo. Sasa hapo tueleweje?
ReplyDeleteHuu ni uthibitisho Dini zemehindwa kuibadili tabia na bila za kiafrika...Kimsingi ni karne kadhaa zimekwishapita tangu dini kutufikia wa Waafrika. Na ushahidi wake ndiyo huo kuendeleza nguvu za kishirikina katika maisha yetu kila siku na hata Sheikh Yahya ndiyo chanzo kipato chake kila siku kuendesha maisha
ReplyDelete