Sunday, 26 September 2010




Video zote kwa hisani ya Coby

NAOMBA MSAMAHA KWENU WAFANYAKAZI WAPENDWA KWA KUWATOA MACHOZI YA UCHUNGU BAADA YA KUANGALIA VIDEO HIZO.LENGO LANGU SIO KUWATIA UCHUNGU BALI KUWAKUMBUSHA JEURI YA JAKAYA KIKWETE KWENU.VILEVILE VIDEO HIZI ZINAWEZA KUSAIDIA KUMPA KIKWETE AIBU YA KUUDANGANYA UMMA KUWA HAJAWAHI KUKATAA KURA ZENU WAFANYAKAZI WAPENDWA.

NAWASIHI MACHOZI YENU YASIMWAGIKE BURE BALI MTAFSIRI UCHUNGU WENU KWA KUMPATIA MGOMBEA ALIYETANGAZA HADHARANI KUWA ANAZIHITAJI SANA KURA ZENU.MGOMBEA HUYO NI DOKTA WILLBROAD SLAA WA CHADEMA.KIKWETE ALIWAADHIRI HADHARANI KUPITIA KWENYE RUNINGA,NINYI MUMSHIKISHE ADABU FARAGHANI KWENYE KISANDUKU CHA KURA HAPO TAREHE 31/10/2010.

OMBI LA BLOGU HII NI KWA KILA MFANYAKAZI ALIYEUMIZWA NA JEURI HIZO ZA KIKWETE KUHAMASISHA MKE,MUME,DADA,KAKA,MWANA,SHANGAZI,BINAMU,MJOMBA,JIRANI,MPANGAJI,SHOSTI,MSHKAJI,MWENYE NYUMBA NA YEYOTE YULE UNAYEFAHAMIANA NAE,KISHA UWAHAMASISHE WAMNYIME KURA KIKWETE NA CCM YAKE NA BADALA YAKE KUMPIGIA KURA DOKTA SLAA NA CHADEMA.CHONDE CHONDE WAFANYAKAZI,MSIACHIE NAFASI HII ADIMU.
Video zote kwa hisani ya Coby

3 comments:

  1. Huu ni udikta! sioni lojiki ya kwenda kukimbilia kwa wazee,raisi angetoa hii hotuba pale Nkurumah hall,hapo tungemwona rais wa maana.

    ReplyDelete
  2. Chahali kampeni zako babu kubwa. yaani unataka kutudanganya tukuamini kabisa ati ulimwaga chozi kwa kuangalia video ya jeuri ya JK kwa wafanyakazi..wachekesha kweli...wafanyakazi walitafakari baina ya akili ya kuambiwa na akili yao wakaona ni upuuzi kumuendekeza Mgaya na kundi lake.
    Tupo Gado tunachapa kazi na labda nikupe habari za kuvunja habari (Breaking News) mwezi oktoba haumaliziki, tunalipwa malimbikizo ya nyongeza na mwisho wa mwezi tunalipwa mishahara mipya...hapo tunaongeza uwezo wa kukopesheka na kuwekeza katika vitega uchumi vidogo vidogo, wewe utabaki na SLAA wako tu....labda mwaka 1995 ulikuwa bado u mtoto hukuona yaliyojiri...Wafanyakazi TUNASEMAA HATUDANGANYIKIIIIIIIIII.......kura YANGU NA za Wafanyakazi wengi tu zinaenda CCM hususan kwa JK.....pole kwa kuoata mchana

    ReplyDelete
  3. RAIZER WEWE SIO MZALENDO HATA KIDOGO . KWANZA NAFIKIRI WEWE NI MAMRUKI NDANI YA CCM YAKO , UNAOFIKIRI NI WENGI SIO KWELI WAFANYAKAZI WENGI HATUKO HUKO ULIKO WEWE . KWANI CHA MLEVI HULIWA TU , NA FADHILA ISIWEPO . KUONGEZA MISHAHARA KWA WAFANYAKAZI NI RUSHWA AMBAYO TUMEIBAINI WENYE AKILI TIMAMU . ENDELEA KUDANGANYIKA , WENZIO MPAKA KIELEWEKE .

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget