Sijaitunga mimi,nimeipokea tu,nikasioma na kuisambaza
Ee KIKWETE Uliye tufilisi,
Jina lako USANII MTUPU,
utakalo lifanyike BAGAMOYO TU,
utupe leo mabilioni yetu ya EPA, uwapeleke MAFISADI wote Mahakamani,
uwape WASTAAFU pesa zao,
uwasamehe wafungwa hasa BABU SEYA kama ulivyomsamehe LOWASA,
Usitutie katika mikataba FEKI,
kwa kuwa UFISADI ni fani yako na uwongo hata milele,
na Uanguke kwenye uchaguzi ujao kama unavyoanguka hovyo jukwaani, AMINA
UPDATE: Nimetumiwa Sala nyingine,hii inamhusu Dokta Slaa,nimeisoma na kuisambaza
""IMANI YA CHADEMA""
Namwamin Dk.WILBROAD, mwana wa SLAA, Ndugu Yetu, aliyepitia vikwazo vingi kwa hujuma za CCM. Akateswa kwa kashfa za Ndoa, Akadhihakiwa, Akapingwa, Akaonyesha msimamo; Siku ya siku akasimama kwa kishindo; Akapaza sauti, Ameketi mkono wa kuume kutetea haki za Watanzania; Kutoka huko atakuja kuwahukumu mafisadi.
hahhahhahah!!!!
ReplyDeletemungu ampe afya kikwete atuongoze milele
ReplyDeleteAfya yakutuongoza milele ampe mungu au walinzi wake anaopewa na Sheikh Yahya Hussein? Mbona mnachanganya mambo?? By the way kuongoza milele hawezi maana ata Mobutu Seseseko hakuweza kuongoza milele. But the prayer is interesting!
ReplyDeleteSala zote zina mantiki!
ReplyDeleteHa ha I love politics with all my soul,mind and heart.. The prayers are too funny Btw,
ReplyDeleteTHIS YEAR IS FOR DR. SLAA..GOD BLESS TZee..