NA HAPA CHINI NI PICHA YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKIPOKEA TUZO YA MILENIA KWA MAFANIKIO HAYO HAPO JUU
HAPA CHINI AKIWA NA BALOZI WETU KWENYE UMOJA WA MATAIFA OMBENI SEFUE
NA KAMA ILIVYOTARAJIWA,HAPO CHINI NI PICHA INAYOONYESHA MAJIGAMBO YA KIKWETE HUKO TWITTER (Kikwete2010)
KUNA MZEMBE MMOJA KANITUMIA COMMENT YA MATUSI AKILAUMU KUWA NAANGALIA MABAYA TU YA CHAGUO LA MUNGU KIKWETE.SIJAICHAPISHA KWA VILE ANATAFUTA UMAARUFU KWA MGONGO WA BLOGU HII.AMETISHIA KUWA ATAPOREJEA HAPA BLOGUNI NIWE NIMEBALANSI STORI.NAMSHAURI AENDE MIREMBE AKABALANSI UBONGO WAKE KWANZA.VITISHO HIVYO NI DALILI KUWA UJUMBE UNAFIKA KUNAKOHUSIKA.ANAYEKERWA NA SIFA ZA BLOGU HII KWA CHAGUO LA MUNGU APONDE CHUPA AMEZE.HAPA HAONEWI HAYA MTU.BRING IT ON!!!!
Sema Chahali sema usiogope wezi, wezi nyumba yao ni jela....unakumbuka hiyo!?
ReplyDeleteMafisadi na mashabiki wao siku zinahesabika...Sheria inalinda haki na pia haki inalindwa na sheria...Muhalifu analindwa na mafisadi, mashabiki, na serikali legelege kama hii ya CCM ikiongozwa na wababaishaji(zuga).
Hivyo wote tukiwajumuisha na hao wanaokutumia ujumbe wa kihalifu -kutukana(mafisadi) kutokana na mazoea yao ya kutenda vitendo vya kihalifu.
Big up ughaibuni blog victory for Dr Slaa 31.10.2010
God bless you kaka!!! Kama kuna mtu ughaibuni anamfagilia JK basi huyo ni kati ya wale watoto wa wale wenye pass tatu za kusafiria na wakati huo baba zao ndo wanazidi kuvoti watoto wa wabeba mabox wazidi kusota.
ReplyDeleteSisi tulosoma kwa kodi ya wananchi na misaada ya wascandnavia bado tunajua jinsi mchonga alivyojitahidi mpaka tukapata elemu na iliyo bora kupita kiasi. mama yangu alikuwa yatima lakini aliweza kusoma kisomo cha ngumbaru na sasa anaweza kuandika na kusoma barua zangu at the same time aliweza kufikia English hatua ya nne. Mama anaweza kuongea kimombo kuliko hata mtoto anayemaliza f. 4 wakati huu.
Tulisomeshwa kwa kahawa na tulilipiwa na BCU sasa iko wapi?? Watoto wa wakulima wa kahawa hawawezi hata kupata mlo mmoja wakati sisi tulilipiwa chakula na BCU. Swali ni je? Kahawa zimebadilika utamu au soko limepungua? Mbona mashangingi hayapungui.
Mimi ni mwalimu kwa ajila. Kuna mradi wa vitabu ulianzishwa na British council nchi nzima watoto wasome na kushindana. Nauliza leo uko wapi? Niliacha ualimu muda kidogo na sipo nchini ila nina uhakika hivyo vitabu vya kiada havipo tena. Ili mtoto apende kusoma ajengewe mazingira kama kujisomea vitabu kama vya Bulicheka au Alf lela ulela lakini unaleta vitabu vya sokoni katerero au sijui brown ashika tama, nani atakuwa na mvuto nani atasikiliza wakati ameshinda anachota maji ya mwalimu na hajui kama nyumbani atakuta hata chakula???
Wazazi wengi wamefariki na kuacha watoto yatima. Vigogo wametumia mwanya kujitajirisha. Mwingine alichukua watoto kabla ya uchaguzi 2005, nasikia juzi juzi kawarudisha eti pesa zimekwisha. Kumbe alitaka sifa ili ateuliwe kama mbunge wa viti maalumu at the same time anachota pesa za kichungaji nje ya nchi.
Nikiandika siwezi kuacha sababu nina uchungu ila kaka ANDIKA NA USIACHE. PIGA PICHA NA UWEKE KWENYE MABANGO YA SARENDA BRIDGE TUTAKUCHANGIA ACHANA NA HAO. HATA WENGINE WAKIONDOKA SABABU YA UMEME LAKINI WANAOBAKI NI SAWA NA HAO HAO.
KAKA MUNGU AKUTANGULIE, HALI IMEKUWA MBAYA MNO ALAFU WENGINE BADO WANAZUBAA!! NASHANGAA BLOG FLANI UNAANDIKA COMMENT ZINABANIWA!! SASA NIKAMUULIZA KAKA COMMENT HAINA KEBEHI, MATUSI,DHARAU WALA NINI, IPO PLAIN ILIYOJAA UKWELI, KWANINI UNAIBANIA? UTAJIVUNIA NINI UKISHAZEEKA KAMA MWANAHABARI WAKATI HALI NDIO IMEKUWA WORSE!! INASIKITISHA SANA, NA KINACHOSHANGAZA HAPA WATU WAMEKUWAJE! HAMUONI UCHUNGU NA HALI TUNAYOISHI WAKATI WENGINE WANAKULA HAKI YAKO KIULAINI? MBONA CHANGE NI KITU KIDOGO TU? IMESHATOKEA NCHI NYINGINE MFANO BOTWANA TU HAPO, KILA MWANANCHI ANAFAIDIKA NA MADINI YALIYOPO KWENYE NCHI YAKE, MJI MSAFI, ELIMU MURUA, YOTE HAYO MADINI, NDIO MAANA NI NGUMU SANA KUKUTANA NA WABOTSWANA POPOTE PALE, AKITOKA KATAKA MWENYEWE,KWANINI SISI TUNAKUWA MAMBUMBUMBU HIVI! MATOKEO YAKE TUMEJAA KILA KONA!! TUNATAKA KURUDI NYUMBANI, TUMECHOKA NA HALI YA SERIKALI YETU YA MAFISADI WALIOKAMUA NCHI YETU MPAKA LEO TUNASHUHUDIA WATOTO WETU WANAKALIA MATOFALI WAKATI SERIKALI INALIPA MAMILIONI KWENYE UONGO WA RICHMOND!! WALAHII THIS IS GETTING SERIOUS PEOPLE!! NA HUYU BALALI TULIYEAMBIWA ALIFIA MAREKANI NA KABURI LAKE WABONGO WAMEFWATILIA BADO HALIJAONEKANA!! NI USHAHIDI TOSHA TUMEDHARAULIWA NA KUFANYWA WAJINGA HASWA WATANZANIA! SISI SIO MAPUMBUANI NAMNA HIYO!! TUSIPOAMKA LEO TUTASHUHUDIA PICHA WATOTO WANAENDA UCHI HAKUNA NGUO! NA NAFIKIRI TUMESHAFIKIA HUKO WAZALENDO, MAANA HATA HIZO PICHA ZA KAMPENI YA UCHAGUZI, HALI YA WATOTO WANAOONEKANA HAPO!! INGEBIDI HUYO MGOMBEA AJIUZULU SIO KUGOMBEA TENA, NI AIBU KUBWA, NI KAMA HIYO PICHA YA MZEE PINDA ANAPOKEA TUNZO!! TUNZO YA NINI HASA?? SHAME!
ReplyDeleteJK kamwe hawezi kuwaletea watanzania maendeleo. Ni miongoni mwa marais ambao pampja na kuwa madarakani kwa muda mrefu kama Mbunge na waziri katika wizara mbalimabli, ameshindwa hata kusaidia maendeleo ya Jimbo lake la Bagamoyo. Leo hii anapitisha Bakuli kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Bagamoyo chini ya Swahiba wake Shubash Patel kuomba watanzania walalahoi kuchangia Maendeleo ya Jimbo lake. Pamoja na Mipango yote ya kusaidia Elimu, hakuna maendeleo yeyote kwa shule za Msingi na Sekondari za UMMa.
ReplyDeleteVijana wetu bado wanakosa hata pa kuandikia, hawana madawati, hawana waalimu. Achilia mbali huko kwenye Zahanati, wakulima nk.
Tembele Tovuti ya Bodi ya Elimu Badamoyo ujionee mambo hapo ndio utaua JK vipau mbele vyake ni nini:
http://bagamoyoeducationfund.org/html/picture.htm
http://bagamoyoeducationfund.org/html/picture1.htm
Haya ni kule LUDEWA
http://ruhuwiko.blogspot.com/2010/04/hospitali-ya-ludewa-mambo-ndio-haya.html
KAKA, MAMBO YA UONGOZI NI MAGUMU. JARIBU KUKARIA KITI CHA UONGOZI UTAKUBARIANA NAMI
ReplyDelete