Blogu Hii inapenda kuungana na mwanahabari mkongwe,John Bwire, wa jarida la Raia Mwema,katika kipindi hiki kigumu cha msiba wa baba yake mzazi .
Nimepata taarifa hizo kutoka kwa barua pepe aliyonitumia Bwire leo.
Kifo ni kifo,lakini kifo cha mzazi kinagusa mno.Hakuna maneno yanayoweza kuwa mwafaka kabisa kumliwaza mfiwa.Hata hivyo,kuna kauli ya kiroho inayoweza kuleta faraja na matumaini,kwamba SIE TULIMPENDA SANA MAREHEMU LAKINI BWANA MUNGU ALIMPENDA ZAIDI,NA NDIO MAANA AMEAMUA KUMCHUKUA.Ni maneno yanayoweza kuonekana mepesi lakini yana uzito mkubwa.
Pumziko la milele Umpe ee Bwana,na Mwanga wa Milele Umwangazie,Astarehe kwa Amani
Amen
Pole sana Bwana John Bwire! R.I.P mpendwa marehemu!
ReplyDeleteInna Lillahi wainna ilaihi Raajiooun...(IWR) Bwire tupo pamoja nawe katika kipindi hiki kigumu cha majonzi ya kuondokewa na baba mzazi.RABBI Akupe nguvu umuombee maghufira kaburini na akhera...
ReplyDelete