Je wajua kuwa licha ya mgombea wa CCM Jakaya Kikwete kukacha mdahalo na wagombea wa vyama vingine anapatikana kirahisi mtandaoni ambapo "anauza" sera zake na "mafanikio" yake?Kama ulikuwa hufahamu basi nenda Twitter kisha tafuta @Kikwete2010 au nenda Facebook kisha tafuta Jakaya Kikwete.
I know siasa za chama kimoja zimeacha kasumba ya kufurahia kugusana mabega na watawala.No wonder kuna wenzetu muda huu wanakenua meno yote thelathini na kitu kwa vile wamepokea ujumbe kama huu "Kikwete2010 is following you..." au "Salma Kikwete is Following you..."
Si ajabu kuna wenzetu wamefotokopi meseji za aina hiyo wakiamini kuwa Kikwete na mkewe Salma wanawajali saaaana hadi wameamua kuwa-follow up huko Twitter au kuungana nao hapo Facebook.KALAGABAHO!Kwanini hujiulizi WHY NOW?Kikwete na mkewe walikuwa Ikulu tangu Desemba 2005 na HAWAKUKUTAFUTA.Hushangai kwanini leo wanataka urafiki nawe?Well,sio kosa kuwa rafiki na rais au mkewe lakini urafiki huu hauna tofauti na ule wa mtenda tendo la ndoa na kondomu.Zana hiyo (kondom) huwa na umuhimu wa kipekee (kwa wale wanaojali) kabla na wakati wa tendo la ndoa,lakini pindi shughuli ikimalizika kondom huwa ni uchafu usiovumilika.ANGALIA,usijetumika kama kondomu: Kikwete akuone muhimu sasa kwa vile anahitaji kura lakini akakusahau (kama alivyokusahau 2005-till now) baada ya kurejea Ikulu.
Badala ya ku-retweet kila anachoandika,tumia haki yako kama Mtanzania kuhoji masuala mbalimbali yanayolikabili taifa.Twende mbali zaidi ya kupongeza na kuona sifa "kugusana mabega" na watawala.Sio kosa kushabikia lakini ushabiki wenye maana ni ule unaombatana na matumizi sahihi ya akili.
Now you-in case you didn't.Muulize Kikwete,je ile kauli aliyotoa mwaka 2006 kuwa anawafahamu wala rushwa kwa majina ila anawapa muda wa kujirekebisha imefikia wapi?Je wameshajirekebisha?Je anaweza kututajia majina ya waliojirekebisha na waliogoma kufuata ombi hilo la kichovu?
Muulize pia kwamba kabla ya sakata la Richmond aliahidi kuwa tatizo la umeme lingebaki kuwa historia.A few months later,matapeli wa Richmond wakaingia kwenye picha.Today,tatizo la umeme ni as sugu as ufisadi.Mkalie kooni na kumhoji,kama huko nyuma alitoa ahadi ya kutupatia ufumbuzi wa umeme na hakutimiza,kwanini tumwamini sasa?
Muulizie pia kama bado anaamini kuwa mimba za wanafunzi wa kike zinasababishwa na kimbelembele chao.Yah,muulize swali hilo kwa vile hadi sasa bado hajakanusha au kuwaomba msamaha Watanzania kwa kauli hiyo ya kizembe.
Usikose kumuuliza pia kama hadi sasa hajui sababu zinazoifanya Tanzania kuwa masikini maana alinukuliwa akijiuliza swali hilo.Nenda mbali kidogo na kumhoji kama alikuwa hajua kwanini Tanzania ni masikini sasa anafanya nini hapo Ikulu?
Sasa hivi amenzisha hash tag #Mafanikio huko Twitter.Hapo utapata nafasi nzuri ya kujionea waziwazi namna Awamu ya Nne ya Kikwete ilivyoshindwa kuikomboa Tanzania kutoka kwenye umasikini licha ya raslimali lukuki tulizonazo.Hapo Kikwete na wapambe wake wanataja mapato yaliyotokana na utalii na madini.Mkalie kooni na kumhoji kama mapato ndio hayo,kwanini sie bado masikini?Fedha hizo zimeenda wapi kama sio kwenye akaunti za mafisadi?Na kwenye utalii muulize pia kuhusu meno ya tembo yaliyokamatwa huko Hong Kong yakitokea Tanzania.
Kumbuka,usikubali kutumika kwa maslahi ya mtu mwingine.Kumhoji mwanasiasa anayeomba kukuongoza ni haki yako.Usiichezee.Badala ya kujipendekeza kwa RT (Retweets za Kikwete2010) tumia fursa hiyo kumuuliza maswali ya msingi yanayohitaji majibu ya haraka.
PAMOJA TUNAWEZA
JK ni ghiliba tuu siyo kiongozi makini mbabaishaji ushahidi unajionesha katika utendaji wake na kauli anazotoa haitaji kuwa malaika kumjua kwamba nafasi anayoiomba tena inamzidi uwezo wake wa kiungozi na utawala.
ReplyDeleteKwanza kabla ya uchaguzi itabidi aende USA au kwingineko ku .... d.... halafu zile ahadi zitasahaulika au atasema namwachia anyenifuata. Meli na viwanja vitaota mbawa ila vijisenti havitakoma kuhamishwa.
ReplyDeleteKikwete angejua wananchi walivyomchoka angeaga tu salama akapumzike amuachie mwingine. Anavyoongea ndio wananchi tunamuelewa alivyo na empty mind. Lakini kwa mtindo huu mwisho wake aibu si yake tu bali ya chama kizima.Sijaona raisi anasikia mtu anasema analindwa na majini alafu amekaa kimya tu au ndio ukweli wenyewe. Ukishaona mtu anatumia muda mwingi wa ushirikina ujue kichwani hamna lolote ni Zero.
ReplyDelete