Sunday, 26 February 2012


Kwa Waafrika wengi,na pengine kwingineko ulimwenguni,Wanigeria wanatamba kwa sifa kuu mbili;moja mbaya  na nyingine nzuri.Mbaya ni tabia yao ya utapeli ambapo ni bora kulala na chatu mwinye njaa kuliko kumwamini Mpopo.Wenye uzoefu nao wanajua ninamaanisha nini.Sifa yao nzuri-hasa kwa wanaume ni kutamba katika soka takriban kila kona ya dunia.Inayoambatana na hiyo ni mfaniko makubwa waliyonayo wengi wao-hasa nje ya nchi (usiulize wameyapataje).

Katika hili la mafanikio,juzi juzi tu tumesikia wanamuziki kadhaa wa Kipopo wakivamia anga za muziki nchini Marekani ambapo tayari majina makubwa kama Snoop Dogg na Akon wameshafanya kazi nao.D'Banj kwa sasa anafanya kazi kwenye lebo ya G.O.O.D Music ya Kanye West



Kwa upande mwingine,wanamuziki maarufu wa Kinigeria P.Square, 2Face Idibia na Whizkid wamesaini kwenye lebo ya Konvict ya Akon.



Na wiki hii,gazeti maarufu la nchini Marekani la New York Times lina makala ndefu kuhusu kiwanda cha filamu za Nigeria kinachojulikana kama Nollywood.Unaweza kusoma makala hiyo ndefu HAPA.

Maendeleo haya ya wasanii wa kipopo yanaweza kuwa changamoto kubwa kwa wasanii wetu huko nyumbani.Japo kuna dalili kidogo za kutia matumaini baada ya wasanii AY na Jay Mo kushirikiana na wasanii wa kimataifa,kimsingi wengi wa wasanii wetu wanaendelea kutafsiri mafanikio kwa kigezo cha umaarufu ndani ya Tanzania (na kidogo kwa Afika Mashariki) na kuendekeza zaidi shoo za hapa na pale.




0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget