Wednesday, 31 December 2008
Tuesday, 30 December 2008
HATIMAYE TUMEFIKA MWISHO WA MWAKA 2008.SIJUI MWENZANGU KWAKO MWAKA HUU TUNAOUMALIZA LEO ULIKUWAJE LAKINI BINAFSI 2008 IMENIACHA NA PENGO AMBALO HALITOZIBIKA HADI KIFO CHANGU.TAREHE 29 MEI NILIMPOTEZA MAMA YANGU MZAZI,MAREHEMU ADELINA MAPANGO.KIFO HICHO KILIHITIMISHA SAFARI YAKE NGUMU NA YA MAUMIVU ILIYOANZA MWISHONI MWA MWEZI FEBRUARI AMBAPO ALIANGUKA NA KUPOTEZA FAHAMU.ILINILAZIMU KWENDA TANZANIA MWEZI MACHI NIKIWA NA MATUMAINI KWAMBA HUENDA HALI YAKE INGEBADILIKA LAKINI KWA BAHATI MBAYA HADI ANAFARIKI SIKUPATA BAHATI YA KUONGEA NAE HATA NENO MOJA.MARADHI NA KIFO CHA MAMA VILIPELEKEA KUSHINDWA KWANGU KUHITIMU MASOMO YANGU MWEZI NOVEMBA KUTOKANA NA KUTUMIA TAKRIBAN MIEZI MITANO HUKO NYUMBANI NIKIUGUZA NA KUSHUGHULIKIA TARATIBU ZA MAZISHI NA AROBANI.BWANA ALITOA NA BWANA ALITWAA,LAKINI PENGO ALILOACHA MAMA HALITOZIBIKA MILELE,NA TUKIO HILO NDILO LILILOKUWA KUBWA ZAIDI KWANGU KWA MWAKA HUU TUNAOUMALIZA LEO.
MATUKIO MENGINE NILIYOFANIKIWA KUYAWEKA BLOGUNI AU KUYAFUATILIA KWA KARIBU KUANZIA MWEZI JANUARI NI KAMA IFUATAVYO:
MIONGONI MWA MATUKIO MAKUBWA YA MWEZI JANUARI ILIKUWA NI PAMOJA NA VURUGU ZILIZOJITOKEZA BAADA YA UCHAGUZI MKUU NCHINI KWENYE AMBAPO WAFUASI WA MGOMBEA RAILA ODINGA WALIDAI WAMEPORWA USHINDI NA MWAI KIBAKI.TUKIO JINGINE KUBWA LILIKUWA KIFO CHA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA PAKISTAN BENAZIR BHUTTO.MAFURIKO NCHINI MSUMBIJI YAUA WATU KADHAA NA KUACHA MAELFU WAKIWA HAWANA MAKAZI.GEORGE W. BUSH ASOMA STATE OF THE UNION ADDRESS KWA MARA YAKE YA MWISHO (HATOKUWA MADARAKANI 2009).PIA SERIKALI ILIYOKUWA CHINI YA WAZIRI MKUU WA ITALIA,ROMANO PRODI,YAVUNJIKA.KADHALIKA,BALOZI WA TANZANIA HUKO AFRIKA KUSINI,EMMANUEL MWAMBULUKUTU APIGWA.SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU ISHU YA EPA.TUKIO JINGINE MUHIMU LILIKUWA KUCHAGULIWA KWA JK KUWA MWENYEKITI WA UMOJA WA AFRIKA (AU).
MWEZI FEBRUARI ULISHUHUDIA UJIO WA RAIS BUSH NCHINI TANZANIA NA KUNG'OKA KWA EDWARD LOWASSA KWENYE UWAZIRI MKUU KUFATIA TUHUMA ZA KAMPUNI YA KITAPELI YA RICHMOND.PIA KATIKA MWEZI HUO KULIKUWA NA KIOJA CHA SPIKA SAMUEL SITTA KUMTAKA NAIBU WAKE ANNE MAKINDA "ASIKURUPUKE" KUENDESHA MJADALA WA ISHU YA RICHMOND HADI HAPO SPIKA ATAPOREJEA KUTOKA SAFARINI UGHAIBUNI.BAADAYE SPIKA ALIAHIRISHA SAFARI HIYO,NA WOTE TUNAJUA KILICHOJIRI BAADA YA MJADALA HUO WA KIHISTORIA.KUJIUZULU KWA LOWASSA KULIMPELEKEA JK KUVUNJA KABINETI YAKE NA KISHA KUMTEUA BW MIZENGO PINDA KUWA WAZIRI MKUU HUKU SURA NYINGI ZA BARAZA LA MAWAZIRI WA ZAMANI ZIKIREJEA.KATI YA WALIOLALAMIKIWA SANA KUTEULIWA KWENYE BARAZA JIPYA NI PAMOJA NA "MZEE WA VIJISENTI" ANDREW CHENGE.PIA KATIKA MWEZI HUO,RAIS MWANAMAPINDUZI WA CUBA,FIDEL CASTRO ALING'ATUKA MADARAKANI.TUKIO JINGINE LILILOVUTA HISIA ZA JAMII YA WATANZANIA MTANDAONI NI KUFUNGIWA KWA JAMBO FORUMS NA WAHUSIKA WAKE WAWILI KUKAMATWA.HATA HIVYO MTANDAO HUO MAHIRI ULIREJEA HEWANI BAADA YA SIKU CHACHE UKIWA NA JINA JIPYA LA JAMII FORUMS.
MWEZI MACHI ULIANZA KWA KUTAWALIWA NA HABARI ZA KINYANG'ANYIRO CHA UCHAGUZI NCHINI MAREKANI AMBAPO MGOMBEA WA CHAMA CHA REPUBLICAN,JOHN MCCAIN,ALI-WIN NOMINATION YA CHAMA CHAKE.PIA SUPER-TUESDAY NDANI YA CHAMA CHA DEMOCRAT ILIZIDISHA MPAMBANO KATI YA HILLARY CLINTON NA BARACK OBAMA.MACHI PIA ILISHUHUDIA KUSAMBARATIKA KWA SERIKALI YA SERBIA.VILEVILE,WAKRISTO SEHEMU MBALIMBALI DUNIANI WALIADHIMISHA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA BWANA YESU KRISTO KATIKA SIKUKUU YA PASAKA.WIKI YA MWISHO YA MACHI ILISHUHUDIA REPORTING YA BLOG HII KUTOKA TANZANIA BAADA YA MIE MTUMISHI WAKO KUELEKEA HUKO KUMUUGUZA MZAZI WANGU.
REPORTING LIVE AND DIRECT KUTOKA BONGO,BLOG ILIANZA MWEZI APRILI KWA PICHA KADHAA ZA KUTOKA NYUMBANI.HII ILIKUWA TRANSITION MUHIMU KWA BLOG YENU KWANI NDIO LILIKUWA JARIBIO LA KWANZA LA KUCHANGANYA NEWS ANALYSIS NA PHOTOBLOGGING.NIKIRI KWAMBA BADO NIKO NYUMA SANA IN THE LATTER.BLOG ILIWALETEA PICHA ZINAZOONYESHA HALI HALISI ILIVYO KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI.PIA KULIKUWA NA MAKALA KUHUSU HUDUMA MBOVU KWENYE HOSPITALI YA REGENCY.KADHALIKA,KULIKUWA NA "BREAKING NEWS YA KIMTINDO" YA MAFURIKO HUKO IFAKARA PAMOJA NA PICHA ZA ADHA YA USAFIRI WILAYANI KILOMBERO.VILEVILE,BLOG ILIJITAHIDI KUUFAHAMISHA UMMA KUHUSU MAPUNGUFU MBALIMBALI KWENYE HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA TAASISI MBALIMBALI ZA HUKO NYUMBANI.MIONGONI MWA HABARI KUBWA ZA MWEZI HUU ILIKUWA NI PAMOJA NA KUJIUZULU KWA MZEE WA VIJISENTI ANDREW CHENGE.
NI VIGUMU KUFANYA EFFECTIVE BLOGGING WAKATI UNAUGUZA MTU MUHIMU KATIKA MAISHA YAKO KAMA MZAZI.KASI YA KU-BLOG NA KU-UPDATE BLOG ILIPUNGUA MWEZI MEI BAADA YA HALI YA MAMA KUZIDI KUDHOOFIKA.KIPINDI HIKI KILINIPA FURSA NZURI YA KUTAMBUA SOME HIDDEN SOCIAL BENEFITS ZA BLOGGING KWANI NILIPATA SALAMU NYINGI ZA SAPOTI KUTOKA KUTOKA KWA WATU NISIOWAFAHAMU LAKINI TULIOJUANA KUPITIA SEHEMU HII AMBAO WALIKUWA WAKINIPA MOYO KATIKA KIPINDI HICHO KIGUMU.PIA MWEZI MEI ULISHUHUDIA SHIRIKA LA NDEGE LA ATC LIKIINGIZA KWA MBWEMBWE DEGE MTUMBA LA AIRBUS A320.WAJUZI WA MAMBO WALIHOJI HATUA HIYO HUKU WAKISISITIZA KWAMBA HUO NI MWENDELEZO WA UFISADI.KADHALIKA,MZEE WA VIJISENTI ANDREW CHENGE ALIZUSHIWA KIFO KABLA YA HABARI HIYO KUKANUSHWA NA FAMILIA YAKE.PIA TAIFA STARS ILIFANYA KWELI KWA KUIBAMIZA THE CRANES 2-0.PIA RAPA MAARUFU 50 CENT ALITUA DAR NA KUFANYA ONYESHO MOJA.ILIFAHAMIKA PIA KWAMBA ALIYEKUWA GAVANA WA BoT DAUDI BALLALI AMEFARIKI HUKO MAREKANI.HABARI HIYO ILIGUBIKWA NA USIRI MKUBWA KIASI CHA BAADHI YA WATU KUHISI NI CHANGA LA MACHO.TAREHE 29 YA MWEZI HUU,SAA 4.30 USIKU (TANZANIAN TIME),MAMA YANGU MPENDWA ALIAGA DUNIA.THIS WAS THE DARKEST DAY OF MY LIFE.
JUNI ILIANZA KWA KUMZIKA MAMA MNAMO TAREHE 2.SINTAISAHAU SIKU HII MAISHANI MWANGU ASILANI.
MATUKIO MENGINE KATIKA MWEZI HUO NI PAMOJA MKUTANO WA LEON SULLIVAN ULIOFANYIKA HUKO ARUSHA HUKU BAADHI YA WAFANYABIASHARA WA NDANI WAKILAUMU KWA KUTELEKEZWA NA WAANDAAJI.TAIFA STARS ILIBORONGA HUKO CAPE VERDE BAADA YA KUTANDIKWA BAO 1-0.PIA MASHABIKI WA SOKA DUNIANI WALIELEKEZA MACHO NA MASIKIO YAO KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA MICHUANO YA EURO 2008 AMBAPO HISPANIA ILIIBUKA KIDEDEA.BAJETI YA SERIKALI YASOMWA,MAUMIVU KWA WALALAHOI YAENDELEA.TIMU YA TAIFA YA CAMEROON YATOKA SULUHU NA TAIFA STARS JIJINI DAR HUKU MASTAA KAMA SAMUEL ETOO WAKIWA KIVUTIO.MABONDIA 6 WA TANZANIA WATIWA MBARONI HUKO MAURITIUS KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA UNGA.JENGO MOJA LA GHOROFA LILILOPO JUNCTION YA ZANAKI/KISUTU STR LAPOROMOKA .TAIFA STARS YANYUKWA 2-1 HUKO CAMEROON.OBAMA ASHINDA KUWA MGOMBEA WA CHAMA CHA DEMOCRAT.MAKALA YANGU KWENYE GAZETI LA RAIA MWEMA LA TAREHE 26 IKITABIRI KIFO CHA CCM (KAMA KILIVYOTABIRIWA NA BABA WA TAIFA) YAZUA SONGOMBINGO NA HATIMAYE KUFIKIA UAMUZI WA KUCHUKUA SABBATICAL LEAVE YA UANDISHI WA MAKALA.
MWEZI JULAI UNAANZA KWA PILIKAPILIKA ZA SABA SABA LAKINI UCHUMI MBOVU JAPO VITU KIBWENA KWENYE MABANDA HUKO KILWA ROAD.RAIS WA SHRIKISHO LA NDONDI TANZANIA,ALHAJI SHABAN MWINTANGA ATIWA MBARONI KUHUSIANA NA SAKATA LA MABONDIA WALIKAMATWA NA UNGA HUKO MAURITIUS.MSANII WA BONGOFLEVA T.I.D ATUPWA JELA MWAKA MMOJA.YANGA WAFANYA KITKO CHA KIHISTORIA:WAINGIA MITINI SIKU YA MPAMBANO KATI YAO NA SIMBA.MBUNGE MACHACHARI NA MAKAMU MWENYEKITI WA CHADEMA,CHACHA WANGWE,AFARIKI KWA AJALI YA GARI HUKO DODOMA.MAHAKAMA YA KIMATAIFA (ICC) YATOA WARRANT YA KUKAMATWA KWA RAIS WA SUDAN,OMAR AL-BASHIR,KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA MAUAJI YA HALAIKI HUKO DARFUR.MHALIFU WA KIVITA,RADOVAN KARADZIC,AKAMATWA KUHUSIANA NA MAUAJI YA HALAIKI HUKO SERBIA.
AGOSTI,MREMBO NASREEM ATWAA TAJI LA MISS TANZANIA 2008.AJALI MBAYA YA BASI YAPOTEZA MAISHA YA WATU 10 NA WENGINE 30 KUJERUHIWA HUKO MBEYA.MWANAMUZIKI SHAGGY ATUA DAR NA KUFANYA ONYESHO.MAANDAMANO NA VURUGU ZATANDA NCHINI VENEZUELA,NA HUKO GEORGIA MAJESHI YA RUSSIA YAENDELEZA UBABE WAKE.HABARI NYINGINE KATIKA MWEZI HUU ILIKUWA NI KUJIUZULU KWA RAIS WA PAKISTAN PERVEZ MUSHARRAF.TUKIO JINGINE KUBWA LILIKUWA NI MICHEZO YA OLIMPIKI HUKO CHINA,NA KWA NYUMBANI WATANZANIA WALITEGESHA MASIKIO YAO HUKO DODOMA WAKATI JK ALIPOHUTUBIA BUNGE.WENGI WALITEGEMEA KUSIKIA HATIMA YA ISHU ZA EPA,RICHMOND NA UFISADI MWINGINE LAKINI HAYO YALIGUSIWA JUU JUU TU.AGOSTI PIA ILISHUHUDIA RAIS WA VISIWA VYA KOMORO,AHMED ABDALLAH MOHAMMED,AKIHUTUBIA BUNGE LA MUUNGANO DODOMA.PM MIZENGO PINDA ASOMA TAARIFA KUHUSU ISHU YA RICHMOND.KAMA KAWAIDA,NI TAARIFA TU HAKUNA ALIYEWAJIBISHWA SO FAR.JK AMTEMBELEA BUSH HUKO WHITE HOUSE NA MWEZI WA TOBA WAANZA.RAIS MWANAWASA WA ZAMBIA AFARIKI DUNIA.
SEPTEMBA YAANZA KWA HABARI ZA VIMBUNGA IKE NA GUSTAV.ASIF ALI ZARDARI,MJANE WA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA PAKISTAN BENAZIR BHUTTO,ACHAGULIWA KUMRITHI JENERALI MUSHARAF.TETESI ZAZUKA KUHUSU AFYA YA KIONGOZI WA KORA YA KASKAZINI,KIM JUNG IL,IKIDAIWA KWAMBA AMEKUFA LAKINI NCHI HIYO YAKANUSHA HABARI HIZO.JONGWE MUGABE NA MORGAN TSHANGIRAI WAFIKIA MAKUBALIANO YA UONGOZI HUKO ZIMBABWE.MLIPUKO WA BOMU KATIKA HOTELI YA MARRIOT HUKO ISLAMABAD PAKISTAN WAUA NA KUJERUHI WATU KADHAA.KESI YA ZOMBE YAENDELEA KUUNGURUMA HUKO NYUMBANI.JACOB ZUMA NAE ATUA DAR.JAPAN YAPATA WAZIRI MKUU MPYA,TARO ASO,AMBAYE NI MKATOLIKI WA KWANZA KUSHIKA WADHIFA HUO NCHINI HUMO.UCHAGUZI WAFANYIKA NCHINI BELARUS LAKINI WAANGALIZI WA KIMATAIFA WADAI HAUKUWA FREE AND FAIR.PIA SAKATA LA MAZIWA YENYE WALAKINI HUKO CHINA YAPAMBA MOTO KWENYE ANGA ZA HABARI.MSHIRIKI WA TANZANIA KWENYE BIG BROTHER AFRICA 3 ATOLEWA MASHINDANONI,CHA AJABU AREJEA BONGO KAMA SHUJAA NA KUANDALIWA PATI YA PONGEZI!RAIS WA AFRIKA KUSINI,THABO MBEKI AJIUZULU.WAFANYAKAZI WA BENKI YA NMB WAGOMA NA KUSABABISHA USUMBUFU MKUBWA KWA WATEJA.SHEREHE ZA IDD EL FITR ZAKUMBWA NA BALAA BAADA YA VIFO VYA WAOTO 20 MJINI TABORA.USTAADH MMOJA MWENYE MSIMAMO MKALI HUKO SAUDI ARABIA ASOMA FATWA DHIDI YA MICKEY MOUSE KWA MADAI KUWA KIKARAGOSI HICHO NI WAKALA WA SHETANI!
ANGA ZA HABARI ZA KIMATAIFA MWEZI OKTOBA ZILIANZISHWA NA TAARIFA ZA WATEKA MELI (PIRATES) HUKO SOMALIA AMBAPO SAFARI HII WATEKA MELI KUTOKA UKRAINE ILYOKUWA NA VIFARU 33.UCHUMI WA DUNIA WAZIDI KWENDA HARIJOJO NA WASIWASI WAJITOKEZA KUHUSU UWEZEKANO KUFILISIKA KWA NCHI YA ICELAND.NENO ECONOMIC BAILOUT LAWA KAMA SALA KWENYE VYOMBO VYA HABARI VYA KIMAIFA HASA BAADA YA RAIS BUSH KUIDHINISHA BAILOUT YA DOLARI BILIONI 700 KUOKOA UCHUMI WA MAREKANI,NA NCHI KADHAA KUFUATA MKONDO.CHADEMA WASHINDA UCHAGUZI MDOGO WA TARIME ULIOAMBATANA NA KILA AINA YA VITUKO.OBAMA AENDELEA KUTESA KWENYE OPINION POLLS ZA UCHAGUZI MKUU WA MAREKANI.JK AZURU MBEYA,ZIARA YAGUBIKWA NA HABARI ZA MSAFARA WAKE KUTUPIWA MAWE.PIA JK ATAWAZWA KUWA "CHIFU MWANGUPILI" WA WANYAKYUSA.GAZETI LA MWANAHALISI LAFUNGIWA NA SERIKALI KWA MIEZI MITATU.RAIS WA MADAGASCAR AZURU TANZANIA.WALIMU DAR WAMPA KISAGO RAIS WA CHAMA CHAO BAADA YA KUTANGAZA KUAHIRISHWA KWA MGOMO.COLLIN POWELL AM-ENDORSE OBAMA,NA MPANGO WA KUM-ASSASSINATE OBAMA WADHIBITIWA.PIA KATIKA MWEZI HUU,SAKATA LA TANZANIA KUJIUNGA NA OIC NA LILE LA KUANZISHWA KWA MAHAKAMA YA KADHI LILITAWALA SANA HUKU MAASKOFU NA VIONGOZI WA KIISLAM WAKIRUSHIANA MANENO.HATARI LAKINI BADO SALAMA.HUKO DRC MAPAMBANO KATI YA MAJESHI YA SERIKALI NA YA WAASI CHINI YA GEN LAURENT NKUNDA YAZIDI KUPAMBA MOTO.
NOVEMBA YAINGIA NA MSISIMKO WA UCHAGUZI WA MAREKANI,NA KAMA ILIVYOTARAJIWA,OBAMA ASHINDA NA KUWEKA HISTORIA YA KUWA MWEUSI WA KWANZA KUWA RAIS WA NCHI HIYO.MALKIA WA DENMARK AZURU TANZANIA.WASANII WA KAMPUNI YA DOWANS WATANGAZA TENDA YA KUUZA MITAMBO YAO MITUMBA.SERIKALI YAFANYA BAILOUT NYINGINE KWA WAHINDI WA TRL,YALIPA TENA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI.WAKATI "JAMES BOND WA SASA" CRAIG DANIEL AKISEMA DUNIA IKO TAYARI KWA "JAMES BOND MWEUSI" (A BLACK BOND),WAJUZI WA MAMBO WADAI KWAMBA HAKUNA UWEZEKANO WA KUWEPO A "BRITISH OBAMA" (PM MWEUSI).MKURUGENZI WA TAKUKURU,EDWARD HOSEA,ADAI KWAMBA WATUHUMIWA WOTE WA EPA WAKIKAMATWA NCHI ITAYUMBA!MAMIA WAFA BAADA YA MASHAMBULIZI YA KIGAIDI HUKO MUMBAI,INDIA.MAMIA WAFA NIGERIA KUFIATIA VURUGU ZA KIDINI NCHINI HUMO.WIMBI LA MIGOMO NA KUFUNGWA KWA VYUO VIKUU LASAMBAA HUKO NYUMBANI.WATUHUMIWA KADHAA WA EPA WAFIKISHWA KORTINI,MRAMBA NA YONA NAO WAFIKISHWA KORTINI,WENGI WAJIULIZA: JUSTICE AT LAST AU CHANGA LA MACHO?
HATIMAYE TUMEINGIA DESEMBA,MWISHO WA MWAKA.MAUAJI DHIDI YA ALBINO YAENDELEA HUKO NYUMBANI NA HAKUNA DALILI YA UFUMBUZI WA TATIZO HILO.VURUGU ZA UGIRIKI ZASAMBAA HADI NCHI NYINGINE ZA ULAYA.BUSH AKUMBWA NA KIMBEMBE HUKO IRAK BAADA YA KUVURUMUSHIWA VIATU NA PAPARAZI MMOJA WAKATI WA PRESS CONFERENCE.UCHAGUZI MKUU NCHINI TURKMENISTAN WAELEZEWA KUWA NI KIINIMACHO NA SIO HURU NA HAKI.KATIBU MKUU WA ZAMANI WA WIZARA YA FEDHA,GRAY MGONJA,NAE APANDISHWA KZIMBANI KWA TUHUMA ZA UFISADI.MEMBE AONYA CCM INAWEZA KUSAMBARATIKA,NAPE NNAUYE AMTUHUMU MAKAMBA KUWA ANAKUMBATIA MAFISADI.HALI YA USALAMA NCHINI SOMALIA YAZIDI KUWA MBAYA KUFUATIA MAPIGANO KATI YA KOO MBALIMBALI NCHINI HUMO.MASTERMIND WA MAUAJI YA KIMBARI NCHI RWANDA,THEONESTE BAGOSORA,AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA.TAKUKURU YAKURUPUKA NA KUDAI HAIMCHUNGUZI MKAPA (SIJUI NANI ALIWAULIZA!).KAPTENI MOUSSA DADIS KAMARA AJITANGAZA RAIS WA GUINEA KATIKA MAPINDUZI YALIYOFUATIA KIFO CHA RAIS LANSANA CONTE.PM PINDA ACHACHAMAA KUHUSU MAGARI YA KIFAHARI SERIKALINI,ILA NI KUANZIA MWAKANI KWANI TAYARI SHEHENA YA MAGARI 700 NA USHEE IMESHAAGIZWA!BEI YA MAFUTA SOKO LA DUNIA YAZIDI KUSHUKA LAKINI BEI YA BIDHAA HIYO HUKO NYUMBANI BADO IKO JUU KABLA YA KUKUMBWA NA UHABA USIOELEZEKA.NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI,AELEZA KWAMBA SERIKALI HAIFAHAMU KWANINI BEI YA MAFUTA IKO JUU LAKINI AKADAI YAKO KIBAO KUKIDHI MAHITAJI.AIAGIZA EWURA IKAE KITAKO NA WAFANYABIASHARA KUHUSIANA NA ISHU HIYO (JAPO AGIZO LA EWURA HIYOHIYO KUWATAKA WAFANYABIASHARA HAO KUPUNGUZA BEI YA MAFUTA LIMEENDELEA KUPUUZWA).ATCL YAENDELEA KUSUASUA JAPO UONGOZI WAKE BADO UNAENDELEA KUPETA.MGOMBEA WA CHADEMA KATIKA UCHAGUZI MDOGO MBEYA VIJIJINI AENGULIWA BAADA YA KUWEKEWA PINGAMIZI NA CCM NA CUF,ADAI AMESHAKATA RUFAA.PIA DESEMBA ILISHUHUDIA TAJIRI WA KIMAREKANI BERNARD MADOFF AKIWALIZA WAWEKEZAJI TAKRIBAN DOLA BILIONI 50 KWENYE PONZI SCHEME.
KWA KIFUPI,HAYO NDIYO MATUKIO YA KUKUMBUKWA NA BLOG HII.NAWASHUKURU NYOTE MNAONITEMBELEA.NAAHIDI KUENDELEA KUWALETEA KILE KITU ROHO ZENU ZINAPENDA.MSISITE KUNIKOSOA,KUNISHAURI NA KUTOA MAONI YENU.BLOGU HII NI YENU NAMI NI MTUMISHI WENU.NAWATAKIA HERI NA BARAKA YA MWAKA 2009.MUNGU AWABARIKI SANA.
MGOMBEA WA CHADEMA KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA MBEYA VIJIJINI,SHAMBWEE SHITAMBALA,AMEENGULIWA NA TUME YA UCHAGUZI KUTOKANA NA KASORO ZILIZOJITOKEZA.KWA MUJIBU WA GAZETI LA Mwananchi NA Tanzania Daima,SHITAMBALA AMBAYE NI WAKILI KITAALUMA,ALIWEKEWA PINGAMIZI NA VYAMA VYA CUF NA CCM AKIDAIWA KULA KIAPO KATIKA OFISI YAKE YA UWAKILI BADALA YA MBELE YA HAKIMU.PIA PINGAMIZI DHIDI YA MWANA-CHADEMA HUYO LILIWEKWA KUTOKANA NA MADAI KWAMBA HAKUJAZA KATIKA FOMU ZA KUGOMBEA IWAPO ALISHAWAHI KUSHTAKIWA AU LA.
HABARI ZAIDI ZINAELEZA KWAMBA MGOMBEA HUYO AMESHAKATA RUFAA HUKU CHAMA CHAKE KIKIONEKANA KUWA NA MSIMAMO HUO PIA.LAKINI KAMA ILIVYO ADA,TAYARI HATUA HIYO IMEANZA KUTAFSIRIWA KAMA MBINU ZA CCM KUUHUJUMU UCHAGUZI HUO.
CHADEMA WANAWEZA KUSEMA LOLOTE KUHUSIANA NA HATUA HIYO LAKINI IWAPO RUFANI YA CHAMA HICHO ITAKATALIWA NA HIVYO MGOMBEA WAKE KUTOSHIRI KATIKA UCHAGUZI HUO,BASI LAWAMA ZOTE ZITAPASWA KUELEKEZWA SIO KWA CCM AU TUME YA UCHAGUZI BALI KWA CHADEMA YENYEWE.HIVI HUYU SHITAMBALA KAMA MWANASHERIA HAKUJUA KUWA ALICHOKIFANYA KINGEWEZA KUMGHARIMU NAFASI YA KUGOMBEA KATIKA UCHAGUZI HUO?IT DOESN'T MAKE ANY SENSE KUDAI SASA KWAMBA SHERIA YA UCHAGUZI INA KASORO AU IMEPITWA NA WAKATI KWA VILE SHERIA HIYOHIYO NDIO ILIYOTUMIKA TARIME AMBAKO CHADEMA ILIIBUKA MSHINDI.HIZI NDIO SIASA ZA ZIMAMOTO,MPAKA TUKIO BAYA LITOKEE NDIPO KUNAKUWA NA REACTIONS FLANI.
KWA MTINDO HUU,CCM ITAENDELEA KUTAWALA KWA MUDA MREFU SANA SIO TU KWA VILE INA MBINU KADHAA ZA KUWADHIBITI WAPINZANI BALI PIA KWA VILE VYAMA VYENYEWE VYA UPINZANI VINAASHIRIA KUTOKUWA TAYARI KUWA MBADALA WA CCM.SHERIA MBAYA ZINAPASWA KUONDOLEWA SI TU KWA VILE ZINAATHIRI MGOMBEA WA CHAMA FLANI BALI MASLAHI YA TAIFA KWA UJUMLA,NA CHADEMA ILIPASWA KULI-ADDRESS HILO MAPEMA ZAIDI KULIKO SASA AMBAPO WAMEKUWA VICTIM WA UDHAIFU WAO.I HOPE THEY LEARN SOMETHING FROM THIS NEGLIGENCE.
Monday, 29 December 2008
- 20:05
- Unknown
- ATCL, MATTAKA, NYANG'ANYI
- 3 comments
Pichani,Mkurugenzi Mkuu wa ATCL David Mattaka akiteremka kutoka kwenye ndege iliyonunuliwa na shirika hilo mwezi Februari mwaka huu.Picha kwa hisani ya HAKI.
HEBU SOMA KWANZA HABARI IFUATAYO KISHA TUIJADILI PAMOJA.
Mali za ATCL zakamatwaBenki ya Stanbic Tanzania Limited, Makao Makuu ya Kinondoni, Dar es Salaam, inayashikilia magari sita ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), baada ya kushindwa kulipa deni la Sh bilioni mbili iliyochukua kama mkopo.Fedha hizo zinazodaiwa kushindwa kulipwa kwa miezi miwili sasa zilikopwa na wafanyakazi wa kampuni kwa mikopo na kutokana na kushindwa kuwalipa mishahara watumishi wake, makato ya kila mwezi yameshindikana kukatwa.Taarifa zilizopatikana kutoka ATCL na katika benki hiyo jana zilithibitisha kushikiliwa kwa magari matano aina ya Toyota Land Cruiser VX, kuanzia Jumanne jioni wiki iliyopita na gari la sita limekamatwa likiwa mjini Moshi, Kilimanjaro na lilipelekwa katika benki hiyo jana na kufanya idadi ya magari hayo kuwa sita.Namba za magari hayo ambazo ‘HabariLeo’ jana ilizipata katika eneo la chini la maegesho yalikohifadhiwa magari hayo japo uongozi wa benki uliokuwapo haukuwa tayari kuzungumza kwa madai kuwa msemaji yupo likizo, ni SU 37079, SU 37081, SU 37082, SU 37086, SU 37083 na lililofikishwa jana ni SU 37084.Habari zaidi kutoka eneo la benki yalikohifadhiwa magari hayo zilieleza jana kuwa yataendelea kushikiliwa mpaka deni hilo lililipwe na uamuzi huo ulifikiwa baada ya hofu kuwa huenda kampuni hiyo ikafa na hivyo benki hiyo ikakosa kila kitu.Gazeti hili lilifika makao makuu ya Stanbic makutano ya barabara za Ali Hassan Mwinyi na Kinondoni, na mhudumu wa mapokezi alieleza kuwa wasemaji waliokuwapo hawakuwa tayari kulizungumzia, na mwenye dhamana ya kutoa taarifa hiyo ni Mkurugenzi Mkuu, Bashir Awale, yuko likizo.Hata hivyo, taarifa za ndani ya benki hiyo zililieleza gazeti hili kuwa deni wanaloidai ATCL ni Sh bilioni mbili kwa mwezi huu na kwamba uamuzi wa haraka ulichukuliwa baada ya akaunti ya kampuni hiyo kwa benki hiyo kuonyesha haina fedha za kulipa deni hilo wala haitarajii kuwa nazo kwa siku za karibuni.Chanzo chetu cha habari ndani ya ATCL kilieleza kuwa magari hayo yalikamatwa tangu wiki iliyopita isipokuwa la Mkurugenzi Mtendaji ATCL, David Mattaka. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya ATCL, Balozi Mustafa Nyang’anyi, alithibitisha jana kupata taarifa ya kukamatwa kwa magari hayo na ameitisha kikao cha dharura kitakachokaa leo makao makuu ya kampuni hiyo.Alisema pamoja na suala hilo, pia watajadili mambo mengine likiwamo la kurejeshewa leseni ya kurusha ndege waliyonyang’anywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Desemba 8, mwaka huu.ATCL ilinyan’ganywa leseni hiyo baada ya kubainika kuwa na dosari za kiufundi zinazosababisha kutokuwa na viwango stahili vya kiusalama vya kuwaruhusu kurusha ndege; ukaguzi uliowataka warekebishe dosari hizo ulifanywa Oktoba mwaka jana na leseni hiyo iliisha kazi tangu Aprili mwaka huu, lakini walikuwa wakiongezewa muda mpaka iliposhindikana wakanyang’anywa leseni hiyo.“Hilo jambo na mimi nimepewa taarifa, lakini kusema ni kiasi gani au ni deni linahusu nini, mimi siyo menejimenti, mpigie Mattaka, ila ninachoweza kusema ni kwamba deni hilo si kitu cha ajabu maana tulikabidhiwa kampuni na deni la shilingi bilioni kumi na tisa,” alisema Balozi Nyang’anyi na kuongeza: “Ufafanuzi zaidi sina.Mnashangaa hilo, kuna na la BP, pia waliokuwa wanatusambazia chakula kwenye ndege… na mengine mengi, yote hayo tutayajadili kesho katika kikao cha dharura na menejimenti nilichokiitisha, tutazungumza hayo na mengine mengi.”Alisema katika kikao hicho pia watazungumzia mishahara ya wafanyakazi ambayo mpaka jana walikuwa hawajapata na pia kupanga namna ya kurudi tena katika uzalishaji mara watakaporejeshewa leseni ya kurusha ndege tena.Mattaka alipoulizwa jana kuhusu kushikiliwa kwa magari, alikanusha kwa kudai taarifa hizo si za kweli, lakini alikiri kuwapo kwa kikao cha Bodi na Menejimenti alichokiita kuwa ni kikao cha kawaida si cha dharura. “Hizo habari umetoa wapi? Si kweli, nasema si kweli?” alisema huku mwandishi akiendelea kumhoji.“Kuhusu kikao ni kweli kipo, lakini si cha dharura, ni cha kawaida……naomba unitafute kesho baada ya kikao kuhusu hilo unalotaka kujua,” alisema Mattaka. Hivi sasa TCAA inaendelea kupitia nyaraka za ATCL na kuna taarifa kuwa leo w.anaenda kukagua namna ya wafanyakazi wa kitengo cha dharura ndani ya ndege wanavyoweza kuchukua hatua pindi tatizo linapotokea.CHANZO: Habari Leo
NI DHAHIRI KWAMBA UONGOZI WA SASA WA ATCL HAUWEZI KULIREJESHA SHIRIKA HILO KATIKA UHAI WAKE.KINACHOSHANGAZA NI KWANINI HADI LEO HAWAJAWAJIBISHWA.LAST WEEK ZILITOLEWA SIKU 7 ZA KUTOA MAELEZO.BINAFSI SIDHANI HATA KAMA KULIKUWA NA HAJA YA KUFANYA HIVYO KWA SABABU YEYOTE ATAKAYEPEWA NAFASI YA KUELEZEA UDHAIFU WAKE ATAJITETEA KWA VISINGIZIO LUKUKI.TATIZO HAPA SIO KWAMBA KUJITETEA NI KITU KIBAYA BALI UKWELI KUWA WAKATI SIKU 7 ZINATOLEWA (NA SI AJABU ZIKAONGEZWA) ATCL INAZIDI KUJIWEKA KATIKA HALI MBAYA YA KUREJEA TENA KATIKA OPERESHENI ZAKE.IKUMBUKWE KUWA CHANZO PEKEE CHA MAPATO KWA ATCL (NA SABABU YA KUANZISHWA KWAKE) NI BIASHARA YA USAFIRI WA ANGA.SIKU ZINAZIDI KUKATIKA TANGU SHIRIKA HILO LIPIGWE FULL STOP KUSAFIRISHA ABIRIA,NA HIYO INAMAANISHA KWAMBA ATCL INATENGENEZA HASARA KILA SIKU KWA VILE WAKATI HAKUNA MAPATO YANAYOINGIA,MATUMIZI LAZIMA YAFANYIKE KATIKA KILA SIKU YA UHAI WA SHIRIKA HILO.
HIVI HAKUNA WATU WENGINE WANAOWEZA KUTEULIWA KWENYE NYADHIFA ZA UENYEKITI WA BODI YA ATCL NA MKURUGENZI MKUU BADALA YA NYANG'ANYI NA MATTAKA,RESPECTIVELY?JE HAWA NDIO WATU PEKEE WANAOWEZA KUIOKOA ATCL?KUNA USHAHIDI WOWOTE WA WANANCHI HAWA KUWA NA UWEZO HUO?JE KUSUASUA KWA ATCL HAKUNA MAHUSIANO NA MAPUNGUFU KATIKA UWEZO WAO WA KUONGOZA SHIRIKA HILO?
NA BWANA MATAAKA AMEZUA TABIA MBAYA YA KUKANUSHA KILA TAARIFA ZISIZOPENDEZA ZINAZOELEKEZWA KWA ATCL.LAST TIME,ALIKANUSHA TAARIFA KWAMBA MAMLAKA YA MAWASILIANO IMEZUIA SHIRKA HILO KURUSHA NDEGE ZAKE,LAKINI BAADAYE AKALAMBA MATAPISHI YAKE NA KUKIRI HABARI HIYO.SASA TENA ANAKANUSHA HABARI YA KUKAMATWA KWA MAGARI HAYO WAKATI GAZETI HUSIKA LIMESHUHUDIA MAGARI HAYO YAKIWA KWENYE YADI YA BENKI YA STANBIC.AU MATTAKA ANATAKA KUTUAMINISHA KWAMBA PARKING YA MAGARI YA ATCL SASA NI HAPO STANBIC?
HIVI HII SERA YA KULINDANA ITAENDELEA MPAKA LINI?VIONGOZI WETU HAWAJISKII UCHUNGU WANAPOONA WENZETU WA KENYA AU ETHIOPIA,KWA MFANO,WANAVYOPASUA ANGA NA MASHIRIKA YAO YA NDEGE YENYE HADHI YA KIMATAIFA?KWA KWELI INATIA UCHUNGU NA KUUDHI HASA UNAPOONA VIONGOZI WA SHIRIKA LILILOKO A.C.U WAKISHINDWA KUONYESHA UCHUNGU KWA MATATIZO YALIYOPO HADI KUDIRIKI KUONYESHA KUWA "na kuna deni la BP...madeni ni jambo la kawaida".HIVI WAUNGWANA HAWA WANAWEZA KUTUELEZA WANAFANYA NINI HASA KUIKWAMUA ATCL?NA KAMA UTETEZI WAO PEKEE NI KUTOPEWA FEDHA NA SERIKALI,KWANINI BASI WASIACHIE NGAZI KUONYESHA KUTORIDHISHWA KWAO?KUNA MASLAHI WANAYOPATA VINGENEVYO WANGESHAJIUZULU ILI LAWAMA ZISIWAANGUKIE WAO PINDI ATCL IKIFA.
TUSIPOZIBA UFA TUTAJENGA UKUTA.
- 11:47
- Unknown
- BLOGGING
- 2 comments
I wouldn't consider myself as an expert in blogging,but hey,I've been around since 2006 and still kicking.I've seen blogs born and die,with some dying as fast as they were born.When going through some discussions in Jamii Forums I found a thread about January Makamba's blog.Putting aside the usual unpleasantries in a public forum,one notable point in the said discussion was how should bloggers communicate with their audiances.For instance,I'm Tanzanian,my national language is Kiswahili,and most of my blog posts are in that language too.But in so doing,am I not limiting my audiance?Talking of audiance,is it the people you share an expertise with,fellow countrymen and women,or anybody who has access to the internet?And,in blogging,should the top priority be on what I want my audiance expect from me or is it what I want them to hear from me?
Perhaps in finding answers to such questions,it's worth looking at how other bloggers from different countries blog.For instance,are most Chinese bloggers blog in Arabic?The answer is definitely no,though I do not have supporting statistics on that.May be the Chinese example doesn't do enough justice because of the number of Chinese speakers in the world.
Why do some bloggers prefer a foreign,or rather an international language,instead of their own?Is it because they are targetting a wider,global audiance?Is it because they master some languages other than their own?Or is it just a personal choice?
In one of the threads in Jamii forum,I found another discussion about a UK-based Tanzanian scholar,who was being criticised for using "poor" English in one of his articles in the web.While not passing my judgement on the said article or his critics,I was just wondering if anyone would be bothered if the article had been written in "poor Kiswahili".My assumption here is,a foreign langauge could easily become vulnerable to criticism.And this might be ONE of the reasons as to why many Tanzanian bloggers prefer using Kiswahili to English.However,there could also be a cultural factor.That is,Kiswahili is my national language,and it's part of my culture.So why should I not be proud of using it to communicate with my people?Cultural relativists might question,though,about those non-Kiswahili speakers?
Anyway,personally,I will continue using Kiswahili in most of my posts,especially those I deem of interests to my fellow Kiswahili speakers.However,English will also be used particularly when I give my analysis or opinion on news articles written in English.I am one of those who believe that although a personal blog should largely remain personal,in the sense of choices of words,language,pictures and even accepting or rejecting comments,it also attains a public status soon as it published because it could be read by anybody anywhere,and that necessitates being considerate TO and OF others.
Sunday, 28 December 2008
Dada yangu ambaye pia ni Mhariri Mkuu wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Bernadina (Dinna) Chahali akiwa kwenye msiba na kuaga mwili wa mfanyakazi mwenzie,Marehemu Henry Makange.Picha kwa hisani ya Mrisho Blog na Father Kidevu.
Saturday, 27 December 2008
Haya ni maongezi ya ki-utu uzima,kwahiyo under-18s mnaombwa kutosoma post hii.Well,just saying it bcoz I know ishu ya umri katika dunia ya sasa ni more theoretical than practical.Anyway,"kuvunja bikra" ni ndoto ya wanaume wengi,na japo ni suala lisilozungumzika hadharani,wengi wa wanaodai kuwa wameshawahi kupata "bahati" hiyo huwa si wakweli (wanaongopa) na wale ambao kweli walishaangukiwa na "kismati" hicho huwa hawaaminiwi wanapotoa "ushuhuda" wao,na wakati mwingine kutakiwa watoe uthibitisho!How could they?
Na pengine wapo akina dada ambao wangetamani kutopeteza bikra "kabla ya muda mwafaka" lakini mara nyingi tukio hilo (la kupoteza bikra) hutokea kwenye foolish age.Inadaiwa (japo sina uthibitisho katika dai hilo) kwamba kuna something very special kwa "ungo kuvunjwa" na mume usiku wa kwanza baada ya ndoa.Hata hivyo,jamaa yangu mmoja anayeelekea kuwa specialist wa kitu chochote kinachohusiana na jinsia ya kike anadai kuwa suala la kuvunjishwa ungo siku ya ndoa lilitengenezwa tu na walinzi wa maadili ili kuhakikisha amri ya sita haivunjwi (kwa wasiofahamu,amri ya sita ni USIZINI.Na kidini,kuzini ni tendo la ndoa nje ya ndoa).
Well,sasa kuna product ambayo "inarejesha" bikra.Nimeweka inverted commas kwa vile urejeshaji huo ni more technological than biological. Ni mithili ya ku-hack elimu-viumbe ya sehemu nyeti.
- 20:56
- Unknown
- KHALIL ISLAM, MALCOM-X
- No comments
Khalil Islam spent 22 years in prison for the murder of Malcolm X. Now a free man - who used to go by the name of Thomas 15X Johnson and was a ranking lieutenant at Elijah Muhammad’s Temple No. 7 on 116th Street and Lenox Avenue - Islam is ready to tell his story to the world...CONTINUE
POSTMORTEM NI MUHIMU HASA KWENYE VIFO VYENYE UTATA.LAKINI POSTMORTEM KWENYE MASUALA YA SIASA NI MBINU INAYOTUMIKA AIDHA KUKWEPA LAWAMA NA KUZIELEKEZA MAHALA KWINGINE AU KUPOOZA MAUMIVU YALIYOSABABISHWA NA MAPUNGUFU KWENYE UWAJIBIKAJI.KATIKA HABARI IFUATAYO,MBUNGE WA HANDENI,DKT ABDALLAH KIGODA, AMETOA POSTMORTEM REPORT YA MPANGO WA "MABILIONI YA JK",KWAMBA HAYAKUWANUFAISHA WATU WA VIJIJINI.PENGINE KABLA YA KUANGALIA VIJIJINI,SWALI KUBWA LILIPASWA KUWA "MABILIONI HAYO YAMEWANUFAISHA WATU WANGAPI REGARDLESS YA LOCATIONS ZAO-MIJINI AU VIJIJINI".LAKINI LA MSINGI ZAIDI,JE POSTMORTEM REPORT KAMA HIYO YA KIGODA INA UMUHIMU GANI KWA WANANCHI AMBAO HAWAKUNUFAIKA NA MPANGO HUO ULIOLENGA KUBORESHA MAISHA YA WATANZANIA?SOMA KWANZA HABARI YENYEWE KISHA TUENDELEE NA MJADALA:
Na Steven William, HandeniMBUNGE wa Handeni Dkt Abdallah Kigoda, amesema kuwa dhamira ya Rais Jakaya Kikwete kutenga fedha kwa ajili ya kukopeshwa wajasiriamali wadogo alikuwa na dhamira nzuri, lakini fedha hizo zilivamiwa na 'wajanja' wachache waliozikopa na wananchi hasa wa vijiji hazikuwafikia.Akizungumza katika mikutano ya hadhara kwenye vijiji vya kata ya Ndolwa wilayani hapa juzi kufuatia wananchi kumbana mbunge huyo kuhusu mikopo hiyo maarufu 'mabilioni ya Kikwete', mbunge huyo alisema kuwa fedha hizo zilitengwa na kupitia benki ambako wananchi wengi hasa wa vijijini hawana uelewa mpana wa kutumia benki zilizopo kukopa."Ndugu zangu wananchi dhamira ya Rais ilikuwa nzuri kwani alitenga fedha hizo kwa ajili ya kuwasaidia wenye mitajhi midogo wapandishe mauzo ya bidhaa zao lakini fedha zile zilipitia benki na nyie uwezo wa kuzitumia benki hamjui, hivyo wajanja wakajitokeza wakazichota," alisema Dkt Kigoda.Aliwapa mfano wa mkoa wa Kagera fedha hizo zilizpopelekwa mkoani humo, ni watu watano tu waliopata fedha hizo kutoka katika benki hizo akiwemo meneja wa benki hiyo hali iliyoleta tafsiri mbaya kwamba waliozichukua ni watu wa mjini waliokuwa na fursa nzuri na uzoefu wa kukopa benki.Hata hivyo, aliwatoa wasiwasi wananchi hao kwamba serikali itatoa tena fedha lakini walishauri kwamba pindi zikitolewa zishirikishe viongozi wa wilaya husika wachama na serikali ambao wamekuwa wakifahamu vikundi mbalimbali vya wajasiriamali katika maeneo husika hivyo fedha hizo zitafika kwa walengwa.Kufuatia kuingizwa tena fedha hizo kwenye mabenki hayo, mbunge huyo aliwataka wananchi wa wilaya ya handeni kuhakikisha wanajiunga na vikundi vya ujasiriamali ambavyo vitatambulika na serikali ili waweze kuomba na kupata mikopo.CHANZO:Mwananchi
HIVI DKT KIGODA ALIKUWA WAPI WAKATI FEDHA HIZO ZIKIELEKEZWA KUSIKOSTAHILI?NA WAKATI ANATOA TAKWIMU ZA KAGERA,KWANINI HATAJI IDADI YA WALIONUFAIKA AU KUATHIRIKA KATIKA JIMBO LAKE LA HANDENI?PIA ANAPASWA KUWAOMBA RADHI ALIOKUWA AKIWAHUTUBIA KWA KUSEMA "..na nyie uwezo wa kuzitumia benki hamjui".HIVI NI KWELI WANAKIJIJI WOTE ALIOKUWA AKIWAHUTUBIA,NA WENGINEO AMBAO HAWAKUPATA MABILIONI HAYO HAWANA UWEZO WA KUZITUMIA BENKI?JE YEYE KAMA KIONGOZI NA MWAKILISHI WAO AMEFANYA NINI KUWASAIDIA WAPIGA KURA WAKE KUWA NA UWEZO WA KUJUA NAMNA YA KUZITUMIA BENKI?BY THE WAY,NENO "KUZITUMIA" NI CONTRADICTORY KWANI LINAWEZA PIA KUMAANISHA KUZITUMIA BENKI KAMA ILIVYOKUWA KATIKA UFISADI WA EPA.ANYWAY,NADHANI ALIKUWA ANAMAANISHA WANAKIJIJI HAWAJUI KUZITUMIA HUDUMA ZA BENKI.IF SO,HAWAJUI KWA VILE HAKUNA BENKI,BENKI ZIPO LAKINI HAZITOI ELIMU YA NAMNA YA KUTUMIA HUDUMA ZAKE,WANAKIJIJI HAWATAKI KUELEKEZWA NAMNA YA KUTUMIA HUDUMA HIZO,AU...?
TATIZO KUBWA LINALOKWAMISHA MIPANGO MIZURI NI MIPANGO MIBOVU.WAINGEREZA WANA MSEMO POOR PLANNING PRODUCES POOR PERFORMANCE.UBOVU WA MPANGO WA MAMILIONI YA JK ULIKUWA KWENYE USIMAMIZI.NI DHAHIRI KWAMBA UKIPELEKA MAMILIONI,LET ALONE MABILIONI,PASIPO KUHAKIKISHA KUWA WAJANJA (ISOMEKE MAFISADI) HAWATABUNI MBINU ZA KUTAFUNA FEDHA HIZO,ITAKUWA NI MITHILI YA KUTWANGA MAJI KWENYE KINU.
MPANGO WA KUWAPATIA FEDHA WANANCHI WASIO NA UWEZO ILI ZIWASAIDIE KUJIKWAMUA KIUCHUMI ULIKUWA MZURI LAKINI ULIHITAJI UCHAMBUZI MAKINI KATIKA USIMAMIZI NA UTEKELEZAJI WAKE.KULIKUWA NA HAJA YA KUANGALIA POWER RELATIONS HUKO ZINAKOPELEKWA FEDHA HIZO,HUSUSAN MAHUSIANO KATI YA WASIMAMIZI NA WALENGWA.UDHAIFU KATIKA HILO NDIO UMEPELEKEA KESI KAMA HIYO YA KAGERA AMBAPO MENEJA WA BENKI NAE AKAJIINGIZA MIONGONI MWA WALENGWA JAPO SIDHANI KAMA ILIPASWA KUWA HIVYO.KILICHOPASWA KUFANYIKA KABLA YA KUPELEKA FEDHA HIZO NI KUTAMBUA WANAOZIHITAJI,KUFAHAMU MIPANGO YAO YA NAMNA WATAKAVYOTUMIA FEDHA HIZO AMBAZO KIMSINGI NI MIKOPO,KUTENGENEZA MAZINGIRA AMBAPO MAFISADI HAWATAZITAFUNA NA MWISHO,KUZIWASILISHA KATIKA WAKATI MWAFAKA.
PENGINE KABLA YA KUFIKIRIA KUTOA AWAMU NYINGINE YA MABILIONI NI MUHIMU KUFANYA TATHMINI YA MAFANIKIO NA FAILURES KATIKA AWAMU ZILIZOTANGULIA.SAMBAMBA NA HILO NI KUCHUKUA HATUA KALI KWA WOTE WALIOFUJA FEDHA HIZO.PIA NI MUHIMU KUFAHAMU FEDHA HIZO ZITAREJESHWA VIPI ILI BAADAYE WASIJE WAJANJA WAKAPORA ARDHI NA MALI NYINGINE ZA WALALAHOI KWA VISINGIZIO VYA KUDAI MAREJESHO YA FEDHA HIZO.
MWISHO,VIONGOZI KAMA DKT KIGODA WANAWEZA KUWA NA UMUHIMU ZAIDI KATIKA KULETA UFANISI WA MPANGO HUO WA MABILIONI YA JK SIO KWA KUTULETEA POSTMORTEM PINDI MAMBO YAKIENDA MRAMA BALI KWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KUHAKIKISHA MAFANIKIO YANAPATIKANA.HILO HALIHITAJI SEMINA ELEKEZI KWANI LIKO NDANI YA UWEZO WETU.KINACHOHITAJIKA NI DHAMIRA NA UWAJIBIKAJI.YES WE CAN!
Friday, 26 December 2008
Thursday, 25 December 2008
- 23:11
- Unknown
- CCM, JANET KAHAMA, RUSHWA, SOPHIA SIMBA
- No comments
CHAGUZI NDANI YA CCM HAZIISHIWI VIOJA.RUSHWA IMETAPAKAA MNO NDANI YA CHAMA HICHO KANA KWAMBA NI SEHEMU YA KATIBA YAKE.SIO MATUSI KUAMINI KWAMBA PENGINE INGEKUWA RAHISI ZAIDI KWA CCM KUAHIDI KUENDELEZA LIBENEKE LA RUSHWA KWENYE MANIFESTO YAKE YA 2005 KULIKO AHADI ZA MAISHA BORA,MAHAKAMA YA KADHI,NK MAMBO AMBAYO HADI SASA YAMEENDELEA KUWA AHADI ZISIZOTEKELEZEKA.NI WAZI,RUSHWA HUZAA VIONGOZI WABOVU,MAFISADI NA WABABAISHAJI.HABARI MBAYA NI KWAMBA HAKUNA DALILI ZA KUISHA KWA GONJWA HILO HATARI NDANI YA CHAMA TAWALA.TAASISI ZA UMMA ZA KUKABILIANA NA RUSHWA ZINAISHIA KUALIKWA TU KWENYE CHAGUZI "KUZUIA RUSHWA" NA VIONGOZI WAANDAMIZI WA CHAMA HICHO WAMEISHIA KUPIGA KELELE TU (SINA HAKIKA KAMA NI ZA DHATI) KUHUSU RUSHWA KWENYE CHAGUZI,LAKINI SOTE TUNAJUA KWAMBA KELELE ZA CHURA HAZIMZUII NG'OMBE KUNYWA MAJI.ENEWEI,HEBU CHEKI MKASA HUU HAPA CHINI KISHA SOMA HITIMISHO LANGU BAADA YA HABARI HII:
Zikiwa zimesalia siku 14 kufika siku ya uchaguzi wa viongozi wa ngazi ya taifa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mambo si shwari katika mchakato wa kumpata mwenyekiti wake.Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mjini Dodoma Januari 7, mwakani ambapo nafasi ya uenyekiti itagombewa na Janet Kahama, Sophia Simba na Joyce Masunga.Hali hiyo, ambayo inazidi kuipaka matope CCM, imedhihirika baada ya mgombea wa nafasi ya Janeth Kahama kuwasilisha rasmi malalamiko kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akimtuhumu mpinzani wake, Sophia Simba kwamba amewahonga wajumbe wote wa Mkutano Mkuu rushwa ya Sh. 100,000 ili wampe kura.Mbali na tuhuma za rushwa, Simba, ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), anatuhumiwa pia na Kahama kuwa yeye na wapambe wake wamekuwa wakiitumia Ikulu kuwaomba kura wajumbe wa Mkutano Mkuu.Kahama, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), amewasilisha malalamiko hayo kupitia barua yake yenye kumbukumbu Na. JBK/01/08 ya Desemba 20, mwaka huu, iliyopelekwa kwa Rais Kikwete, Ikulu, jijini Dar es Salaam.Nakala ya barua hiyo, ambayo Nipashe inayo, imepelekwa kwa Katibu Mkuu wa UWT Taifa na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.Makamba alipoulizwa na Nipashe juzi jioni kama amepokea nakala ya barua hiyo, alithibitisha kuipokea.Simba anadaiwa kutoa hongo hiyo kupitia kadi alizochapisha kwa lengo la kuwatakia heri ya Mwaka Mpya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UWT Taifa.Kadi hizo, ambazo zinadaiwa kusambazwa na Diwani wa Kata ya Ilala, Moshi Kondo, zina picha, jina na saini ya Waziri Simba, kalenda ya Mwaka Mpya wa 2009 na nembo ya CCM.Barua hiyo yenye kichwa cha habari kisemacho: `Yah: Malalamiko dhidi ya Mhe. Sophia Simba kugawa vipeperushi mikoani`, Kahama anamueleza Mwenyekiti Kikwete kama ifuatavyo:``Kwa heshima ya pekee, nakuomba uhusike na mada ya barua hii kama inavyosomeka hapo juu. Mheshimiwa Mwenyekiti, kama unavyofahamu, Jumuiya yetu ya UWT hivi sasa ipo katika mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa ngazi ya taifa unaotarajiwa kufanyika mapema mwakani.````Mimi nikiwa mmoja wa wagombea wa nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Taifa wa UWT, natambua kuwa wagombea wote tulizuiwa na vikao vya UWT Taifa kutoa vipeperushi vya aina yoyote kwa minajili ya kujinadi kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa UWT.````Lakini, ajabu ni kwamba, mgombea mwenzangu, Bi Sophia Simba amechapisha kalenda na kadi za `Heri ya Mwaka Mpya` zenye picha yake na nembo ya CCM na kuzisambaza kwa wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa UWT Taifa nchi nzima, ndani zikiwa na kitita cha Sh. 100,000 (kwa kila kadi).````Mheshimiwa Mwenyekiti, nalazimika kukuandikia waraka huu ili kukupa angalizo juu ya suala hilo hasa ikizingatiwa kuwa Mheshimiwa Sophia Simba ni Waziri katika ofisi yako mwenye dhamana ya Utawala Bora.````Hivyo hatua yake na nembo ya CCM, inakwenda kinyume na kanuni za uchaguzi za CCM, kipengele cha Miiko ya Kuzingatiwa wakati wa Shughuli za Uteuzi na Uchaguzi`, ibara ya 33 kifungu kidogo cha 14 kinachosema: `Ni mwiko kutumia makaratasi ya kampeni nje ya utaratibu wa chama au kutumia vishawishi vya aina yoyote ile kwa minajili ya kupata kura.````Je, hatua hii ya Mheshimiwa Simba kuchapisha nyaraka hizo zenye picha yake na nembo ya CCM na kuzitawanya nchi nzima, si uvunjaji wa makusudi wa kanuni hizo za uchaguzi za CCM tena kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa UWT?````Je hatuoni kwamba hatua yake hiyo ambayo haijakemewa mpaka sasa ni kielelezo kingine cha ubabe na matumizi mabaya ya madaraka yake kama Waziri tena mwenye dhamana ya Utawala Bora?Nasisitiza hili kwa sababu Mheshimiwa Simba na wapambe wake wamekuwa wakipita mikoani na kupotosha wapigakura kuwa yeye ndiye chaguo la Ikulu.````Mheshimiwa Mwenyekiti, nawasilisha kwako waraka huu wenye malalamiko haya ili uweze kujua nini kinaendelea na kuchukua hatua kwani kama kitaachwa, kinaweza kujenga matabaka ndani ya UWT na mpasuko usio wa lazima ndani ya chama chetu, hasa pale hisia za mgombea mmoja kuandaliwa mazingira ya ushindi dhidi ya wenzake zinapoanza kujengwa.````Naambatanisha moja ya vipeperushi hivyo vya Mheshimiwa Simba vilivyosambazwa mikoani kinyume na utaratibu nilioueleza hapo juu.``Makamba alipoulizwa na Nipashe juzi, licha ya kukiri kupokea nakala ya barua hiyo ya Kahama, alimtaka mwandishi kama ana swali lolote kuhusiana na suala hilo, akamuulize Rais Kikwete kwa vile ndiye aliyeandikiwa barua hiyo.``Mtafute Mwenyekiti wa CCM, yeye ndiye aliyeandikiwa barua, aliyeandikiwa ndiye anayejibu. Mimi nimepewa nakala, anayepewa nakala, anaarifiwa tu,`` alisema Makamba.Nipashe ilipowasiliana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu, Salvatory Rweyemamu, alisema kwa vile malalamiko ya Kahama yanahusiana na Chama, anayepaswa kujibu suala hilo ni Katibu Mkuu.Baada ya Makamba kuulizwa tena, alisema: ``Mimi sina cha kusema, sijaisoma (hiyo barua), sijajua maudhui.Nitakapoisoma na kujua maudhui, nitatoa maoni yangu.``Kahama alipoulizwa na Nipashe jana kama barua hiyo ndiye aliyeiandika, hakukiri wala kukanusha, badala yake alisema kwa sasa hawezi kuzungumza lolote kwa vile kipindi hiki ni cha sikukuu ya Krismasi, ambayo yeye kama Mkristo anapaswa kuitukuza.``Sina comments (maoni) kabisa kabisa, mpaka nionane na Katibu Mkuu. Pia mimi ni Mkristo na kipindi hiki ni cha Krismasi,`` alisema.Naye Diwani wa Kata ya Ilala, Moshi Kondo, alipoulizwa juzi, alikataa kuzungumzia suala hilo, badala yake alimtaka mwandishi akamuulize Simba.``Kwani Sophia Simba mimi ni nani kwake?`` alihoji Kondo, ambaye alipojibiwa na mwandishi kuwa ``Simba anadaiwa kuwa ni mtu wake wa karibu``, alisema: ``Nenda kamuulize Simba.``Tangu juzi hadi jana jioni Nipashe ilimtafuta Simba bila kumpata na baadaye kuelezwa na mmoja wa wanafamilia yake kuwa yuko safarini Malaysia.
CHANZO:Nipashe
WAKATI MAMA KAHAMA AMETUMIA HAKI YAKE YA MSINGI KAMA MGOMBEA NA MWANANCHAMA WA UWT/CCM KUWASILISHA MALALAMIKO YAKE KWA MWENYEKITI WA CCM TAIFA (JK),NADHANI ANGEWEZA PIA KUWASILISHA TUHUMA HIZO POLISI AU TAKUKURU.HIVI KUTOA RUSHWA SI NI KOSA LA JINAI?JE MAMA KAHAMA YUKO MORE CONCERNED NA RUSHWA HIYO KUATHIRI NAFASI YAKE YA KUCHAGULIWA KULIKO UKWELI KWAMBA MTUHUMIWA (SOPHIA SIMBA) SIO WAZIRI TU BALI NI WAZIRI MWENYE DHAMANA YA UTAWALA BORA (ISOMEKE MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA)?
- 21:22
- Unknown
- AFGHANISTAN, CIA, HEARTS AND MINDS, VIAGRA
- No comments
The Afghan chieftain looked older than his 60-odd years, and his bearded face bore the creases of a man burdened with duties as tribal patriarch and husband to four younger women. His visitor, a CIA officer, saw an opportunity, and reached into his bag for a small gift.Four blue pills. Viagra...CLICK HERE FOR FULL STORY
SOURCE:The Washington Post
Kiongozi wa mapinduzi hayo,Kapteni Moussa Dadis Kamara,aliyejitangaza kiongozi mpya wa Guinea baada ya kifo cha Rais Lansana Conte.Kwa habari zaidi,BONYEZA HAPA.
Subscribe to:
Posts (Atom)