Monday, 29 December 2008

Pichani,Mkurugenzi Mkuu wa ATCL David Mattaka akiteremka kutoka kwenye ndege iliyonunuliwa na shirika hilo mwezi Februari mwaka huu.Picha kwa hisani ya HAKI.

HEBU SOMA KWANZA HABARI IFUATAYO KISHA TUIJADILI PAMOJA.
Mali za ATCL zakamatwa
Benki ya Stanbic Tanzania Limited, Makao Makuu ya Kinondoni, Dar es Salaam, inayashikilia magari sita ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), baada ya kushindwa kulipa deni la Sh bilioni mbili iliyochukua kama mkopo. 

Fedha hizo zinazodaiwa kushindwa kulipwa kwa miezi miwili sasa zilikopwa na wafanyakazi wa kampuni kwa mikopo na kutokana na kushindwa kuwalipa mishahara watumishi wake, makato ya kila mwezi yameshindikana kukatwa. 

Taarifa zilizopatikana kutoka ATCL na katika benki hiyo jana zilithibitisha kushikiliwa kwa magari matano aina ya Toyota Land Cruiser VX, kuanzia Jumanne jioni wiki iliyopita na gari la sita limekamatwa likiwa mjini Moshi, Kilimanjaro na lilipelekwa katika benki hiyo jana na kufanya idadi ya magari hayo kuwa sita. 

Namba za magari hayo ambazo ‘HabariLeo’ jana ilizipata katika eneo la chini la maegesho yalikohifadhiwa magari hayo japo uongozi wa benki uliokuwapo haukuwa tayari kuzungumza kwa madai kuwa msemaji yupo likizo, ni SU 37079, SU 37081, SU 37082, SU 37086, SU 37083 na lililofikishwa jana ni SU 37084. 

Habari zaidi kutoka eneo la benki yalikohifadhiwa magari hayo zilieleza jana kuwa yataendelea kushikiliwa mpaka deni hilo lililipwe na uamuzi huo ulifikiwa baada ya hofu kuwa huenda kampuni hiyo ikafa na hivyo benki hiyo ikakosa kila kitu. 

Gazeti hili lilifika makao makuu ya Stanbic makutano ya barabara za Ali Hassan Mwinyi na Kinondoni, na mhudumu wa mapokezi alieleza kuwa wasemaji waliokuwapo hawakuwa tayari kulizungumzia, na mwenye dhamana ya kutoa taarifa hiyo ni Mkurugenzi Mkuu, Bashir Awale, yuko likizo. 

Hata hivyo, taarifa za ndani ya benki hiyo zililieleza gazeti hili kuwa deni wanaloidai ATCL ni Sh bilioni mbili kwa mwezi huu na kwamba uamuzi wa haraka ulichukuliwa baada ya akaunti ya kampuni hiyo kwa benki hiyo kuonyesha haina fedha za kulipa deni hilo wala haitarajii kuwa nazo kwa siku za karibuni. 

Chanzo chetu cha habari ndani ya ATCL kilieleza kuwa magari hayo yalikamatwa tangu wiki iliyopita isipokuwa la Mkurugenzi Mtendaji ATCL, David Mattaka. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya ATCL, Balozi Mustafa Nyang’anyi, alithibitisha jana kupata taarifa ya kukamatwa kwa magari hayo na ameitisha kikao cha dharura kitakachokaa leo makao makuu ya kampuni hiyo. 

Alisema pamoja na suala hilo, pia watajadili mambo mengine likiwamo la kurejeshewa leseni ya kurusha ndege waliyonyang’anywa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Desemba 8, mwaka huu. 

ATCL ilinyan’ganywa leseni hiyo baada ya kubainika kuwa na dosari za kiufundi zinazosababisha kutokuwa na viwango stahili vya kiusalama vya kuwaruhusu kurusha ndege; ukaguzi uliowataka warekebishe dosari hizo ulifanywa Oktoba mwaka jana na leseni hiyo iliisha kazi tangu Aprili mwaka huu, lakini walikuwa wakiongezewa muda mpaka iliposhindikana wakanyang’anywa leseni hiyo. 

“Hilo jambo na mimi nimepewa taarifa, lakini kusema ni kiasi gani au ni deni linahusu nini, mimi siyo menejimenti, mpigie Mattaka, ila ninachoweza kusema ni kwamba deni hilo si kitu cha ajabu maana tulikabidhiwa kampuni na deni la shilingi bilioni kumi na tisa,” alisema Balozi Nyang’anyi na kuongeza: “Ufafanuzi zaidi sina. 

Mnashangaa hilo, kuna na la BP, pia waliokuwa wanatusambazia chakula kwenye ndege… na mengine mengi, yote hayo tutayajadili kesho katika kikao cha dharura na menejimenti nilichokiitisha, tutazungumza hayo na mengine mengi.” 

Alisema katika kikao hicho pia watazungumzia mishahara ya wafanyakazi ambayo mpaka jana walikuwa hawajapata na pia kupanga namna ya kurudi tena katika uzalishaji mara watakaporejeshewa leseni ya kurusha ndege tena. 

Mattaka alipoulizwa jana kuhusu kushikiliwa kwa magari, alikanusha kwa kudai taarifa hizo si za kweli, lakini alikiri kuwapo kwa kikao cha Bodi na Menejimenti alichokiita kuwa ni kikao cha kawaida si cha dharura.Hizo habari umetoa wapi? Si kweli, nasema si kweli?” alisema huku mwandishi akiendelea kumhoji. 

“Kuhusu kikao ni kweli kipo, lakini si cha dharura, ni cha kawaida……naomba unitafute kesho baada ya kikao kuhusu hilo unalotaka kujua,” alisema Mattaka. Hivi sasa TCAA inaendelea kupitia nyaraka za ATCL na kuna taarifa kuwa leo w.anaenda kukagua namna ya wafanyakazi wa kitengo cha dharura ndani ya ndege wanavyoweza kuchukua hatua pindi tatizo linapotokea.

NI DHAHIRI KWAMBA UONGOZI WA SASA WA ATCL HAUWEZI KULIREJESHA SHIRIKA HILO KATIKA UHAI WAKE.KINACHOSHANGAZA NI KWANINI HADI LEO HAWAJAWAJIBISHWA.LAST WEEK ZILITOLEWA SIKU 7 ZA KUTOA MAELEZO.BINAFSI SIDHANI HATA KAMA KULIKUWA NA HAJA YA KUFANYA HIVYO KWA SABABU YEYOTE ATAKAYEPEWA NAFASI YA KUELEZEA UDHAIFU WAKE ATAJITETEA KWA VISINGIZIO LUKUKI.TATIZO HAPA SIO KWAMBA KUJITETEA NI KITU KIBAYA BALI UKWELI KUWA WAKATI SIKU 7 ZINATOLEWA (NA SI AJABU ZIKAONGEZWA) ATCL INAZIDI KUJIWEKA KATIKA HALI MBAYA YA KUREJEA TENA KATIKA OPERESHENI ZAKE.IKUMBUKWE KUWA CHANZO PEKEE CHA MAPATO KWA ATCL (NA SABABU YA KUANZISHWA KWAKE) NI BIASHARA YA USAFIRI WA ANGA.SIKU ZINAZIDI KUKATIKA TANGU SHIRIKA HILO LIPIGWE FULL STOP KUSAFIRISHA ABIRIA,NA HIYO INAMAANISHA KWAMBA ATCL INATENGENEZA HASARA KILA SIKU KWA VILE WAKATI HAKUNA MAPATO YANAYOINGIA,MATUMIZI LAZIMA YAFANYIKE KATIKA KILA SIKU YA UHAI WA SHIRIKA HILO.

HIVI HAKUNA WATU WENGINE WANAOWEZA KUTEULIWA KWENYE NYADHIFA ZA UENYEKITI WA BODI YA ATCL NA MKURUGENZI MKUU BADALA YA NYANG'ANYI NA MATTAKA,RESPECTIVELY?JE HAWA NDIO WATU PEKEE WANAOWEZA KUIOKOA ATCL?KUNA USHAHIDI WOWOTE WA WANANCHI HAWA KUWA NA UWEZO HUO?JE KUSUASUA KWA ATCL HAKUNA MAHUSIANO NA MAPUNGUFU KATIKA UWEZO WAO WA KUONGOZA SHIRIKA HILO?

NA BWANA MATAAKA AMEZUA TABIA MBAYA YA KUKANUSHA KILA TAARIFA ZISIZOPENDEZA ZINAZOELEKEZWA KWA ATCL.LAST TIME,ALIKANUSHA TAARIFA KWAMBA MAMLAKA YA MAWASILIANO IMEZUIA SHIRKA HILO KURUSHA NDEGE ZAKE,LAKINI BAADAYE AKALAMBA MATAPISHI YAKE NA KUKIRI HABARI HIYO.SASA TENA ANAKANUSHA HABARI YA KUKAMATWA KWA MAGARI HAYO WAKATI GAZETI HUSIKA LIMESHUHUDIA MAGARI HAYO YAKIWA KWENYE YADI YA BENKI YA STANBIC.AU MATTAKA ANATAKA KUTUAMINISHA KWAMBA PARKING YA MAGARI YA ATCL SASA NI HAPO STANBIC?

HIVI HII SERA YA KULINDANA ITAENDELEA MPAKA LINI?VIONGOZI WETU HAWAJISKII UCHUNGU WANAPOONA WENZETU WA KENYA AU ETHIOPIA,KWA MFANO,WANAVYOPASUA ANGA NA MASHIRIKA YAO YA NDEGE YENYE HADHI YA KIMATAIFA?KWA KWELI INATIA UCHUNGU NA KUUDHI HASA UNAPOONA VIONGOZI WA SHIRIKA LILILOKO A.C.U WAKISHINDWA KUONYESHA UCHUNGU KWA MATATIZO YALIYOPO HADI KUDIRIKI KUONYESHA KUWA "na kuna deni la BP...madeni ni jambo la kawaida".HIVI WAUNGWANA HAWA WANAWEZA KUTUELEZA WANAFANYA NINI HASA KUIKWAMUA ATCL?NA KAMA UTETEZI WAO PEKEE NI KUTOPEWA FEDHA NA SERIKALI,KWANINI BASI WASIACHIE NGAZI KUONYESHA KUTORIDHISHWA KWAO?KUNA MASLAHI WANAYOPATA VINGENEVYO WANGESHAJIUZULU ILI LAWAMA ZISIWAANGUKIE WAO PINDI ATCL IKIFA.

TUSIPOZIBA UFA TUTAJENGA UKUTA.


3 comments:

  1. NIMEPITA KUKUSALIMIA.
    \AHSANTE KWA KUNITEMBELEA NA KUTOA MAONI YAKO.
    USHAURI WAKO NITAUZINAGTIA.

    ReplyDelete
  2. NIMEPITA KUKUSALIMIA.
    \AHSANTE KWA KUNITEMBELEA NA KUTOA MAONI YAKO.
    USHAURI WAKO NITAUZINAGTIA.

    ReplyDelete
  3. Asante kwa kunitembelea.Karibu tena

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget