Kwenye uchambuzi makini,vitu kama laana,nuksi au bahati mbaya huwa havileti maana yoyote.Lakini katika maisha yetu kijamii tunafahamu kuwa jambo likiandamwa na kutofanikiwa linaweza kuhusishwa na laana au bahati mbaya.Na kama kuna sekta ambayo imekuwa ikiandamwa na matatizo kwa muda mrefu huko nyumbani basi ni usafiri.
Ukiangalia usafiri kuanzia kwenye cities hadi vijijini utabaini kwamba kadri unavyozidi kwenda chini (city ikiwa juu na kijiji chini) ndivyo matatizo yanavyozidi kuongezeka.Matatizo ya daladala jijini Dar ni "cha mtoto" ukilinganisha na namna ya kufika sehemu iitwayo Tanganyika Masagati (sijui kama ushawahi kuisikia).
Na hata hapo Dar,kero ya usafiri inazidi kuongezeka kadri unavyoelekea kwenye vitongoji vya jiji hilo.Ushawahi kufika Pemba Mnazi?Mara kwa mara tunasikia mipango mipya ya kuboresha usafiri,hasa jijini Dar.Tulisikia kuwa vipanya vingekuwa phased out lakini wajuzi wa mambo walishajua kuwa hilo ni changa la macho kwa vile wamiliki wengi wa vipanya hivyo ndio haohao wanaotuzuga kwenye media kuwa vipanya ni kero.Wanajuaje kero za vipanya ilhali wao wanazungushwa na ma-VX au Vogue yao yenye viyoyozi?
Na hata hapo Dar,kero ya usafiri inazidi kuongezeka kadri unavyoelekea kwenye vitongoji vya jiji hilo.Ushawahi kufika Pemba Mnazi?Mara kwa mara tunasikia mipango mipya ya kuboresha usafiri,hasa jijini Dar.Tulisikia kuwa vipanya vingekuwa phased out lakini wajuzi wa mambo walishajua kuwa hilo ni changa la macho kwa vile wamiliki wengi wa vipanya hivyo ndio haohao wanaotuzuga kwenye media kuwa vipanya ni kero.Wanajuaje kero za vipanya ilhali wao wanazungushwa na ma-VX au Vogue yao yenye viyoyozi?
Tukiachana na usafiri wa barabara,wa majini ndio wa roho mkononi zaidi.Na hapa sizungumzii meli au boti pekee.Angalia pale Kigamboni!Au kama unadhani pale ndio kiboko cha matatizo basi jaribu kwenda kivuko cha Mto Kilombero!Nilipokuwa huko hivi karibuni nilihabarishwa kwamba kivuko kipya kilichotarajiwa kutatua kero katika eneo hilo kiliishia kusomwa na maji.Kisa?Bila shaka fisadi flani kanunua kivuko mtumba.Kama kawaida,hakuna aliyewajibika hadi leo.
Hapo feri jijini Dar nako ni ngonjera kila siku.Mara sijui kuna daraja litajengwa,mara sijui kuna nini kitafanyika.Kama kawaida yetu,tunasubiri litokee janga flani kisha ndio mabwana mipango wetu waje na mipango mipya ya kujali maisha yetu.Vivuko vingi huko nyumbani ni sawa majeneza yanayoelea.Hakuna la muhimu tulilojifunza kutokana na janga la Mv Bukoba,na sijui hata kama policy makers wetu wanakumbuka janga hilo.
Usafiri wa reli ndio balaa.Zamani za kale,ukiwa ndani ya treni ya Tazara ungeweza kujiskia kama uko kwenye treni ya nchi zilizoendelea.Siku hizo tulikuwa tunasafiri na watalii kibao.Si unajua reli ya Tazara inakatiza katika hifadhi ya Selous,kwahiyo kwa wenzetu wanaotafuta vivutio safari hiyo ilikuwa ni kuua ndege wawili kwa jiwe moja:kufikishwa waendako na kupata uhondo wa wanyama mbugani.Hivi sasa Tazara iko dhoful khal,inakaribia kukata kauli.Mara ya mwisho niliposafiri kwa Tazara,jamaa mmoja Mzambia alinieleza bayana kuwa wanasubiri tu kifo cha shirika hilo.
Huko Reli ya Kati ndio habari mbaya zaidi.Hivi inaingia akilini kweli kwa mtu anayejiita mwekezaji kuwa anapewa fedha na serikali kulipa mishahara ya watumishi?Huyu ni m-babaishaji tu.Watu pekee wanaofahamu sababu za kwanini hadi leo TRL bado iko mikononi kwa wababaishaji hao wa kidosi ni Watanzania wenzetu wachache wanaoendela kuamini kwamba ipo siku TRL itasisima na kujiendesha yenyewe.Wajuzi wa mambo wanaiona TRL kama kipofu anayetafuta sindano kwenye chumba chenye kiza totoro,huku sindano hiyo ikiwa haipo humo!
Kitu pekee kitachowakimbiza Wahindi hao ni janga.Kwanza tukubaliane kwamba kama wangekuwa hawapati faida katika huduma yao mbovu wasingeendelea kuwepo hadi leo.Si unawajua Wahindi linapokuja suala la faida?Yes,janga ndio itawakimbiza wadosi hao.Mungu aepushe janga hilo lakini likitokea la kutokea na kisha tukaishia kumlaumu Mungu,atatuadhibu vikali.Hawa wababaishaji hawajafanya matengenezo ya reli,wanasafirisha abiria kwenye mabehewa ambayo hata ng'ombe hawastahili kupanda,na ratiba zao ni za bahati nasibu.Yayumkinika kuhitimisha kuwa mazingira hayo ni sawa na a catastophy in the making.And once that happens,God forbid,hawa jamaa wataingia mitini just like wawekezaji wababsiahji wengine wanavyotukimbia baada ya kuukamua uchumi wetu.Na huwezi kuwalaumu kwani hata mwenye nyumba ambaye anaacha mboga yake jikoni pasipo kuhofia nyau,hawezi kuwalaumu paka wakikwiba mboga hiyo kukidhi njaa zao!
Hatuwezi kuuzungumzia usafiri wa anga pasipo kutaja AIR TANZANIA.Uongozi mmoja umeupisha mwingine one times too much,nembo zimebadilishwa mara lukuki,mgogoro mmoja umeupisha mwingine,lawama za wasafiri ndio usiseme!Hivi Waethiopia ni wachawi kwa namna walivyoweza kuifanya Ethiopian Airlines kuwa moja ya mashirika ya ndege ya mfano barani Afrika?Vipi kuhusu watani zetu na Kenyan Airways yao?Sisi tunashindwa nini?Hivi kuna ugumu gani wa kukodi ndege,kutoa huduma ya kuridhisha,kutumia itakayopatikana kununua ndege zaidi na kisha kutanua safari katika maeneo mbalimbali duniani?
Tatizo kubwa la Air Tanzania,or whatever its current name is,ni ufisadi.Na chanzo cha ufisadi huo ni hao wanaofanya teuzi pasipo kuzingatia rekodi.Hivi hawa viongozi wa sasa wa ATC wana sifa stahili za kulitoa shirika ICU na kulirejesha angani?Majuzi David Mattaka aliruka kimanga alipoulizwa iwapo ndege za shirika hilo zimepigwa stop kutoa huduma (kutoa non-existent huduma?) kabla ya kukiri muda mfupi baadaye kwamba habari hiyo ni ya kweli.Hivi background ya mtu huyu inaleta matumaini yoyote ya kufufuka kwa ATC?Na hapo sizungumzii maisha yake binafsi (hapa sio mahala pake).
Sababu kubwa ya nuksi,mikosi na bahati mbaya zinazoiandama sekta ya usafiri huko nyumbani ni uksefu wa uzalendo.Hilo linaanzia kwa hao wanaofanya uteuzi wa kuongoza taasisi zinazotoa huduma za usafiri wa angani,majini,barabara na reli.Pia uteuzi usiozingatia rekodi kwenye mamlaka zinazosimamia sekta hiyo ni tatizo jingine la msingi.Takriban maeneo yote yaliyoguswa katika uchambuzi huu yana Waziri,Naibu Waziri,Katibu Mkuu,Naibu Katibu Mkuu,Mkurugenzi Wizarani na Mkurugenzi shirikani,mameneja lukuki,Wenyeviti na wajumbe wa bodi ambao vikao vyao ni about posho tu na sio maendeleo ya shirika husika,na mlolongo mwingine wa watendaji.Sasa hapo inahitajika domino effect top to down.Waziri akiweka mbele uzalendo na uwajibikaji hao wote chini yake watatimiza majukumu yao.Lini tutapata Waziri ambaye ataapa kuwa lazima AIR TANZANIA itarudi hewani,TRC itafufuka kutoka katika wafu,TAZARA itapata uhai mpya,vivuko vinakuwa na maana ya vivuko,na hatua nyingine nyingi.Na isiishie kuapa tu kwani waheshimiwa wneig tu huapa lakini huishia kufisadi nchi na viapo vyao.
Uzalendo ni kuweka maslahi ya nchi mbele badala ya maslahi binafsi,Uzalendo ni kuchagua watu wenye sifa na uwezo na sio ku-recycle watendaji wenye sifa zisizostahili personally na professionally.It can be done,if wenzetu wakiamua ku-play their part....au just kusema YES WE CAN!
0 comments:
Post a Comment