SALAAM ZA MWAKA MPYA
Uongozi na wafanyakazi wa
MwanaHALISI,
hata ndani ya kifungo cha
siku 90 cha gazeti hili,
tunayo furaha kukutakia
heri katika sherehe za msimu huu
zinazoambatana na
kuaga mwaka huu na kukaribisha
Mwaka Mpya.
Tumetambua na kuthamini
upendo na ujasiri wako katika kutetea
uhuru wa mawazo na uhuru wa
habari; na tunaahidi
kuendelea kutenda kwa mujibu wa
uhuru, haki na wajibu
mara baada ya kurejea ulingoni.
Heri ya Mwaka Mpya – 2009
Saed Kubenea
Mkurugenzi Mtendaji
Hali Halisi Publishers
0 comments:
Post a Comment