Saturday, 13 December 2008

Watanzania wengi wanapenda habari.Na siku hizi vyombo vya habari viko vya kumwaga.Hata hivyo,upatikanaji wa habari za uhakika bado ni tatizo.Kwanza,wanahabari wengi wa huko nyumbani wanapendelea zaidi kuripoti habari badala ya kuleta habari iliyochunguzwa.Leo hii ukitoka ughaibuni na vizawadi viwili vitatu kisha ukaitisha press conference na kudai unataka kuanzisha mradi flani,kesho yake habari hizo zitaripotiwa kama ulivyotaka.Na kama hiyo press conference itaambatana na makulaji na vinywaji basi si ajabu habari hiyo ikawa ukurasa wa kwanza.Of course,kuna exceptions kwenye magazeti kama This Day,Kulikoni,Raia Mwema,Mwanahalisi na mengine machache.

Tatizo la pili katika upitakanaji wa habari liko katika mafungu mawili.Kwanza,japo magazeti ni mengi,wenye uwezo wa kununua bado si wengi sana.Bei ya wastani ya gazeti ni shilingi 400.Ukizingatia ugumu wa maisha,ni vigumu kutoa kiasi hicho kwa gazeti ambalo ukishasoma linakuwa halina matumizi mengine ya muhimu.Pili,upatikanaji wa habari kwa njia ya runinga na redio bado ni mgumu katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.Nilipokuwa Ifakara hivi karibuni,nilibaini kwamba ili uweze kukamata matangazo ya vituo vyote vya televisheni ni lazima uwe na "ungo".Sasa unaweza ku-imagine ni watu wangapi wenye uwezo wa kumudu gharama za kununua na ku-install satellite dish.

Pamoja na "chengachenga" za hapa na pale,redio imeendelea kuwa tegemeo la wengi hasa vijijini.Na ukipta hapa na pale utakuta wazee wetu nyakati za jioni wakisikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC au Deutsche Welle.Na kupitia matangazo hayo ndipo mzee wangu mmoja niliyeongea nae kwa simu jioni ya leo alipata habari kwamba kuna wawekezaji kadhaa "walioingizwa mkenge" na tapeli mmoja,Bernard Madoff,katika kile kinachofahamika kama Ponzi Scheme.Mzee huyo aliniuliza inakuwaje "wazungu" wenye uelewa mkubwa wa mambo waliweza kuhadaika na kushiriki "upatu" huo?Sikua na jibu kwa vile habari yenyewe ilikuwa bado ngeni kwangu.Kama mwenzangu nawe hujaipata,BONYEZA HAPA kuisoma kwa undani.

Related Posts:

  • UFISADI WA PESA,KISHA WA NDUMBA (MAKALA NDANI YA GAZETI LA RAIA MWEMA) Makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema inaanza kwa kuwashutumu watangazaji wa radio na runinga za Bongo ambao wanafanya mzaha kwenye shughuli muhimu.Makala inawalenga watangaza taarifa za habari ambao … Read More
  • SOPHIA: A DOWN-TO-EARTH CELEBRITYMore than a decade ago, I happened to share a flat with a Tanzanian High Court judge’s son. Knowing how publicity-shy he is, I better keep his name to myself. Call me 'old-fashioned' who’s never had  opportunity to mingl… Read More
  • SERIKALI YAJIKUTA KATIKA MTEGO WA KULIADHIBU GAZETI LAKENa Daniel Mjema, DodomaSERIKALI imekiri kuwa gazeti lake la Habari Leo liliandika habari ya uchochezi na kuliahidi Bunge kuwa italichukulia hatua zinazostahili gazeti hilo.Hatua hiyo ya serikali inafuatia agizo la Bunge kwamb… Read More
  • HABARI MOJA,MITIZAMO TOFAUTIYAH,WANASEMA NI SUALA LA MTIZAMO: KUSEMA GLASI IKO HALF EMPTY AU HALF FULL.HABARI MBILI ZIFUATAZO ZINADHIHIRISHA MANTIKI YA MSEMO HUO.Na Boniface MeenaUMAARUFU wa Rais Jakaya Kikwete unaonyesha kuendelea kuporomoka, kwa mujib… Read More
  • "WAZUNGU" WALIZWA NA UPATU (PONZI SCHEME)Watanzania wengi wanapenda habari.Na siku hizi vyombo vya habari viko vya kumwaga.Hata hivyo,upatikanaji wa habari za uhakika bado ni tatizo.Kwanza,wanahabari wengi wa huko nyumbani wanapendelea zaidi kuripoti habari badala y… Read More

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget