Tuesday, 30 December 2008

HATIMAYE TUMEFIKA MWISHO WA MWAKA 2008.SIJUI MWENZANGU KWAKO MWAKA HUU TUNAOUMALIZA LEO ULIKUWAJE LAKINI BINAFSI 2008 IMENIACHA NA PENGO AMBALO HALITOZIBIKA HADI KIFO CHANGU.TAREHE 29 MEI NILIMPOTEZA MAMA YANGU MZAZI,MAREHEMU ADELINA MAPANGO.KIFO HICHO KILIHITIMISHA SAFARI YAKE NGUMU NA YA MAUMIVU ILIYOANZA MWISHONI MWA MWEZI FEBRUARI AMBAPO ALIANGUKA NA KUPOTEZA FAHAMU.ILINILAZIMU KWENDA TANZANIA MWEZI MACHI NIKIWA NA MATUMAINI KWAMBA HUENDA HALI YAKE INGEBADILIKA LAKINI KWA BAHATI MBAYA HADI ANAFARIKI SIKUPATA BAHATI YA KUONGEA NAE HATA NENO MOJA.MARADHI NA KIFO CHA MAMA VILIPELEKEA KUSHINDWA KWANGU KUHITIMU MASOMO YANGU MWEZI NOVEMBA KUTOKANA NA KUTUMIA TAKRIBAN MIEZI MITANO HUKO NYUMBANI NIKIUGUZA NA KUSHUGHULIKIA TARATIBU ZA MAZISHI NA AROBANI.BWANA ALITOA NA BWANA ALITWAA,LAKINI PENGO ALILOACHA MAMA HALITOZIBIKA MILELE,NA TUKIO HILO NDILO LILILOKUWA KUBWA ZAIDI KWANGU KWA MWAKA HUU TUNAOUMALIZA LEO.

MATUKIO MENGINE NILIYOFANIKIWA KUYAWEKA BLOGUNI AU KUYAFUATILIA KWA KARIBU KUANZIA MWEZI JANUARI NI KAMA IFUATAVYO:
MIONGONI MWA MATUKIO MAKUBWA YA MWEZI JANUARI ILIKUWA NI PAMOJA NA VURUGU ZILIZOJITOKEZA BAADA YA UCHAGUZI MKUU NCHINI KWENYE AMBAPO WAFUASI WA MGOMBEA RAILA ODINGA WALIDAI WAMEPORWA USHINDI NA MWAI KIBAKI.TUKIO JINGINE KUBWA LILIKUWA KIFO CHA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA PAKISTAN BENAZIR BHUTTO.MAFURIKO NCHINI MSUMBIJI YAUA WATU KADHAA NA KUACHA MAELFU WAKIWA HAWANA MAKAZI.GEORGE W. BUSH ASOMA STATE OF THE UNION ADDRESS KWA MARA YAKE YA MWISHO (HATOKUWA MADARAKANI 2009).PIA SERIKALI ILIYOKUWA CHINI YA WAZIRI MKUU WA ITALIA,ROMANO PRODI,YAVUNJIKA.KADHALIKA,BALOZI WA TANZANIA HUKO AFRIKA KUSINI,EMMANUEL MWAMBULUKUTU APIGWA.SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU ISHU YA EPA.TUKIO JINGINE MUHIMU LILIKUWA KUCHAGULIWA KWA JK KUWA MWENYEKITI WA UMOJA WA AFRIKA (AU).

MWEZI FEBRUARI ULISHUHUDIA UJIO WA RAIS BUSH NCHINI TANZANIA NA KUNG'OKA KWA EDWARD LOWASSA KWENYE UWAZIRI MKUU KUFATIA TUHUMA ZA KAMPUNI YA KITAPELI YA RICHMOND.PIA KATIKA MWEZI HUO KULIKUWA NA KIOJA CHA SPIKA SAMUEL SITTA KUMTAKA NAIBU WAKE ANNE MAKINDA "ASIKURUPUKE" KUENDESHA MJADALA WA ISHU YA RICHMOND HADI HAPO SPIKA ATAPOREJEA KUTOKA SAFARINI UGHAIBUNI.BAADAYE SPIKA ALIAHIRISHA SAFARI HIYO,NA WOTE TUNAJUA KILICHOJIRI BAADA YA MJADALA HUO WA KIHISTORIA.KUJIUZULU KWA LOWASSA KULIMPELEKEA JK KUVUNJA KABINETI YAKE NA KISHA KUMTEUA BW MIZENGO PINDA KUWA WAZIRI MKUU HUKU SURA NYINGI ZA BARAZA LA MAWAZIRI WA ZAMANI ZIKIREJEA.KATI YA WALIOLALAMIKIWA SANA KUTEULIWA KWENYE BARAZA JIPYA NI PAMOJA NA "MZEE WA VIJISENTI" ANDREW CHENGE.PIA KATIKA MWEZI HUO,RAIS MWANAMAPINDUZI WA CUBA,FIDEL CASTRO ALING'ATUKA MADARAKANI.TUKIO JINGINE LILILOVUTA HISIA ZA JAMII YA WATANZANIA MTANDAONI NI KUFUNGIWA KWA JAMBO FORUMS NA WAHUSIKA WAKE WAWILI KUKAMATWA.HATA HIVYO MTANDAO HUO MAHIRI ULIREJEA HEWANI BAADA YA SIKU CHACHE UKIWA NA JINA JIPYA LA JAMII FORUMS.

MWEZI MACHI ULIANZA KWA KUTAWALIWA NA HABARI ZA KINYANG'ANYIRO CHA UCHAGUZI NCHINI MAREKANI AMBAPO MGOMBEA WA CHAMA CHA REPUBLICAN,JOHN MCCAIN,ALI-WIN NOMINATION YA CHAMA CHAKE.PIA SUPER-TUESDAY NDANI YA CHAMA CHA DEMOCRAT ILIZIDISHA MPAMBANO KATI YA HILLARY CLINTON NA BARACK OBAMA.MACHI PIA ILISHUHUDIA KUSAMBARATIKA KWA SERIKALI YA SERBIA.VILEVILE,WAKRISTO SEHEMU MBALIMBALI DUNIANI WALIADHIMISHA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA BWANA YESU KRISTO KATIKA SIKUKUU YA PASAKA.WIKI YA MWISHO YA MACHI ILISHUHUDIA REPORTING YA BLOG HII KUTOKA TANZANIA BAADA YA MIE MTUMISHI WAKO KUELEKEA HUKO KUMUUGUZA MZAZI WANGU.

REPORTING LIVE AND DIRECT KUTOKA BONGO,BLOG ILIANZA MWEZI APRILI KWA PICHA KADHAA ZA KUTOKA NYUMBANI.HII ILIKUWA TRANSITION MUHIMU KWA BLOG YENU KWANI NDIO LILIKUWA JARIBIO LA KWANZA LA KUCHANGANYA NEWS ANALYSIS NA PHOTOBLOGGING.NIKIRI KWAMBA BADO NIKO NYUMA SANA IN THE LATTER.BLOG ILIWALETEA PICHA ZINAZOONYESHA HALI HALISI ILIVYO KATIKA HOSPITALI YA MUHIMBILI.PIA KULIKUWA NA MAKALA KUHUSU HUDUMA MBOVU KWENYE HOSPITALI YA REGENCY.KADHALIKA,KULIKUWA NA "BREAKING NEWS YA KIMTINDO" YA MAFURIKO HUKO IFAKARA PAMOJA NA PICHA ZA ADHA YA USAFIRI WILAYANI KILOMBERO.VILEVILE,BLOG ILIJITAHIDI KUUFAHAMISHA UMMA KUHUSU MAPUNGUFU MBALIMBALI KWENYE HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA TAASISI MBALIMBALI ZA HUKO NYUMBANI.MIONGONI MWA HABARI KUBWA ZA MWEZI HUU ILIKUWA NI PAMOJA NA KUJIUZULU KWA MZEE WA VIJISENTI ANDREW CHENGE.

NI VIGUMU KUFANYA EFFECTIVE BLOGGING WAKATI UNAUGUZA MTU MUHIMU KATIKA MAISHA YAKO KAMA MZAZI.KASI YA KU-BLOG NA KU-UPDATE BLOG ILIPUNGUA MWEZI MEI BAADA YA HALI YA MAMA KUZIDI KUDHOOFIKA.KIPINDI HIKI KILINIPA FURSA NZURI YA KUTAMBUA SOME HIDDEN SOCIAL BENEFITS ZA BLOGGING KWANI NILIPATA SALAMU NYINGI ZA SAPOTI KUTOKA KUTOKA KWA WATU NISIOWAFAHAMU LAKINI TULIOJUANA KUPITIA SEHEMU HII AMBAO WALIKUWA WAKINIPA MOYO KATIKA KIPINDI HICHO KIGUMU.PIA MWEZI MEI ULISHUHUDIA SHIRIKA LA NDEGE LA ATC LIKIINGIZA KWA MBWEMBWE DEGE MTUMBA LA AIRBUS A320.WAJUZI WA MAMBO WALIHOJI HATUA HIYO HUKU WAKISISITIZA KWAMBA HUO NI MWENDELEZO WA UFISADI.KADHALIKA,MZEE WA VIJISENTI ANDREW CHENGE ALIZUSHIWA KIFO KABLA YA HABARI HIYO KUKANUSHWA NA FAMILIA YAKE.PIA TAIFA STARS ILIFANYA KWELI KWA KUIBAMIZA THE CRANES 2-0.PIA RAPA MAARUFU 50 CENT ALITUA DAR NA KUFANYA ONYESHO MOJA.ILIFAHAMIKA PIA KWAMBA ALIYEKUWA GAVANA WA BoT DAUDI BALLALI AMEFARIKI HUKO MAREKANI.HABARI HIYO ILIGUBIKWA NA USIRI MKUBWA KIASI CHA BAADHI YA WATU KUHISI NI CHANGA LA MACHO.TAREHE 29 YA MWEZI HUU,SAA 4.30 USIKU (TANZANIAN TIME),MAMA YANGU MPENDWA ALIAGA DUNIA.THIS WAS THE DARKEST DAY OF MY LIFE.
JUNI ILIANZA KWA KUMZIKA MAMA MNAMO TAREHE 2.SINTAISAHAU SIKU HII MAISHANI MWANGU ASILANI.

MATUKIO MENGINE KATIKA MWEZI HUO NI PAMOJA MKUTANO WA LEON SULLIVAN ULIOFANYIKA HUKO ARUSHA HUKU BAADHI YA WAFANYABIASHARA WA NDANI WAKILAUMU KWA KUTELEKEZWA NA WAANDAAJI.TAIFA STARS ILIBORONGA HUKO CAPE VERDE BAADA YA KUTANDIKWA BAO 1-0.PIA MASHABIKI WA SOKA DUNIANI WALIELEKEZA MACHO NA MASIKIO YAO KWENYE KINYANG'ANYIRO CHA MICHUANO YA EURO 2008 AMBAPO HISPANIA ILIIBUKA KIDEDEA.BAJETI YA SERIKALI YASOMWA,MAUMIVU KWA WALALAHOI YAENDELEA.TIMU YA TAIFA YA CAMEROON YATOKA SULUHU NA TAIFA STARS JIJINI DAR HUKU MASTAA KAMA SAMUEL ETOO WAKIWA KIVUTIO.MABONDIA 6 WA TANZANIA WATIWA MBARONI HUKO MAURITIUS KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA UNGA.JENGO MOJA LA GHOROFA LILILOPO JUNCTION YA ZANAKI/KISUTU STR LAPOROMOKA .TAIFA STARS YANYUKWA 2-1 HUKO CAMEROON.OBAMA ASHINDA KUWA MGOMBEA WA CHAMA CHA DEMOCRAT.MAKALA YANGU KWENYE GAZETI LA RAIA MWEMA LA TAREHE 26 IKITABIRI KIFO CHA CCM (KAMA KILIVYOTABIRIWA NA BABA WA TAIFA) YAZUA SONGOMBINGO NA HATIMAYE KUFIKIA UAMUZI WA KUCHUKUA SABBATICAL LEAVE YA UANDISHI WA MAKALA.

MWEZI JULAI UNAANZA KWA PILIKAPILIKA ZA SABA SABA LAKINI UCHUMI MBOVU JAPO VITU KIBWENA KWENYE MABANDA HUKO KILWA ROAD.RAIS WA SHRIKISHO LA NDONDI TANZANIA,ALHAJI SHABAN MWINTANGA ATIWA MBARONI KUHUSIANA NA SAKATA LA MABONDIA WALIKAMATWA NA UNGA HUKO MAURITIUS.MSANII WA BONGOFLEVA T.I.D ATUPWA JELA MWAKA MMOJA.YANGA WAFANYA KITKO CHA KIHISTORIA:WAINGIA MITINI SIKU YA MPAMBANO KATI YAO NA SIMBA.MBUNGE MACHACHARI NA MAKAMU MWENYEKITI WA CHADEMA,CHACHA WANGWE,AFARIKI KWA AJALI YA GARI HUKO DODOMA.MAHAKAMA YA KIMATAIFA (ICC) YATOA WARRANT YA KUKAMATWA KWA RAIS WA SUDAN,OMAR AL-BASHIR,KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA MAUAJI YA HALAIKI HUKO DARFUR.MHALIFU WA KIVITA,RADOVAN KARADZIC,AKAMATWA KUHUSIANA NA MAUAJI YA HALAIKI HUKO SERBIA.

AGOSTI,MREMBO NASREEM ATWAA TAJI LA MISS TANZANIA 2008.AJALI MBAYA YA BASI YAPOTEZA MAISHA YA WATU 10 NA WENGINE 30 KUJERUHIWA HUKO MBEYA.MWANAMUZIKI SHAGGY ATUA DAR NA KUFANYA ONYESHO.MAANDAMANO NA VURUGU ZATANDA NCHINI VENEZUELA,NA HUKO GEORGIA MAJESHI YA RUSSIA YAENDELEZA UBABE WAKE.HABARI NYINGINE KATIKA MWEZI HUU ILIKUWA NI KUJIUZULU KWA RAIS WA PAKISTAN PERVEZ MUSHARRAF.TUKIO JINGINE KUBWA LILIKUWA NI MICHEZO YA OLIMPIKI HUKO CHINA,NA KWA NYUMBANI WATANZANIA WALITEGESHA MASIKIO YAO HUKO DODOMA WAKATI JK ALIPOHUTUBIA BUNGE.WENGI WALITEGEMEA KUSIKIA HATIMA YA ISHU ZA EPA,RICHMOND NA UFISADI MWINGINE LAKINI HAYO YALIGUSIWA JUU JUU TU.AGOSTI PIA ILISHUHUDIA RAIS WA VISIWA VYA KOMORO,AHMED ABDALLAH MOHAMMED,AKIHUTUBIA BUNGE LA MUUNGANO DODOMA.PM MIZENGO PINDA ASOMA TAARIFA KUHUSU ISHU YA RICHMOND.KAMA KAWAIDA,NI TAARIFA TU HAKUNA ALIYEWAJIBISHWA SO FAR.JK AMTEMBELEA BUSH HUKO WHITE HOUSE NA MWEZI WA TOBA WAANZA.RAIS MWANAWASA WA ZAMBIA AFARIKI DUNIA.

SEPTEMBA YAANZA KWA HABARI ZA VIMBUNGA IKE NA GUSTAV.ASIF ALI ZARDARI,MJANE WA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA PAKISTAN BENAZIR BHUTTO,ACHAGULIWA KUMRITHI JENERALI MUSHARAF.TETESI ZAZUKA KUHUSU AFYA YA KIONGOZI WA KORA YA KASKAZINI,KIM JUNG IL,IKIDAIWA KWAMBA AMEKUFA LAKINI NCHI HIYO YAKANUSHA HABARI HIZO.JONGWE MUGABE NA MORGAN TSHANGIRAI WAFIKIA MAKUBALIANO YA UONGOZI HUKO ZIMBABWE.MLIPUKO WA BOMU KATIKA HOTELI YA MARRIOT HUKO ISLAMABAD PAKISTAN WAUA NA KUJERUHI WATU KADHAA.KESI YA ZOMBE YAENDELEA KUUNGURUMA HUKO NYUMBANI.JACOB ZUMA NAE ATUA DAR.JAPAN YAPATA WAZIRI MKUU MPYA,TARO ASO,AMBAYE NI MKATOLIKI WA KWANZA KUSHIKA WADHIFA HUO NCHINI HUMO.UCHAGUZI WAFANYIKA NCHINI BELARUS LAKINI WAANGALIZI WA KIMATAIFA WADAI HAUKUWA FREE AND FAIR.PIA SAKATA LA MAZIWA YENYE WALAKINI HUKO CHINA YAPAMBA MOTO KWENYE ANGA ZA HABARI.MSHIRIKI WA TANZANIA KWENYE BIG BROTHER AFRICA 3 ATOLEWA MASHINDANONI,CHA AJABU AREJEA BONGO KAMA SHUJAA NA KUANDALIWA PATI YA PONGEZI!RAIS WA AFRIKA KUSINI,THABO MBEKI AJIUZULU.WAFANYAKAZI WA BENKI YA NMB WAGOMA NA KUSABABISHA USUMBUFU MKUBWA KWA WATEJA.SHEREHE ZA IDD EL FITR ZAKUMBWA NA BALAA BAADA YA VIFO VYA WAOTO 20 MJINI TABORA.USTAADH MMOJA MWENYE MSIMAMO MKALI HUKO SAUDI ARABIA ASOMA FATWA DHIDI YA MICKEY MOUSE KWA MADAI KUWA KIKARAGOSI HICHO NI WAKALA WA SHETANI!

ANGA ZA HABARI ZA KIMATAIFA MWEZI OKTOBA ZILIANZISHWA NA TAARIFA ZA WATEKA MELI (PIRATES) HUKO SOMALIA AMBAPO SAFARI HII WATEKA MELI KUTOKA UKRAINE ILYOKUWA NA VIFARU 33.UCHUMI WA DUNIA WAZIDI KWENDA HARIJOJO NA WASIWASI WAJITOKEZA KUHUSU UWEZEKANO KUFILISIKA KWA NCHI YA ICELAND.NENO ECONOMIC BAILOUT LAWA KAMA SALA KWENYE VYOMBO VYA HABARI VYA KIMAIFA HASA BAADA YA RAIS BUSH KUIDHINISHA BAILOUT YA DOLARI BILIONI 700 KUOKOA UCHUMI WA MAREKANI,NA NCHI KADHAA KUFUATA MKONDO.CHADEMA WASHINDA UCHAGUZI MDOGO WA TARIME ULIOAMBATANA NA KILA AINA YA VITUKO.OBAMA AENDELEA KUTESA KWENYE OPINION POLLS ZA UCHAGUZI MKUU WA MAREKANI.JK AZURU MBEYA,ZIARA YAGUBIKWA NA HABARI ZA MSAFARA WAKE KUTUPIWA MAWE.PIA JK ATAWAZWA KUWA "CHIFU MWANGUPILI" WA WANYAKYUSA.GAZETI LA MWANAHALISI LAFUNGIWA NA SERIKALI KWA MIEZI MITATU.RAIS WA MADAGASCAR AZURU TANZANIA.WALIMU DAR WAMPA KISAGO RAIS WA CHAMA CHAO BAADA YA KUTANGAZA KUAHIRISHWA KWA MGOMO.COLLIN POWELL AM-ENDORSE OBAMA,NA MPANGO WA KUM-ASSASSINATE OBAMA WADHIBITIWA.PIA KATIKA MWEZI HUU,SAKATA LA TANZANIA KUJIUNGA NA OIC NA LILE LA KUANZISHWA KWA MAHAKAMA YA KADHI LILITAWALA SANA HUKU MAASKOFU NA VIONGOZI WA KIISLAM WAKIRUSHIANA MANENO.HATARI LAKINI BADO SALAMA.HUKO DRC MAPAMBANO KATI YA MAJESHI YA SERIKALI NA YA WAASI CHINI YA GEN LAURENT NKUNDA YAZIDI KUPAMBA MOTO.

NOVEMBA YAINGIA NA MSISIMKO WA UCHAGUZI WA MAREKANI,NA KAMA ILIVYOTARAJIWA,OBAMA ASHINDA NA KUWEKA HISTORIA YA KUWA MWEUSI WA KWANZA KUWA RAIS WA NCHI HIYO.MALKIA WA DENMARK AZURU TANZANIA.WASANII WA KAMPUNI YA DOWANS WATANGAZA TENDA YA KUUZA MITAMBO YAO MITUMBA.SERIKALI YAFANYA BAILOUT NYINGINE KWA WAHINDI WA TRL,YALIPA TENA MISHAHARA YA WAFANYAKAZI.WAKATI "JAMES BOND WA SASA" CRAIG DANIEL AKISEMA DUNIA IKO TAYARI KWA "JAMES BOND MWEUSI" (A BLACK BOND),WAJUZI WA MAMBO WADAI KWAMBA HAKUNA UWEZEKANO WA KUWEPO A "BRITISH OBAMA" (PM MWEUSI).MKURUGENZI WA TAKUKURU,EDWARD HOSEA,ADAI KWAMBA WATUHUMIWA WOTE WA EPA WAKIKAMATWA NCHI ITAYUMBA!MAMIA WAFA BAADA YA MASHAMBULIZI YA KIGAIDI HUKO MUMBAI,INDIA.MAMIA WAFA NIGERIA KUFIATIA VURUGU ZA KIDINI NCHINI HUMO.WIMBI LA MIGOMO NA KUFUNGWA KWA VYUO VIKUU LASAMBAA HUKO NYUMBANI.WATUHUMIWA KADHAA WA EPA WAFIKISHWA KORTINI,MRAMBA NA YONA NAO WAFIKISHWA KORTINI,WENGI WAJIULIZA: JUSTICE AT LAST AU CHANGA LA MACHO?

HATIMAYE TUMEINGIA DESEMBA,MWISHO WA MWAKA.MAUAJI DHIDI YA ALBINO YAENDELEA HUKO NYUMBANI NA HAKUNA DALILI YA UFUMBUZI WA TATIZO HILO.VURUGU ZA UGIRIKI ZASAMBAA HADI NCHI NYINGINE ZA ULAYA.BUSH AKUMBWA NA KIMBEMBE HUKO IRAK BAADA YA KUVURUMUSHIWA VIATU NA PAPARAZI MMOJA WAKATI WA PRESS CONFERENCE.UCHAGUZI MKUU NCHINI TURKMENISTAN WAELEZEWA KUWA NI KIINIMACHO NA SIO HURU NA HAKI.KATIBU MKUU WA ZAMANI WA WIZARA YA FEDHA,GRAY MGONJA,NAE APANDISHWA KZIMBANI KWA TUHUMA ZA UFISADI.MEMBE AONYA CCM INAWEZA KUSAMBARATIKA,NAPE NNAUYE AMTUHUMU MAKAMBA KUWA ANAKUMBATIA MAFISADI.HALI YA USALAMA NCHINI SOMALIA YAZIDI KUWA MBAYA KUFUATIA MAPIGANO KATI YA KOO MBALIMBALI NCHINI HUMO.MASTERMIND WA MAUAJI YA KIMBARI NCHI RWANDA,THEONESTE BAGOSORA,AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA.TAKUKURU YAKURUPUKA NA KUDAI HAIMCHUNGUZI MKAPA (SIJUI NANI ALIWAULIZA!).KAPTENI MOUSSA DADIS KAMARA AJITANGAZA RAIS WA GUINEA KATIKA MAPINDUZI YALIYOFUATIA KIFO CHA RAIS LANSANA CONTE.PM PINDA ACHACHAMAA KUHUSU MAGARI YA KIFAHARI SERIKALINI,ILA NI KUANZIA MWAKANI KWANI TAYARI SHEHENA YA MAGARI 700 NA USHEE IMESHAAGIZWA!BEI YA MAFUTA SOKO LA DUNIA YAZIDI KUSHUKA LAKINI BEI YA BIDHAA HIYO HUKO NYUMBANI BADO IKO JUU KABLA YA KUKUMBWA NA UHABA USIOELEZEKA.NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI,AELEZA KWAMBA SERIKALI HAIFAHAMU KWANINI BEI YA MAFUTA IKO JUU LAKINI AKADAI YAKO KIBAO KUKIDHI MAHITAJI.AIAGIZA EWURA IKAE KITAKO NA WAFANYABIASHARA KUHUSIANA NA ISHU HIYO (JAPO AGIZO LA EWURA HIYOHIYO KUWATAKA WAFANYABIASHARA HAO KUPUNGUZA BEI YA MAFUTA LIMEENDELEA KUPUUZWA).ATCL YAENDELEA KUSUASUA JAPO UONGOZI WAKE BADO UNAENDELEA KUPETA.MGOMBEA WA CHADEMA KATIKA UCHAGUZI MDOGO MBEYA VIJIJINI AENGULIWA BAADA YA KUWEKEWA PINGAMIZI NA CCM NA CUF,ADAI AMESHAKATA RUFAA.PIA DESEMBA ILISHUHUDIA TAJIRI WA KIMAREKANI BERNARD MADOFF AKIWALIZA WAWEKEZAJI TAKRIBAN DOLA BILIONI 50 KWENYE PONZI SCHEME.
KWA KIFUPI,HAYO NDIYO MATUKIO YA KUKUMBUKWA NA BLOG HII.NAWASHUKURU NYOTE MNAONITEMBELEA.NAAHIDI KUENDELEA KUWALETEA KILE KITU ROHO ZENU ZINAPENDA.MSISITE KUNIKOSOA,KUNISHAURI NA KUTOA MAONI YENU.BLOGU HII NI YENU NAMI NI MTUMISHI WENU.NAWATAKIA HERI NA BARAKA YA MWAKA 2009.MUNGU AWABARIKI SANA.

4 comments:

  1. Katika watu ambao hawatausahau 2008, ni Joji Kichaka na hicho kiatu. Hatasahau hata kama alijifanya kutokustauka.

    Heri ya mwaka mpya kaka Evarest!

    ReplyDelete
  2. Pole sana Kaka. Kwa hakika kuandika ni kazi lakini kutupa zile "top" za mwaka naamini ni kazi ya ziada. Pole sana kwa mizunguko ya maisha na zaidi pole kwa kuuguza na kuondokewa na Mama. Pole kwa kutoweza kumaliza masomo kwa muda, lakini hakuna ulilokosa maana ulilofanya lilikuwa zaidi ya ulilokosa. Zaidi asante kwa maoni yako popote uyatoapo na pia asante kwa uandishi na uchambuzi uufanyao.
    Kila la kheri katika mwaka tuuanzao na tuko pamoja.
    Blessings

    ReplyDelete
  3. ASanteni sana wadau.Heri ya Mwaka mpya.

    ReplyDelete
  4. Nilipopitia vizuri zaidi matukio haya, nikasikitika kukuta habari ya kuondokewa na mama yako.

    Pole sana kaka kuondokewa na mama. Ni sehemu ya maisha tusiyoipenda na inayohuzunisha sana.

    Pole sana kaka.

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget