Leo ni tarehe 10/05/2011,na deadline aliyotoa Ridhiwani Kikwete,mtoto wa Rais Jakaya Kikwete,kwa Katibu Mkuu wa Chadema,Dkt Willibroad Slaa,na Mwenyekiti wa DP,Mchungaji Christopher Mtikila,imemalizika jana.Ridhiwani alitoa dealine ya siku saba kuwataka Dkt Slaa na Mtikila wamwombe radhi kufuatia tuhuma zao dhidi yake kuwa amekuwa bilionea kwa njia za kutilia shaka.
Ni mapema mno kubashiri chochote lakini habari ifuatayo inaweza kutoa mwangaza kuhusu uwezekano wa Ridhiwani kwenda mahakamani kama livyotishia au kutokwenda (which would imply tuhuma hizo dhidi yake ni za kweli).Soma kwanza habari yenyewe
Mtoto wa Rais Kikwete ang’akana Janet JosiahMTOTO wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani, amesema hataki kufuatiliwa maisha yake na wanasiasa hasa wanaomtuhumu kuwa ni bilionea huku akisisitiza kuwashughulikia waolimchafua.Ridhiwani, alisema hayo jana alipozungumza na Tanzania Daima akitakiwa kueleza hatua atakazochukua baada ya muda wa siku saba aliowapa Mwenyekiti wa Demokratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Willbrod Slaa kupita.Awali, mtoto huyo wa Rais aliwataka wanasiasa hao wamwombe radhi katika kipindi cha siku saba vinginevyo angewapeleka mahakamani kwa kuwa wamemchafua pamoja na familia yake.Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika kwa njia ya simu, ili kujua lini angekwenda mahakamani kuwafungulia mashtaka viongozi hao, alijibu kwa jazba kwamba jambo hilo linahusu maisha yake hivyo haoni sababu ya kufuatiliwa na vyombo vya habari.“Jambo la kuwafikisha wanasiasa hao mahakamani si jambo lenu, hilo ni jambo linalonihusu mimi na maisha yangu hivyo nitachokifanya nakijua mwenyewe,” alisema Ridhiwani huku akisisitiza kwamba hata alipozungumza na waandishi wa habari juma lililopita alisema lengo lake ni kuueleza umma na sio kufuatiliwa maisha yake.Kwa nyakati tofauti Mchungaji Mtikila na Dk. Slaa, walimtuhumu Ridhiwani kwa ukwasi huku wakiitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kumchunguza.
CHANZO: Tanzania Daima
Pasipo nia ya kufanya hitimisho lolote,nashindwa kumwelewa Ridhiwani anaposema "jambo la kuwafikisha mahakamani wanasiasa hao si jambo lenu..."Hivi sio Ridhiwani huyuhuyu aliyeitisha mkutano na waandishi wa habari,ambapo pamoja na mambo mengine alikanusha tuhuma zilizotolewa na wanasiasa hao,na akawataka wamwombe rahdi vinginevyom angewafikisha mahakamani?Sasa kama jambo la kuwafikisha mahakamani wanasiasa hao si jambo lao (wanahabari) kwanini basi aliitisha mkutano nao na kuwaelezea same thing anachodai hakiwahusu?
Waandishi wa habari wana kila sababu ya kumhoji kama atawafikisha Slaa na Mtikila mahakamani au la.Kwanini?Kwa sababu,kwanza,alitamka hayo mbele ya waandishi hao hao wa habari,na pili,yeye ni mtoto wa Rais na ametuhumiwa kuwa bilonea kwa mgongo wa baba yake.Sasa hakuna Mtanzania asiyependa kujua kama madai ya wanasiasa hao ni zushi mtupu au yana ukweli ndani yake.
Wito wangu kwa Ridhiwani ni huu:TIMIZA AHADI YAKO YA KWENDA MAHAKAMANI.Tuhuma za wanasiasa hao dhidi yako si ndogo,kwani licha ya kukugusa wewe binafsi zinamgusa pia baba yako ambaye ni Rais wetu (na ambaye siku za karibuni ametangaza kuwa anadhamiri kuukalia kooni ufisadi).Usipokwenda mahakamani itaonyesha kuwa tuhuma hizo zina ukweli.
And to make matter even worse,Dkt Slaa na Mtikila wanaweza kukufungulia kesi ya kuwakashifu,kwani ulidai ni wazushi tu.Sasa kama sio wazushi then go to the court as you promised,bearing in mind kwamba wewe ni mwanasheria.
Enewei,tunasikiliza WHAT'S NEXT!
Ngoma inogire!
0 comments:
Post a Comment