Osama (kushoto) na Zawahiri |
Ayman al-Zawahiri,daktari mwenye umri wa miaka 59 aliyezaliwa Misri,anatarajia kuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda baada ya kuuawa kwa Osama Bin Laden.
Gazeti la Wall Street Journal la Marekani linamwelezea Zawahiri kuwa ni mwenye msimamo mkali kuliko Osama,japo ana mapungufu wa mvuto (charisma) na utajiri wa Osama.
Taarifa za kwenye kompyuta Zililopatikana katika eneo alilokuwa akiishi Osama,kama zinavyoelezwa HAPA na mtandao wa Politico,zinaweza kuwasaidia mashushushu wa Marekani kufahamu mengi zaidi kuhusu Al-Qaeda na kupelekea uwezekano wa kufahamu alipo Zawahiri.Hadi itapokuwa hivyo,gaidi huyo aliyekuwa namba 2 (Osama akiwa namba 1) katika kundi la Al-Qaeda anaendela kubaki kwenye orodha ya Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) ya watu wanaosakwa kwa udi na uvumba,na tishio kubwa.
Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) limeshawahi kukaribia kumkamata Zawahiri.Huku akiwa mafichoni,gaidi huyo alitoa mkanda wa video kuhusu vuguvugu la mageuzi nchini Misri mwanzoni mwaka huu,akisema demokrasia inawezekana tu katika ukafiri.Pia alimtukana Rais Obama akitumia neno la ki-baguzi wa rangi (racial epithet).
CHANZO: Huffington Post
0 comments:
Post a Comment