Hatimaye tovuti hii imeamua kushiriki kuwania tuzo za blogu za Kitanzania zijulikanazo kama TANZANIAN BLOGS AWARDS.
Blogu hii inawania tuzo kwenye kundi la BLOGU BORA YA SIASA au kwa kimombo BEST POLITICAL BLOG.
Cha kufanya,nenda kwenye link hii http://www.tanzanianblogawards.com/2011/04/faqs.html
Kisha jaza kama ifuatavyo (nimeweka picha za vipengele vilivyopo kwenye fomu ya kuchagulia blogu uipendayo
Hapa wanahitaji jina la mwandishi wa blogu.Kwahiyo kama unaona Kulikoni Ughaibuni inastahili basi jina linalotakiwa hapa chini ni EVARIST CHAHALI
Hapa chini wanahitaji jina la makazi.Makazi yangu ni GLASGOW, SCOTLAND
Hapa chini wanahitaji jina la blogu.Kama ujuavyo,blogu hii inaitwa KULIKONI UGHAIBUNI
Hapa wanakupa fursa ya kuchagua ni kundi gani unadhani blogu uipendayo inastahili tuzo.Tovuti hii inaomba kura yako katika kundi la blogu za siasa,yaani hapo chini walipoandika BEST POLITICAL BLOG.Weka tiki hapo kwenye kipengele cha 19
Hapa wanauliza kama blogu uliyoipigia kura ina "mambo ya kiutu uzima/ngono".Na kama unavyofahamu,huo ni mwiko kwa tovuti hii.Kwahiyo,kama unaona tovuti hii inastahili tuzo,tiki hapo kwenye NO
Malizia kwa kubonyeza kitufe kilichoandikwa SUBMIT
NATANGULIZA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI
NAKUTAKIA KILA LA HERI MY DEAR,, AND WHY NOT YOU ? KEEP UP THE GOOD WORK NA PAMOJAAA..STAY BLESS ALWAYS.
ReplyDeleteASANTE SANA FLORA.PAMOJA AND STAY BLESSED
ReplyDelete