Monday, 9 May 2011


Baada ya Rais Jakaya Kikwete kuonekana kituko kwa kupokea hundi yenye tarakimu zinazokinzana na thamani ya hundi hiyo kwa maandishi,na yeye kuonekana akitoa tabasamu la nguvu (trademark yake),sasa imekuwa zamu ya mkewe.

Ukiangalia hundi anayokabidhiwa Mama Salma Kikwete (pichani juu) utabaini kuwa thamani ya hundi kwa maandishi ni shilingi milioni tatu na laki nane,ambayo kwa tarakimu inapasa kuwa 3,800,000.Sasa sijui ni umaimuna au uzembe tu,tarakimu za hundi hiyo zimeandikwa kichakachuaji- TZS 3,800,00.Unaweza kudhani ni shilingi elfu tatu mia nane (3,800.00) lakini maelezo ya hundi yatakusuta kwani yametamka bayana kuwa ni SHILINGI MILIONI TATU NA LAKI NANE.

Na hapa chini tunamwona mtu tuliyemkabidhi dhamana ya kutuongoza Watanzania takriban milioni 50 akikenua meno kwa furaha huku hundi imeandikwa TWO HUNDRED THOUSAND lakini tarakimu ni 300,000



Hivi kabla ya hafla hizi, hao jamaa wa  PSU  hawakagui vitu anavyokabidhiwa Rais au mkewe?Au nao hadithi ni hiyohiyo?

Na haya ni madudu nadra tunayobahatika kuyaona hadharani.Je yanayofanyika kwa kwa faragha ua sirini inakuwaje?Npatwa na wasiwasi kuwa hadi Kikwete anaondoka madarakani hapo 2015 (kama hatoombwa na mafisadi kugombea tena ili aendelee kuwalinda) tunaweza kushtukia Tanzania ishauzwa zamani hizo.Unashangaa nchi inawezaje kuuzwa?Waulize "Zaire" (DRC Kinshasa)!!!!

Chanzo: Nimkutana na habari hii kwa ndugu yangu MPAYUKAJI MSEMAOVYO

Related Posts:

  • MHESHIMIWA MBUNGE HUYU VIPI?MBUNGE wa Jimbo la Buchosa, Samwel Chitalilo ameingia katika mkasa mpya baada ya kudaiwa kumshambulia Mabula Matulanya, ambaye ni mlinzi wa ghati la ofisi ya kivuko cha Nyakaliro Kome, linalomilikiwa na serikali.Mlinzi huyo a… Read More
  • SOKO LA TANDIKA LAUZWAPicha kwa hisani ya MjengwaMWAKA 2006,MANISPAA YA TEMEKE ILITANGAZA AZMA YAKE YA KULIBORESHA SOKO LA TEMEKE.LAKINI KATIKA HALI YA KUSTAAJABISHA,KUNA TAARIFA KWAMBA SASA SOKO HILO LIMEUZWA KWA MWEKEZAJI.KWA MWENENDO HUU,SI AJA… Read More
  • SWALI:MWEKEZAJI GANI M-BABAISHAJI AMEBEBWA SANA 2008?Photo courtesy of MJENGWAKURA YANGU INAWAANGUKIA WABABAISHAJI WA TRL.CHEKI "MBELEKO" NYINGINE HII KUTOKA KWA SUMATRA:HATIMAYE Kampuni ya MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imeiruhusu Kampuni ya R… Read More
  • SALAMU ZA FUNGA MWAKA KUTOKA KWA WADOSI WA RELWE (TRL)KAMPUNI iliyopewa jukumu la kusimamia na kutunza mali za lililokuwa Shirika la Reli Tanzania (RAHCO), imeanza kukatakata injini 27 na mabehewa 19 ili yauzwe kama chuma chakavu.Mabehewa hayo na injini zake yanadaiwa yalikuwa n… Read More
  • KIPIGO CHA SIMBA KUTOKA KWA YANGA:NILIKITARAJIA LAKINI MATARAJIO MENGINE HAYAJATIMIAPicha kwa hisani ya SPOTI NA STAREHEUbabaishaji unakwamisha sana maendeleo ya taifa letu.Lakini hapa nataka nizungumzie ubabaishaji kwenye uongozi na uendeshaji wa vilabu vya Simba na Yanga.Hebu soma kwanza hapa chini kabla h… Read More

2 comments:

  1. This is a jokeeeeeeeeeee lol

    ReplyDelete
  2. hayo sio matatizo ya viongozi hayo matatizo ya watu waliongozana na raisi ambao wao ndio wanalihakikisha kwanza kabla kufika kwa kiongozi sawa,hao walinzi wake wanafanya nini?na ndio wenye hilo kosa,wao wakihahakisha ndio wanaruhusu kukabidhiwa raisi,mdau bwegenaz

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget