Monday, 16 May 2011



Yanga wampa uchifu Manji 
Sunday, 15 May 2011 20:54

Clara Alponce
WAZEE wa klabu ya Yanga jana walimkabidhi Mkuki, Ngao na Kigoda kama alama ya cheo cha uchifu kwa aliyekuwa mfadhili wao Yussuf Manji.Manji alikabidhiwa heshima hiyo na kamati ya wazee ya muafaka wa Yanga chini ya kiongozi wake Mzee Yahaya Akilimali.

Akizungumza kwenye hafla hiyo mama Shadia Karume alisema Manji amejifunza mengi Yanga na amerejea rasmi kwa ajili ya kufanya kazi ya kuijenga Yanga mpya.Mama Karume alisema," Manji anatakiwa kujua hasira, jazba hazifai namtaka asahau yote yaliyopita."

Mama Karume aliongeza kuwa kuna watu wengi waliofanya mambo makubwa na mazuri Yanga huko nyuma na Manji ni moja wao."Mume wangu ndiye aliyejenga jengo la Yanga hapa Dar es Salaam, lakini angejisikia vibaya kama lingeachwa na kuharibika bila ya kufanyiwa ukarabati kama aliousimamia Manji,"alisema Mama Karume ambaye pia alimtaka Manji kujenga jengo lingine la Yanga huko Zanzibar kwa sababu uwanja umeshapatikana.

Tukio hilo lilishuhudiwa na viongozi wa serikali akiwemo Jamal Rwambo, Mbunge Mussa Zungu, Mudhihir Mudhihir pamoja na wachezaji wa Yanga huku burudani ikitolewa na bendi za Msondo, Sikinde na Tanzanite

CHANZO: Mwananchi.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget