Wakati Gazeti la Serikali HABARI LEO linaripoti
Gazeti la MWANANCHI kwa upande wake linahabarisha kwamba
WALIMU kote nchini jana walianza mgomo usio na kikomo wa kuishinikiza serikali kuwalipa madai yao ya zaidi ya Sh16 bilioni, katika siku ambayo ilijaa matukio mbalimbali, yakiwemo ya kuchapwa viboko kwa walimu waliokataa kugoma, jitihada za serikali kukwamisha mgomo, walimu kuripoti kazini na kuanza kupiga soga na wengine kuanza kulipwa madai yao.Waandishi wetu kutoka mikoa mbalimbali wanaripoti kuwa mgomo huo, uliotakiwa kuanza Oktoba 15 lakini ukakwamishwa, ulifanikiwa kwa asilimia 70 ikiwa ni pamoja na baadhi ya wanafunzi kushindwa kuanza mitihani ya kumaliza mwaka, lakini katika baadhi ya shule walimu walifundisha kama kawaida.Katika ufuatiliaji uliofanywa na Mwananchi katika sehemu kadhaa, walimu ama hawakwenda kabisa kazini ama walienda na kufanya vikao, vilivyoonekana kuwa vya kupoteza muda. Walimu wakuu, wakurugenzi wa halmashauri na wakuu wa wilaya wengi walidai kuwa hali ilikuwa shwari kwenye maeneo yao, lakini waandishi wetu walipoenda kwenye shule walikuta migomo ikiendelea kwa mikutano hiyo ya soga maofisini, huku wengine wakipata kinywaji kwenye baa jirani.Mgomo huo ni matokeo ya serikali kushindwa kuwatimizia walimu madai yao nane tangu walipotangaza mgomo na kutoa siku 60 kwa serikali kuhakikisha inatatua matatizo hayo. Madai hayo ni pamoja na malimbikizo ya Sh6.6 bilioni, masomo (Sh1.01 bilioni), likizo (Sh1.07 bilioni), matibabu (589.9 milioni), posho za kujikimu (Sh565.8 milioni) na mirathi (72.9 milioni), kwa mujibu wa serikali.Pia walimu wanadai kupandishwa daraja na kuundwa kwa baraza la maridhiano.Serikali imekuwa ikidai kila mara kuwa inaendelea na zoezi la uhakiki na kuwataka walimu kuvuta subira, lakini baada ya Mahakama ya Rufaa kubatilisha amri ya muda ya kuzuia mgomo, kasi ya kushughulikia madai hayo ilionekana kuongezeka na jana baadhi ya walimu walianza kulipwa madai yao, huku Chama cha Walimu (CWT) kikisitiza kuwa mgomo utaisha baada ya walimu kulipwa senti ya mwisho.Mwandishi wetu, Shija Felician anaripoti kutoka Kahama, Shinyanga kuwa walimu waliotii uamuzi wa kugoma, jana walitembeza viboko kwa wenzao walioingia darasani kufundisha.Katibu wa CWT Kahama, Said Mselem alisema asilimia 70 ya walimu wote walioko wilayani hapa waligoma, lakini wale wachache ambao waliandikisha majina kuonyesha wamehudhuria kazini, walijikuta kwenye hali ngumu baada ya kuondolewa madarasani kwa viboko na wenzao waliogoma.Sakata hilo lilitokea kwenye shule za msingi za Kilima "A" na "B", Nyashimbi na Mbulu, ambako walimu wachache walioamua kuingia darasani waliondolewa kwa viboko.Baadhi ya shule zilizotembelewa na waandishi wa habari jana zilikuwa zimefungwa wanafunzi walikuwa wamezagaa nje wakicheza. Viongozi wa serikali ngazi ya wilaya, tarafa, kata na vijiji walikuwa wakizunguka kila shule kufuatilia walimu waliogoma baada ya Wizara ya Serikali za Mitaa (Tamisemi) kuagiza hivyo juzi.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kahama, Theresia Mahango alisema amepokea Sh34,300,000 kwa ajili ya kulipa madai ya walimu. Walimu wilayani Kahama wanadai zaidi ya Sh300 milioni, lakini Mahango alisema fedha hizo ni kwa ajili ya malipo yaliyoonekana kuwa ni halali tu.Awali jana, Katibu Tawala wa Kahama, Bulla Gwandu alisema walimu walikuwa darasani wakifundisha, lakini mashuleni hali haikuwa hivyo.Jijini Dar es salaam, Hussein Kauli anaripoti kuwa walimu walianza mgomo wao wakifananisha ahadi za serikali na ahadi za kuku kwa vifaranga kuwa atavinyonyesha wakati ni jambo lisilowezekana.Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Pwani, Method Rugambarala alisema walimu wake walianza mgomo asubuhi na walimueleza kuwa wanafanya hivyo kuunga mkono tamko la CWT, lakini akasema watafika maeneo ya kazi kuhofia vitisho vya serikali.Naye mmoja wa walimu wakuu wa shule za msingi Temeke ambaye hakutaka kutajwa gazetini, aliilalamikia serikali kuwa inatafuta ugomvi na walimu kwa kuwa haina sababu ya kutowalipa madai yao."Serikali haina sababu inayowafanya wasitulipe madai yetu kwa kipindi kirefu kiasi hiki. Upole wetu kwa watu hawa umefikia kikomo na tutashindwa kufanya kazi hali ambayo itawaathiri watoto wetu," alisema.Walimu wengi wa shule za msingi za Kunduchi na Pius Msekwa hawakuhudhuria shuleni jana, hatua iliyofanya kushindwa kuanza kwa mitihani ya mwisho wa mwaka.Walimu wengine waliounga mkono mgomo huo ni wa shule za msingi za Bunge, Uhuru Mchanganyiko, Boma na Diamond za Wilaya ya Ilala, hali iliyowafanya baadhi yao kuandamana kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro kufikisha kilio chao.Naye, Patricia Kimelemeta anaripoti kuwa, zaidi ya asilimia 75 ya walimu wa Manispaa ya Kinondoni walifika shuleni kama kawaida, lakini hawakufundisha.Mkuu wa Wilaya ya Kindondoni, Kanali Fabian Massawe alisema kuwa alipata taarifa kuwa baadhi ya walimu hawakufika shuleni na kuelezea kitendo hicho kuwa ni kiburi kwa serikali ambayo tayari imeanza kutoa fedha kulingana na madai yao nchi nzima.Naye Aziza Nangwa, anaripoti kuwa shule za msingi za Ubungo Kibangu na Ubungo Kisiwani hakukuwepo na mgomo."Sisi bwana tunaendelea na kazi kama kawaida na suala la kugoma kwetu halipo. Si unaona tunavyochapa kazi au huoni watoto wanaingia madarasani kama kawaida kwahiyo tunafuata selikali inasemaje," alisema Mwalimu Kilimba.Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ubungo, Kibangu Juma Abdallah alisema kuwa suala la kugoma ni la mtu binafsi kwa hiyo wanaendelea na kazi.Mwandishi wetu, Angela Mwakilasa anaripoti kuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Air Wing, Devota Stambuli alisema kuwa, taarifa za mgomo alizisikia kwenye vyombo vya habari na kwamba ataendelea kufundisha hadi apate barua ya CWT.Kutoka Morogoro, Samuel Msuya anaripoti kuwa asilimia 70 ya walimu waliitikia wito wa kugoma.Katibu Mkuu wa CWT Morogoro, Issa Ngayama alisema walimu katika wilaya za Ulanga, Kilombero, Kilosa na Mvomero hawakuingia darasani, lakini wa Manispaa ya Morogoro waliendelea kufundisha.Ngayama alidai kuwa walipata taarifa kutoka Ulanga na Kilombero kuwa, polisi walikuwa wakipita sehemu kadhaa kuhakikisha kuwa mgomo unadhibitiwa."Lakini sisi tunaona kuwa mgomo umefanikiwa kutokana na viongozi wa serikali kuacha kazi zao na kuzunguka katika shule kuhakikisha wanauzima mgomo huu," alisema.Hata hivyo, uchunguzi katika shule mbalimbali za Manispaa ya Morogoro na Ulanga unaonyesha kuwa walimu waliripoti kwenye vituo vya kazi, lakini hawakuingia darasani kwa madai ya kuandaa ripoti za mwaka.Katibu wa CWT Kilombero, Maswi Mudani alisema walimu wamefuata maelekezo ya chama chao ya kugoma hadi walipwe haki zao, wakati wilayani Kilombero, Mkurugenzi Mtendaji, Alferd Luanda alisema wamepokea Sh63 milioni kwa ajili ya malipo hayo.Naye Juddy Ngonyani wa Sumbawanga anaripoti kuwa, walimu wa shule za sekondari na msingi walianza mgomo na kufanya wanafunzi wa shule nyingi kupata fursa ya kucheza nje tangu asubuhi.Mwananchi ilishuhudia hali hiyo katika shule za msingi Mwenge A na B, Chanji, Kizwite, Chemechem, Majengo, Jangwani, Kanda, Mazwi na Shule ya Kutwa Sumbawanga, wakati walimu wengi wa shule za sekondari hawakwenda kabisa kazini .Katika Shule ya Msingi ya Jangwani, Mwalimu Mkuu Morris Kibona alisema kuwa walimu wameripoti kazini kama kawaida asubuhi, lakini hawakuingia darasani isipokuwa wale wa darasa la kwanza.Mmoja wa walimu hao, Mary Kameme alisema: "Hatufurahishwi na kitendo cha kugoma kwa kuwa kinawaathiri wanafunzi, lakini ni lazima serikali itambue kuwa kama walimu wamefikia hatua ya kugoma, inamaanisha wamechoshwa na hali iliyopo."Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwenge "A", Gilbert Mwangosi alisema: "Leo nimechelewa kwa sababu nimekuja kwa mguu... sikuona sababu ya kuchoma mafuta yangu ya pikipiki ili kuwahi shule wakati leo walimu tunaanza mgomo nchi nzima."Kutoka Arusha, Hemed Kivuyo anaripoti kuwa kulikuwa na walimu waliogoma na walioamua kuingia darasani.Uchunguzi uliofanywa jana katika shule za msingi na sekondari umebaini kuwa pamoja na walimu wengi kukataa kushiriki mgomo, wengi walikaa kwenye vikundi kujadili hatima yao.Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Uhuru ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema hakukuwepo na mgomo isipokuwa baadhi ya walimu wapo katika majadiliano na kwamba, anawasubiri ili waweze kusimamia mitihani."Hakuna mgomo kama unavyoona walimu wapo ofisini na wengine wale kule nje wapo katika majadiliano na ninawasubiri waje kusimamia mitihani," alisema mwalimu huyo.Lakini walimu walioongea na Mwananchi walisema hawawezi kuingia madarasani kwa kuwa, kufanya hivyo ni kusaliti msimamo wa wenzao."Hatuingii darasani; huyo mwalimu aliyekueleza hakuna mgomo yeye ndiye hayupo katika mgomo, lakini sisi tunagoma," alisema mmoja wa walimu hao ambao hawakutaka kuandikwa majina yao gazetini.Katika shule ya msingi Ungalimited, baadhi ya walimu waliingia madarasani kama kawaida huku baadhi yao wakiwa katika baa ya jirani iliyoandikwa `NARA` wakinywa bia, wakidai kuwa wameamua kujiburudisha kwa kuwa kwa sasa wanasimamia mitihani.Katibu wa CWT Arusha, Nuru Shenkalwa alisema mpaka sasa chama hicho hakina tamko lolote na kwamba wanasubiri maelekezo toka juu, wakati Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Evance Balama alisema kuwa amefanya ziara ya ghafla katika baadhi ya shule na hapakuwepo na mgomo wowote kwa walimu.Mwandishi wetu wa Mbeya, Brandy Nelson anaripoti kuwa baadhi ya walimu waliamua kuendelea na kazi, ikiwa ni pamoja na kusimamia mitihani ya kumaliza mwaka, wakidai kuwa hawajapata taarifa ya maandishi ya kuwataka wagome."Taarifa za mgomo tumezisikia kwenye vyombo vya habari, lakini hatujapata barua yoyote kutuarifu kuhusu mgomo kutoka CWT mkoa," alisema Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Sisimba, Ephata Mbisemmoja.Naye Afisa Elimu wa Mbeya, Juma Kaponda alisema kuwa tayari Sh 636,507,743 zimeshafika kwa ajili ya kulipa walimu madai yao na kwamba zimeanza kufanyiwa utaratibu wa kuingizwa katika akaunti za halmshauri kwa ajili ya kuanza kuwalipa walimu.Katibu wa CWT Mbeya, Tweedsmur Zambi alikiri kupata taarifa kuwa katika baadhi ya shule walimu waliamua kuendelea na kazi."Lakini si kweli kwamba hawana taarifa ya mgomo. Naomba uelewe kuwa mgomo kwa Mkoa wa Mbeya upo kama ulivyo mikoa mingine,"alisema.Jijini Tanga walimu waliochelewa vituoni walitumiwa ujumbe mfupi wa simu (sms) kubembelezwa wafike vituoni, anaripoti Burhani Yakub.Walimu kadhaa walitumiwa ujumbe kwenye simu zao wakiombwa kufika shule na kuhakikishiwa kuwa fedha zao zimeshawasilishwa na kwamba, ziko kwenye akaunti ya halmashauri.Mwananchi ilionyeshwa ujumbe uliokuwa kwenye simu ya mwalimu mmoja wa shule ya msingi iliyo katikati ya Jiji la Tanga ikisema: “Unoambwa kufika shuleni kwako, usifanye mgomo fedha zimeshaingia na mtaanza kulipwa leo.”“Hata wenzangu wa shule mbalimbali wametumiwa ujumbe kama huu hivyo tukaamua kuja shuleni baada ya kuhakikishiwa kuwa, fedha zetu zimeshawasilishwa,” alisema mwalimu huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwajuma.Kutoka mkoani Mwanza, Frederick Katulanda anaripoti kuwa walimu waliendesha mgomo baridi, baadhi wakiripoti kazini na wengine kutoripoti kabisa huku wakisubiri taarifa za malipo yao.Karibu katika shule zote za msingi kulikuwa na walimu wachache na hivyo kushindwa kufundisha na kuachia wanafunzi waendelee na michezo nje.Katika shule za Nyamagana, Buhongwa, Kitangiri, Mirongo, Mbugani na Nyamanoro, walimu walikuwepo, lakini hawakuweza kufundisha.Mmoja wa wanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya Kitangiri, Zelaida Filbert alisema ingawa baadhi ya walimu wamefika shuleni hapo, hakuna aliyefundisha na kuongeza: “Tumekaa darasani kwa muda mrefu sasa nimeamua kuondoka tu kwenda nyumbani, walimu hawafundishi wapo tu. Alikuja mwalimu wa Hisabati na kutupatia mitihani yetu halafu akaondoka.”Mwanafunzi mwingine, Charles James wa shule ya Nyanza alisema leo hatahudhuria shule kutokana na ukweli kuwa, walimu wanaendelea na mgomo.Mwenyekiti wa CWT Mwanza, Benedicto Raphael alisema jana walikuwa na mgomo baridi kutokana na taarifa kuchelewa kuwafikia walimu wengi na kutangaza kuwa mgomo rasmi ni leo.“Serikali imetimiza madai mawili kati ya nane, tunaendelea na mgomo wetu. Tunaiomba serikali kutekeleza madai yetu badala ya kututolea vitisho na napenda itambue hatutaogopa vitisho... tutaendelea kudai haki yetu mpaka ilipwe,” alisema na kubainisha kuwa walimu wa Mwanza wanadai Sh1.1 bilioni.Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya jiji alisema wamelipa jumla ya madai 67 kiasi cha Sh 37 ml. kuanzia majira ya saa 3:00 asubuhi. Kuna madai 195 ya walimu, lakini madai 128 yamebainika kuwa na kasoro.Julieth Ngarabali anaripoti kutoka mkoani Pwani kuwa, wanafunzi walishindwa kufanya mitihani ya kumaliza mwaka kutokana na mgomo wa walimu.Habari ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa shule nyingi za msingi katika wilaya za Kibaha Vijijini, Bagamoyo, Kisarawe na Kibaha Mjini mitihani haikuanza kama ilivyopangwa.Katika shule kadhaa ikiwemo Msangani, Nyumbu, Umoja, Mwendapole na Chalinze walimu walikiri kuwa mitihani haikufanyika, lakini wakasema kuwa hiyo ilitokana na kutokamilika kuchapishwa na kwa sababu ya mgomo, lakini katika shule za Mkuza, Mkoani, Maili Moja, Nyumbui na Soga wanafunzi waliendelea na mitihani.Baadhi ya walimu walisema mitihani itaanza Jumatano.Mwenyekiti wa CWT, Pwani Kelvin Mahundi alisema walimu waliingia darasani kutokana na kuogopa vitisho vya serikali, lakini si kwamba hawana nia ya kugoma, wakati mwenyekiti wa Kibaha, Donald Machapula alikiri kuwepo kwa shule ambazo walimu waligoma kusimamia mitihani."Sidhani hapa kuna la maana linaloendelea; naishauri Serikali iharakishe malipo ya walimu maana hakuna kitakachokuwa kinafanyika huko kwa watoto mashuleni," alisema Mahundi.Mkurugenzi wa Wilaya ya Kibaha, Festo Kang'ombe alisema wamepokea hundi ya Sh55 milioni kwa Wilaya ya Kibaha Vijijini na Sh51,818,107 kwa Kibaha Mjini na kwamba wahasibu jana walikuwa wakihaha kuandika malipo kwa walimu.Hali ya mgawanyiko pia ilionekana mkoani Singida, ambako baadhi ya walimu waliingia darasani na wengine kutoenda kabisa kazini, anaripoti Jumbe Ismaily.Katika Shule ya Msingi ya Kindai, wanafunzi wake walihudhuria shuleni, lakini hawakuweza kusoma kutokana na mgomo huo, hali iliyokuwa pia katika shule za msingi za Bomani, Sabasaba, Ukombozi na Chief Senge Sekondari ambako wanafunzi walitakiwa kurudi nyumbani.Katika shule za Utemini na Singidani, walimu wote walihudhuria kazini na kusimamia mitihani ya mwisho wa mwaka.Waandishi wetu walio Babati, Iringa na Handeni wanaripoti kuwa hakukuwepo na mgomo na zoezi lililotawala jana lilikuwa ni malipo.

HABARI LEO LIMEFANYA KAZI YAKE KAMA YALIVYOKUWA YANAFANYA MAGAZETI YA SERIKALI YA KIKOMUNISTI YA MUUNGANO WA KISOVIETI (USSR),KUTOA TAARIFA ZINAZOASHIRIA UDOGO AU KUTOKUWEPO KABISA KWA TATIZO (KATIKA HABARI HII,MGOMO WA WALIMU UMEDORORA,HAIJALETA ATHARI ZILIZOKUSUDIWA,MAMBO YOTE "POA",NK).UKISOMA MWANANCHI UTAGUNDUA KUWA HALI NI TOFAUTI NA INAYOZUNGUMZIWA NA HABARI LEO.IFAHAMIKE KWAMBA HAKUNA ANAYENUFAIKA KWA KUPEWA TAARIFA ZA KUPENDEZESHA MACHO.SUALA HAPA SIO UKUBWA AU UDOGO WA MGOMO HUO BALI ATHARI ZAKE KWA WADOGO,WATOTO NA WAJUKUU ZETU.IKUMBUKWE PIA KWAMBA TUKIO HILI LINATOKEA WAKATI SUALA LA MIGOMO LINAANZA KUWA KAMA "FASHENI" FLANI.
HILI TATIZO LINGEWEZA KUEPUKWA ZAMANI HIZO LAITI WAHUSIKA WASINGEENDEKEZA PRIORITIES ZAO BADALA YA ZA WALE WANAOPASWA KUWATUMIKIA.UTARATIBU WA KUTATUA MATATIZO KWA NJIA YA ZIMAMOTO NI HATARI SANA,YAANI MPAKA TATIZO LITOKEE NDIO ZIANZE JITIHADA ZA KUTAFUTA UFUMBUZI.HIVI SIKU ZOTE HIZI WALIKUWA WAPI HAO WANAOPASWA KUHAKIKI MADENI YA WALIMU?HIVI HAKUNA WATU WANAOLIPWA MISHAHARA KWA AJILI YA KAZI HIYO YA KUHAKIKI NA KUHAKIKISHA MASLAHI YA WALIMU NA WATUMISHI WENGINE WA UMMA?
KUKIMBILIA MAHAKAMANI KUZUIA MIGOMO NI SULUHISHO LA MUDA TU,UFUMBUZI WA KUDUMU NI KUWAJIBIKA IPASAVYO KATIKA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU (UWAJIBIKAJI).TATIZO LA WALIMU NI SEHEMU NDOGO TU YA MATATIZO KADHAA AMBAYO KWA HAKIKA YANGEWEZA KUEPUKIKA LAITI WAHUSIKA WANGEWAJIBIKA IPASAVYO.WALIMU WATALIPWA KWA ZIMAMOTO,INAWEZA KUZIMA MGOMO LAKINI KESHO TRL NAO WATAGUNDUA KUWA WAKIGOMA WATAFANYIWA MALIPO YA ZIMAMOTO,KESHOKUTWA MADAKTARI,MANESI,NK NK NK.
WAHUSIKA WATEKELEZE WAJIBU WAO.PIA,SISI NI MASIKINI NA TUNAPASWA KUISHI KIMASIKINI KAMA TUNATAKA KUMUDU GHARAMA ZA MAISHA YETU.UNUNUZI WA VITU VYA FAHARI NA MATUMIZI MENGINE YASIYO YA LAZIMA YANAATHIRI KWA KIWANGO KIKUBWA UWEZO WETU WA KUJIHUDUMIA NA KUJIENDESHA WENYEWE.HIVI NI LAZIMA KILA MHESHIMIWA ATUMIE "SHANGINGI" LA MAMILIONI KADHAA?JE GHARAMA ZA GARI HILO ZINGEKATWA JAPO ROBO ZISINGEWEZA KUWALIPA WATUMISHI WENZETU WANAODAI MALIMBIKIZO YAO?
0 comments:
Post a Comment