Tuesday, 18 November 2008


UONGOZI wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) umekifunga chuo hicho kwa muda usiojulikana kutokana na mgomo wa wanafunzi.

Uongozi wa chuo hicho umefikia uamuzi huo, baada ya wanafunzi katika chuo hicho kufanya mgomo kuishinikiza serikali kuwarudisha vyuoni wanafunzi waliofungiwa.

Kabla ya kufungwa kwa chuo hicho jana, bodi ya chuo hicho ilifanya kikao, ili kujua wachukue uamuzi gani.

Awali, akizungumza na Tanzania Daima jana chuoni hapo, Rais wa DIT, Cleophace Maharangata, alisema mgomo wao bado unaendelea lakini bodi ya chuo inafanya kikao kuamua kama chuo kifungwe ama la.

“Sisi tunasubiri tamko baada ya kikao…uamuzi wowote utakaotolewa sisi tupo tayari,” alisema.

Naye mwalimu wa chuo hicho ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini alisema mgomo huo upo kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza, huku wanafunzi wa astashahada (diploma) wakiendelea na masomo kama kawaida.

Awali Rais wa wanafunzi hao, alisema mgomo huo ulianza rasmi juzi baada ya wanafunzi kutoingia madarasani huku wakiwa wameshika mabango yaliyobeba ujumbe mbalimbali.

Kufungwa kwa chuo hicho kunafanya idadi ya vyuo vilivyofungwa kufikia saba. Vyuo vingine ambavyo vimeshafungwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), Chuo Kikuu cha Elimu Mkwawa (MUCE), Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na Moshi Ushirika.

Related Posts:

  • SERIKALI YAAMURU WANAFUNZI MLIMANI WAINGIE MADARASANISerikali imewataka wanafunzi wote wa vyuo vya elimu ya juu nchini kuingia madarasani mara moja ifikapo saa moja asubuhi leo. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya … Read More
  • WIMBI LA MIGOMO: "DAR TECH" NAYO YAFUNGWAUONGOZI wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) umekifunga chuo hicho kwa muda usiojulikana kutokana na mgomo wa wanafunzi.Uongozi wa chuo hicho umefikia uamuzi huo, baada ya wanafunzi katika chuo hicho kufanya mgomo kui… Read More
  • CHUO KIKUU MKWAWA NACHO CHAFUNGWANa Francis Godwin, Iringa SIKU moja baada ya askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) mkoa wa Iringa kulazimika kutumia mabomu ya machozi kutuliza vurugu za wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE), uongozi… Read More
  • CHUO KIKUU CHA USHIRIKA NA BIASHARA CHATIMUA WANAFUNZIChuo Kikuu cha Ushirika na Biashara mkoani Kilimanjaro (MUCCoBS) kimewatimua wanafunzi 595 wa mwaka wa kwanza kutokana na kuanzisha mgomo chuoni hapo. Aidha wanafunzi hao pamoja na mgomo huo,wametuhumiwa pia kuhatarisha maish… Read More
  • WANAFUNZI CBE WAFUNGA MAGETIWanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dar es Salaam, wameamua kufunga mageti ya chuo hicho kuzuia uongozi wa chuo kuingia na kutoka baada ya Menejimenti kutotimiza ahadi ya kuongea nao, kutokana na mgogoro wa kufeli k… Read More

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget