Friday, 7 November 2008


Na John Daniel, Dodoma 

SERIKALI imeeleza kukasirishwa na gumzo la uvujaji wa mitihani na tatizo la vyeti visivyo halali na kuahidi kumulika upya kwa ukali zaidi Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na kuhakikisha tatizo hilo linakwisha. 

Akijibu maswali ya papo kwa hapo bungeni jana, Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, alisema ni aibu kwa Taifa kuzungumza kuvuja kwa mitihani mara kwa mara na kwamba analazimika kulizungumzia suala hilo kwa kuwa ni tatizo lililopo, lakini ni wakati muafaka wa kulikomesha. 

Katika swali lake kwa Waziri Mkuu, Mbunge wa Viti Maalumu, Bibi Magdalena Sakaya (CUF), aliitaka Serikali kutoa tamko kutokana na tatizo hilo, ambalo lililikumba Taifa hivi karibuni na kusababisha wanafunzi wa kidato cha nne kuahiroisha kufanya mtihani wa Hisabati. 

Pia Mbunge huyo aliitaka Serikali kutoa tamko akiihituhumu NECTA kwamba ndiye mhusika mkuu wa kuchapisha na kuuza vyeti bandia mitaani, jambo linalochangia kushusha kiwango cha elimu nchini. 

"Kwanza ni aibu sana kwa Taifa mitihani inavuja ni aibu kwa wazazi kununua mtihani mtaani, rai yangu kwa wazazi na Watanzania wote, tukatae tatizo hili, tumekubaliana na Waziri wa Elimu chombo chetu hiki NECTA lazima kiangaliwe kwa ukali zaidi,” alisema Bw. Pinda. 

Alisema licha ya mtihani wa Hisabati ulioandaliwa kwa ajili ya kidato cha nne mwaka huu kuvuja, lakini mitihani mingine haikuvuja na badala yake baaadhi ya watu waliibuka na kuuza makaratasi mitaani na kuvutia hisia za watu kwamba ndiyo mitihani halisi. 

CHANZO:
Majira

KUKASIRISHWA PEKEE NA KUINGALIA NECTA KWA UKALI ZAIDI PASIPO KUWAWAJIBISHA WAHUSIKA ITASAIDIAJE KUTATUA TATIZO HILI?

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget