Tuesday, 18 November 2008


Kwa mujibu wa gazeti la kila wiki la Changamoto,toleo la wiki hii,mahusiano ya kikazi kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii Bi Shamsa Mwangunga na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi Blandina Nyoni ni mabovu kiasi kwamba hawapiti mlango mmoja wa kuingilia na kutokea ofisini.

Kwa mujibu wa gazeti hilo,inasemekana chanzo cha uhasama huo ni tofauti za kimtazamo katika utendaji kazi ambapo mmoja wao anadaiwa kuzingatia taratibu na sheria katika utekelezaji wa majukumu yake huku mwenzie akitaka kupindisha kwa sababu anazojua yeye.

Uhasama kati ya vigogo hao unadaiwa kuanza nyuma kabla ya sasa kwani wakati flani wote walikuwa viongozi waandamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Maji Taka (DAWASCO).Inaelezwa pia kuwa uhasama huo umepelekea mmoja wao kuwa "anaingizwa mkenge" kwa kupewa taarifa feki za kuwapo kwa nyara za serikali na hivyo kulazimika kulipa dola 70 baada ya kukagua kontena na kugundulika kuwa halikuwa na nyara zozote.

Kumbukumbu zinaonyesha kwamba Wizara hii imekuwa na desturi za migogoro baina ya watendaji wake wakuu ambapo ilisharipotiwa huko nyuma kuhusu mgogoro kati ya aliyekuwa Waziri wakati huo,Anthony Diallo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Wanyamapori,Bw Severe,kisha "bifu" kati ya aliyekuwa Waziri,Prof Jumanne Maghembe na aliyekuwa Katibu Mkuu,Salehe Pamba.

SWALI LA KUJIULIZA,MIGOGORO HII SIO DALILI ZA MGONGANO KATI YA WAPINGA UFISADI NA WALEA UFISADI?JEURI YA WALEA UFISADI INATOKA WAPI?UFANISI UTAPATIKANA VIPI IWAPO WATENDAJI WAKUU WANAWINDANA KAMA PANYA NA PAKA?KWA STAILI HII MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YATAWEZEKANA KWELI?

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget