Bajeti ndio hiyo ishasomwa.Ila nimeonelea nami niiweke hapa.Isome hapo chini baada ja mjadala huu kiduchuTunaambiwa kuna maeneo takriban sita yaliyopewa kipaumbele katika bajeti hiyo.Naamini hata bajeti ya mwaka jana ilikuwa na vipaumbele vilevile lakini sote tunajua hali ikoje muda huu.Tatizo letu kubwa halipo katika kuainisha vipaumbele.Wala hatuna tatizo kuja na grand schemes zinazoweza kabisa kukuaminisha kuwa huenda sooner or later "maisha bora kwa kila Mtanzania yatakuwa sio tena slogan bali ukweli halisi".Tatizo la msingi ni kuvifanya vipaumbele hivyo viwe na maana,in the sense of kuvitafsiri kwa vitendo na si porojo.Sambamba na hilo ni namna vipaumbele hivyo vitakavyoweza kuruka vihunzi vya mafisadi.
Anyway,hilo sio la muhimu sana kwa sasa kulinganisha na uwezekano wa kufanikiwa kwa hizo tahadhari tunazoelezwa.Kwanza,yote yaliyoelezwa yanawezekana kwa sababu nia ipo,sababu zipo na njia zipo pia.Kinachoweza kukwamisha utekelezaji wa mpango mzima wa kunusuru uchumi ni ufisadi.
Nilitarajia bashasha zilizoambatana na bajeti hii zingegusia ishu ya ufisadi lakini wapi!Tuwe wakweli,hivi kuna uhakika gani kuwa hizo fedha zinazotengwa kwa ajili ya kufidiwa sijui watu gani hazitaishia kwa mafisadi?Ni muhimu kuuliza hilo kwa vile akina Kagoda bado wako huru uraiani na yayumkinika kuamini kuwa watashawishika kuchangamkia tenda hii ya "kunusuriwa na mtikisiko wa uchumi wa dunia."Simple logic ni kwamba kama waliweza kuiba bilioni 40 za EPA na taasisi husika zinaogopa hata kuwataja hadharani,kwanini safari hii wasikwapue tena fedha za umma kwa "njia halali"?
Naomba nitoe mfano hao katika kupigia mstari wasiwasi wangu kuhusu hatma ya hizo tahadhari tulizopewa kuhusu mtikisiko wa uchumi duniani.Hivi karibuni ulifanyika mheshimiwa mmoja aitwaye Peter Noni aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Benki wa Raslimali Tanzania (TIB).Uteuzi huu unaweza kuashiria ni kwa namna gani kelele dhidi ya watu wanaohusishwa kwa namna moja au nyingine na ishu za ufisadi zinavyopuuzwa.Jina la Noni limekuwa likitajwa sana kwa wanaojua undani wa ishu nzima ya EPA.Sasa sijui inamaanisha nini kumpeleka sehemu kama TIB,ambayo kwa hakika itapaswa kuwajibika ipasavyo kama tunataka tahadhari ya bajeti iwe na maana.Hii si ni mithili ya kumpa "teja" usimamizi ya stoo ya madawa?
Pasipo kudhibiti ufisadi na mafisadi,yayumkinika kuamini kuwa jitihada zote hizi zitaishia kunufaisha mafisadi na nyumba ndogo zao.Ni kweli kwamba Watanzania wengi wameonyesha umahiri mkubwa wa kukabiliana na hali ngumu ya uchumi na wameshazowea "kukaza mikanda kila wanapotakiwa kufanya hivyo" lakini hii inapswa iwe kwa Watanzania wote na si walalahoi pekee.Ikumbukwe kuwa mikanda hiyo imekuwa ikikazwa tangu wakati na baada ya Vita vya Kagera,na hatujawahi kusikia tamko kwamba WAKATI UMEFIKA KULEGEZA MIKANDA HIYO.Inwezekana kuwa tamko kama hilo halijatolewa kwa vile wakati huo (wa kulegeza mikanda) bado haujafika lakini inauma kuona kufunga mikanda kwa wengi kunatoa fursa kwa walafi wachache kufumuka vitambi (kiasi cha kushindwa hata kuvaa hiyo mikanda,let alone kuikaza) kwa matendo yao ya ufisadi.
Tuweke ushkaji pembeni,tuweke siasa za 2010 pembeni,tutambue kuwa mtikisiko wa uchumi ulimwengini ni kitu halisi na hata wafadhili wetu wanasumbuliwa nao.Tukiendeleza hadithi nzuri pasipo utekelezaji mzuri,tutajikuta pabaya.Tukumbuke kwamba tulikuwa masikini kabla hata ya huu mtikisiko wa sasa.Kinachotuweka pabaya kwa muda huu ni ukweli kwamba tofauti na huko nyuma,sasa hivi wafadhili wetu nao wana matatizo pia.Na kwa vile hakuna uhakika as to lini mtikisiko huu utapungua makali,ni vema pia tukatambua kuwa wafadhili hao wanaweza kutusahau kabisa ili waweze kumudu matatizo yao binafsi.
Inawezekana,only if kukiwa na dhamira thabiti pamoja na kuweka mbele maslahi ya nchi badala vikundi vya watu wachache.Na katika hilo,tayari kuna ishara isiyopendeza kwani waliofikiriwa katika stimulus plan ni wafanyabiashara (kwa maana ya taasisi na watu binafsi) pekee huku wakulima wakipuuzwa.Yet,tunaambiwa KILIMO KWANZA!I hope sio kilimo cha fedha za walipakodi kitachopelekea mavuno mwanana kwa mafisadi na kampeni zao za 2010!
Mungu ibariki Tanzania,na waadhibu pasipo huruma mafisadi wote.
BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2009/2010
0 comments:
Post a Comment