Tuesday, 16 June 2009


Ni dua pekee linaloweza kubadili viumbe wa aina hii.Sijui ni kujikomba,sijui uhaba wa tafakari au...!!!Soma kwanza stori hii kisha utafakari

Chenge asimikwa utemi

na Sitta Tumma, Magu

MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, ambaye amekuwa akiandamwa na kashfa mbalimbali, ametawazwa kuwa mtemi wa kabila la Wasukuma-Bagole, Kanda ya Itilima, wilayani Bariadi.

Chenge alichaguliwa katika sherehe maarufu za kabila hilo, maarufu kama Bolabo, mwishoni mwa wiki, wilayani hapa, ambazo mbali naviongozi wa kimila, Mkuu wa Mkoa, Abbas Kandoro, alikuwa ni miongoni mwa waliohudhuria.

Baadhi ya watu waliokuwepo kwenye sherehe hizo, waliuelezea utemi wa Chenge kwa mtazamo tofauti, huku baadhi wakidai kaupata ili kuweka mambo yake sawa, na wengine wakidai anastahili kupata nafasi hiyo kwa kuwa ni miongoni mwa watu wa kabila hilo.

Mbunge huyo ambaye alilazimika kujiuzulu nafasi yake ya uwaziri alisema, utemi huo ni karama aliyopewa na Mungu na kwamba wajibu huo ni sawa na daraja la kuunganisha jamii ya kabila husika.

"Utemi niliopewa naweza kusema ni karama iliyotoka kwa Mwenyezi Mungu! Kazi hii ya utemi ni nzito kwa sababu ina masuala yake yanayohusiana na mambo ya kimila pamoja na kuunganisha jamii ya kabila husika," alisema Chenge.




Ndio maana wakati mwingine hawa "wazungu" wanapata wakati mgumu kutuelewa.Hivi inaingia akilini kweli kwa mtuhumiwa wa ufisadi wa zaidi ya shilingi bilioni moja,Mzee wa Vijisenti Andrew Chenge,kutunikiwa utemi?Watoto wanaozaliwa leo na kesho na kukuta mtemi wao ni miongoni mwa watu waliochuma utajiri kwa njia za miujiza kabisa (fedha alizonazo haziwezi kuwa zimepatikana kwa njia halali,piga ua) watawaelewa kweli wazazi wao?

Mtemi wa nini?Au wanamaanisha utemi wa kuifanya sheria imwogope?Maana kesi yake ya kuua ni vituko vitupu.Mara iundiwe tume,mara iahirishwe kwa hili na lile!Mtu kasababisha ajali huku gari ikiwa na bima iliyoisha muda wake,mnamuundia tume ya nini?Na kwanini hiyo tume iwe kimya kama haikuundwa vile?

Mtuhumiwa huyu wa ufisadi ameendelea pia kuwa kwenye kamati ya maadili ya CCM.Halafu ukisema CCM chama cha kifisadi kuna waungwana wananuna!

Kaaazi kwelikweli

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget